Mwenge wa Uhuru una muundo wa tochi ya mafuta ya taaambayo inaashiria uhuru na mwanga. Mwenge wa uhuru ulinyanyuliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 na shujaa Brigedia Alexander Nyirenda ikiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki.
Sababu ya huyu brigedia kunyanyua mwenge huu ni kuonesha fahari ya nchi na pia kuleta matumaini kwa Watanzania wote kwa kutokata tamaa, kupendana, kuheshimiana na kutogombana ikimaanisha kuwa na ushirikiano.
Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka kuanzia maeneo mbalimbali nchini.
Wanabodi, kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, huzungukia maeneo mbalimbali ya nchi yetu kushuhudia haya na yale.
Leo nimepata fursa kushuhudia shamra shamra za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Dodoma.
Jana Mwenge ulilala Kijiji cha Mwitikira Wilaya ya Bahi. Mambo niliyoyaona usiku wakati wa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.