uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Tetesi: Uchaguzi wa CHADEMA,Kuna uwezekano Lissu akakosa Bara na Pwani Umakamu mwenyekiti na uwenyekiti

    Katika uchaguzi ujao wa Chadema, kuna dalili kwamba Tundu Lissu huenda akakosa nafasi za uongozi bara na pwani, hasa (katika nafasi za umakamu mwenyekiti na uwenyekiti.) Hali hii inatokana na changamoto mbalimbali zinazokabili chama hicho, ikiwa ni pamoja na mpasuko wa ndani na ushindani mkali...
  2. PreGE2025 Masaa 48 ya Mbowe kuamua hatma na uelekeo wa chadema kuelekea uchaguzi mkuu 2025

    Ni wazi kauli ya mbowe inayosubiriwa kwa hamu na gamu kubwa sana na wana chadema na taifa kwa ujumla, atakayoitoa mbele ya waandishi wa habari, ndani ya masaa 48 yajayo, itaamua mustakabali, uelekeo na myukano wa kisiasa wa aina ya kitofauti mno ndani ya chadema kuelekea uchaguzi wa ndani ya...
  3. Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Majibu ya kitendawili cha 'Governor's Dilemma' yanamkweza Tundu Lissu na kuwashusha Mbowe, Samia na Hussein Mwinyi

    "Hata alipokwisha kunena, Yesu alimwambia Simoni Petro, twika mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi...
  4. B

    PreGE2025 Mtego unaowakabili chama cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi wa 2025

    Hello! Natumai mu wazima! Nchi ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni yetu sote watanzania ila kitu kibaya kuna baadhi ya kundi dogo la watu kuona nchi hii ya Tanzania inapaswa kuwa mali yao binafsi. Hilo ni kosa kubwa kwa chama tawala kudhani wao ndio wanapaswa kutawala nchi hii miaka yote...
  5. LGE2024 Askofu Pisa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa kama 'Mchezo Mchafu'

    Maaskfu kutoka Madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini wamekutana leo, Jumatano Desemba 18.2024 katika ukumbi wa Kurasini Conference and Training Center uliopo makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), jijini Dar es Salaam Maaskofu hao pamoja na wadau wengine wa...
  6. Naibu Waziri TAMISEMI apongeza watumishi wa TAMISEMI kwa kuendesha Uchaguzi kwa haki. Asema malalamiko ni kawaida

    Wakuu, Wiki chache baada ya kumalizika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI )Dkt. Festo Dugange amewapongeza watumishi wa TAMISEMI kwa kusimamia Uchaguzi vizuri Dugange amesema kuwa pamoja na malalamiko yaliyokuwepo...
  7. S

    Tundu Lissu nisikilize, upepo wa kisiasa uko kwako 100% lakini mkakati wa kuibiwa kura umeshaanza kusukwa, jiandae

    Mimi sio mwanachama wa Chadema na sifurahii siasa zao za kutukana tukana viongozi hivyo hasa vijana wao wanavyofanya harakati za kijinga mitandaoni jambo linalosababisha wawaudhi viongozi wa serikali na ndio maana wanakamatwa kamatwa hivyo lakini najaribu kulinganisha sifa za uongozi kati ya...
  8. Mbeya: Viongozi walioshinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa warudisha fadhila kwa wananchi

    Wakuu, Viongozi wa mtaa wa Masewe na Ilemi kutoka mkoani Mbeya,Patrick Mwashuma na Lupakisyo Mwasasu, wamefanya hafla ya kuwashukuru wananchi wa kata hizo kwa kuwapigia kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, uliofanyika Novovemba 27.2024. Katika hafla hiyo iliyofanyika leo kwenye viwanja...
  9. M

    Kuelekea kutafuta Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi, maoni yangu ni haya

    Ndugu zangu Watanzania, nimeona nitoe maoni yangu machache tunapoelekea kutafuta Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi. Mimi nilidhani tufanye yafuatayo:- 1. Kiundwe chombo cha kitaifa kitakachoongoza na kuratibu hii movement. - Chombo hiki kitokane na angalau Watanzania wa makundi...
  10. PreGE2025 Ratiba Kamili Ya Uchaguzi Wa CHADEMA Taifa

    Ratiba Kamili Ya Uchaguzi Wa CHADEMA Taifa. Katibu Mkuu anawatangazia wanachama wote kuwa kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Chama na Mabaraza kwa ngazi ya Taifa utakaofanyika Januari, 2025. Fomu za kuomba kugombea nafasi za uongozi ngazi ya Taifa zinapatikana ofisi za Makao Makuu ya Chama...
  11. Swali la Siku:Jambo gani wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 unahisi halikuwa la Kweli?

    Novemba 27, 2024, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulifanyika, ukiambatana na matukio ya aina mbalimbali, yaliyokuwa ya Kweli, huku mengine yakitia shaka kuhusu Uhalisia wake. Mdau, je, ni jambo gani hasa, kuanzia hatua ya kutangaza nia kwa wagombea hadi mchakato mzima wa uchaguzi, unahisi...
  12. PreGE2025 Naibu Katibu Mkuu CHADEMA: Bila mabadiliko, 2025 hakutafanyika Uchaguzi wowote

    Wakuu, Akiongea hivi karibuni katika mdahalo maalum ulioandaliwa na Jamii Forums pamoja na Star TV, Benson Kigaila ambaye ni Naibu Katibu Mkuu CHADEMA amesema kuwa sio kwamba CHADEMA itasusia uchaguzi ujao bali uchaguzi huo unaweza usifanyike kabisa, Kigaila amesema kuwa bila mabadiliko ya...
  13. Mbowe hana mpango mkakati mpya wa mabadiliko kwa uchaguzi wa 2025.

    CHADEMA mkimchagua Mbowe awe mwenyekiti tena tegemeeni uchaguzi wa 2025 kuwa kama wa 2024, 2020 na 2019. Mbowe hana mbinu mpya au hamasa ya kushawishi mabadiliko ya uchaguzi 2025, Lissu ndio mtu sahihi wa kuongoza na kuleta mabadiliko mwakani. Mbowe alifaa kuwa mwenyekiti enzi za JK ila sio...
  14. Kwenye Uchaguzi Huu CHADEMA hatuna cha kujifunza kutoka CCM

    Chadema inacheza katika kiwanja cha Demokrasia kiwanja ambacho CCM haiwezi kuingiza team uwanjani, Chadema imeshikilia kurasa zote za mbele za vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi juu ya uenyekiti wa chama. CCM ni wageni wa mashindano haya ya Demokrasia ukiona wanashangilia usiwashangae...
  15. S

    Jicho la tatu: Tundu Lissu unaweza kukabiliwa na assassination attempt nyingine wakasingiziwa CHADEMA kiwa hoja ya maswala ya uchaguzi ndani ya chama

    Tundu Lissu, wewe kwa sasa ndio tishio kubwa sana kwa watu wa chama fulani na mgombea wao mtatajiwa wa uchaguzi mkuu wa mwakani. Hivyo, nakushauri uwe makini sana katika mienendo yake yote kwani wanaweza kukufanyia jambo lolote baya na wakasingia chama chako ndio kimehusika kwa hoja ya vuguvugu...
  16. Tetesi: Huenda uchaguzi wa CHADEMA wa taifa ukaahirishwa hadi baada ya uchaguzi mkuu october 2025

    Inasemekana, barua inayelezea kinagaubaga sababu mahususi za msingi za kuahirishwa kwa uchaguzi huo wa ndani Chadema, tayari imewasilishwa na kupokelewa kwenye taasisi mahususi, inayohusika na masuala ya vyama vya siasa nchini. Haijafahamika bado ikiwa wajumbe wahusika wa uchaguzi huo wa...
  17. Uchaguzi kwenye taasisi una kanuni na taratibu zake, Ni jambo nyeti. Huweza sambaratisha tasisi. Jee alichofanya Lissu ni sahihi?

    Uchaguzi wa viongozi wa vyama vya siasa na wale wa serikali una sheria, kanuni na taratibu zake ambazo zisipozingatiwa huweza kusababisha vurugu na kusambaratisha chama au nchi. Kwa ujumla taratibu ziko hivi: 1. Siku na mwezi wa uchaguzi hujulikana mapema. Ni miaka mitano baada ya uchaguzi...
  18. Uchaguzi ni sayansi: Lissu anaenda kugaragazwa vibaya sana na Mbowe

    Tundu Lissu ni baba aambiliki nilimuonya hapa majuzi aache mission yake ya kukiua chama hajataka kusikia. Sasa anaenda kufundishwa adabu na bingwa wa sayansi ya siasa za upinzani Aikael Mbowe. Kelele ni nyingi mtandaoni lakini hazitomsaidia Lissu na kichapo cha mbwa mwizi toka kwa Mbowe...
  19. PreGE2025 Lissu aendelea kupanga safu yake kwa ustadi mkubwa. Anaumaliza uchaguzi mapema sana

    Lissu hapoi wala haboi, ameendelea kuipanga safu yake na jana usiku nyumbani kwake alikuwa na kikao kizito na wajumbe wa mkutano mkuu kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ambao hawakutokea kwenye press yake kwa sababu ambazo zipo kapuni. Awa ni wale wanaingia kama wapiga kura kwenye uchaguzi wa nafasi...
  20. LGE2024 Mwenyekiti wa CHADEMA Dodoma aliyekimbia na daftari wakati wa Uchaguzi aripoti Polisi

    Wakuu, Mnakumbuka yule Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Dodoma ambaye siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa alikimbia na daftari la wapiga kura akidai kuwa kuna hujuma zimefanyika? Inaonekana sasa "watu wa system wameanza ku-deal nae. ========================================================...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…