Maji huku Mwanza imekuwa ni kero kubwa sana, wanachuo tunaishi kwa tabu sana tunapata shida kubwa ya maji ilihal tuko karibu na ziwa Victoria
Sijui mnatusaidiaje kuepukana na hili. Tunalipia bili za maji kwa wakati lakini bado maji kuyapata ni changamoto.
Ni siku ya 4 sasa maji hayatoki
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam(DAWASA) @dawasatz Mhandisi Mkama Bwire amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kinondoni kufikia asilimia 97%.
Akizungumza katika Kikao Kazi cha DAWASA na...
Mh Rais Samia Suluhu Hassan
Nakusalimia kwa Jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Awali ya yote nianze kwa kukutakia uzima na afya katika kutekeleza majukumu yako.
Baada ya salamu hizo nije katika ujumbe ninaokusudia kukuandikia.
Ni hivi ndugu Rais, WANANCHI HATUNA MAJI YA UHAKIKA na...
Hadi leo Januari 21, 2025, maeneo ya Isyesye hapa Jijini Mbeya haujapata maji kwa wiki moja sasa, tumetoa taarifa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA UWSA) lakini hatuoaji majibu yanayoeleweka.
Hii sio mara ya kwanza, kila inapotokea kunakuwa na ugumu kwa kupata majibu...
Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, amewaasa wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuacha kuzoea shida za wananchi, na badala yake kuzitafutia ufumbuzi ili wananchi wapate huduma ya Majisafi ya uhakika.
Waziri Aweso amewaasa wafanyakazi hao wakati wa Mkutano...
Sisi Wananchi wa Kijiji cha Unyianga kilichopo Kata ya Mtamaa, Manispaa ya Singida tunalia kukosa huduma ya maji safi, ni miaka kadhaa sasa tangu ‘Danganya Toto’ ya kujengewa Tenki la Maji na kuwekwa mabomba ifanyike lakini hadi leo hatujawahi ona maji yakitoka.
Tulijengewa tenki la maji na...
Ni karibu mwezi sasa maji ya dawasa yanatoka kwa machale maeneo ya kimara.
Yaani, yanatoka kwa masaa 24, baada ya hapo hayapo mpka baada ya siku tatu ndio yanatoka tena.
Mfano mara ya mwisho mabomba kutiririsha maji ni siku ya jumanne, hadi leo hakuna kitu.
Na hii hali ina karibia mwezi sasa...
Mimi Mkazi wa Geita kwa muda mrefu sasa mkoa wetu umekuwa na changamoto ya mgao wa maji.
Maji yamekuwa yakitoka mara moja kwa wiki. Hii ni kwa Mtaa wetu na maeneo mengine mengine.
Kila tukiuliza shida ni nini viongozi wetu wamekuwa wakitoa visingizio. Kila mara wamekuwa wakisema kuwa wapo...
Mapato yanayopatikana kwenye malipo ya maji si yangeboresha upatikanaji wa maji, na kama inawezekana wafanye utafiti wa kuchimba visima vikuu vya kila wilaya kuliko kusubiri maji ya mto Ruvu maana maji tunayachota yana chumvi nyingi hayafai kwa afya ya tumbo
Kama ilivyo kawaida, inapofika miezi ya 9, 10 na 11 Shida ya maji huwa kubwa katika jiji la Dar es salaam. Cha ajabu jili jambo lipo kwa miaka nenda rudi, lakini Serikali hii dhaifu ya CCM, isiyojielewa, iliyoshindwa kusolve ishu za msingi kama maji halafu inadhani bado ina legitimacy mbele ya...
Hii ni dhahiri kuwa hayupo serious na maisha ya wananchi. Zaidi ya kampeni za chinichini alizoanza kwa kulaghai wananchi ili wajazane kila anapopita.
Mradi wa Kidunda una umuhimu sana kutatua shida za maji kwa mkoa wa Morogoro. Nilitegemea kiongozi makini aombe msamaha kwa kutotekeleza mradi...
Ndgu waandishi wa habari,
Wizara hii ina historia kubwa. Iliwahi kushikwa na wakubwa na watu maarufu.
Haijawahi kuboronga. Haijawahi kutokea migongano ya kimaslahi. Kwa maana hiyo haijawahi kuwa maji yapo na wananchi wanahangaika kwa sababu za kisiasa wakakosa maji.
Hili jambo sasa lipo.
Katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya wananchi serikali ina husika moja kwa moja kuhakikisha watu/wananchi wake wanapata maendeleo endelevu.
Huku wananchi tukiwa tunajitutumua kuhakikisha tunaishi vizuri, ni vyema serikali nayo ikatoa kwa ubora huduma za msingi kwa wananchi wake...
Kumekua na tatizo la maji kwa zaidi ya wiki sasa maeneo ya Kimara Temboni kwa Msuguri.
Taarifa zilizopo ni kuwa kumekuwa na tabia chafu ya watumishi wa DAWASA kuchepusha maji kwa nia ya kufanya biashara na kujiingizia kipato.
Shida ya maji imejitokeza tena kipindi hiki ambapo eneo kubwa la...
Group limeundwa na watu wa DAWASA wenyewe cha ajabu hawasikilizi shida za wananchi.
Mh. Waziri anahangaika huku na kule lakini wafanyakazi wa DAWASA wachache wanafanya masihara na maisha ya wananchi.
Rais anahangaika huku na kule kuna wapuuzi wamekaa kwenye kiyoyozi wanashika videvu.
Mh...
Malamba Mawili maji ni ya mgao yanaweza maliza wiki 2 bila kutoka na yakitoka yanatoka usiku wa manane yakitoka kidogo kidodo, yanachirizika hayana kasi hata kidogo kiasi ambacho baadhi ya watu ambao nyumba zao zimepo kwenye miinuko kidogo maji hayafiki kabisa.
Kuna baadhi ya watu wana miezi...
Wana morogoro maeneo ya manyuki mwisho tuna teseka na Maji ya Serikari Maana kuna mambomba lakin maji yana toka jumanne tu kila Week
Licha ya kutoka mara 1 bado yanakuwa hayana nguvu kiasi kwamba yanashindwa kupanda kwenye Matenki na kutulazimisha kubebelea Ndoo na Madumu
Sasa hii imekuwa...
Mimi kama mama. Naomba waziri waa mbie waache visa vyao, wanapogombana wao kwa wao anayeumia ni mama. Wasichana wadogo wanabakwa, wakinamama tunadhalilika. Jamani tuoneeni huruma mpate uongofu wa Mungu.
Hawa watu waache kumtesa mwanamke. Imetosha baasi.
Haiwezekani nadamka asb kuchota maji...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.