chadema

CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.

Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
  1. Z

    JamiiForums Tanzania No reforms No Chadema.

    No Reforms No Chadema. Uchaguzi Mkuu uko palepale, Mwezi Octoba 2025. Vyama zaidi ya 17 Vitashiriki, watanzania wote wanajiandaa kuwachagua viongozi wao hiyo October.
  2. JamiiForums Tanzania LGE2024 Jionee tofauti kati ya Mikutano ya CCM na ya CHADEMA iliyofanyika eneo moja la Kariakoo

    Mungu fundi sana! Polisi wakiendelea kutumiwa vibaya na CCM ambao wanawanyonya na kuwafanya waishi maisha magumu leo wamezuia Mkutano wa Chadema uliopaswa kufanyika pale Kariakoo Angalia picha hapa chini👇 Cha kufurahisha zaidi Polisi hawahawa wamekuwa wanawaruhusu CCM kufanya Mikutano eneo...
  3. JamiiForums Tanzania Chadema waacheni Watanzania wataamka wenyewe kujipambania

    Huwa nawaonea huruma kuwapigania Watanzania wapumbavu hii ni sadaka kubwa wanajitoa chadema Nina uhakika mtoto wa Lissu haki chini Mke wa Lema hakosi matibabi ya kujifungua Heche hakosi maji ya kunywa Wananchi wana matatizo makubwa wanaowapigania wanawaona kama wajinga Shule hakuna madawati...
  4. JamiiForums Tanzania Lema anatakiwa aelezwe Simba na Yanga ni zaidi ya CHADEMA

    Lema akitaka kuhakikisha Simba na Yanga ni zaidi ya CHADEMA aombe polisi wamchukue Hersi au Mo dewji kama wataweza si kama viongozi wa CHADEMA wanachukuliwa kindezi mbele ya wafuasi wao.. Soma Pia: Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja Wajaribu kuchukua kiongozi wa...
  5. R

    JamiiForums Tanzania Mbunge wa Chadema??? asema" Shida iko wapi referee akiwa Neutral? msikilize

    4R za Rais Samia ndizo chadema wanajaribu kuzitekeleza. REFORM
  6. JamiiForums Tanzania PreGE2025 John Mrema: CHADEMA imeua ndoto za waliotaka kugombea, mpaka 2030 sina uhakika kama tutakuwepo

    Wakuu, Akiwa anazungumza leo, John Mrema amesema kuwa CHADEMA imeua ndoto za wanachama wengi waliotaka kugombea kwenye Uchaguzi ba kuongeza kuwa hana uhakika kuwa kama chama hicho kitakuwepo hadi kufikia mwaka 2030 "Jambo la pili ni chama chetu kutosaini kanuni za maadili ya uchaguzi na...
  7. JamiiForums Tanzania CHADEMA wafukuzeni G-55 mara moja, kama ambavyo CCM walimfukuza Mzee Malisa kwa kuhoji úhuni wa Dodoma, halafu tuone Mahakamani watakakokimbilia.

    Mzee Malissa alifukuzw CCM bila hata kuitwa na kujitetea, na Alifukuzwa sababu tu kahoji Uhuni ulotokea DODOMA. Hawa G-55 wanachofanya ni kutafuta Kufukuzwa, ili WAKIMBILIE Mahakaman, Cha kiwe na Kesi mara Kwa mara. Kwa Bahati Mbaya, mshauri wao ni kakikundi kadogo ka Dola na CCM na ambao...
  8. JamiiForums Tanzania John Mrema, sawa Tume Iko sahihi, kinachokuwasha nini? CHADEMA haingii uchaguzin bila Mabadiliko, hatuna Mpango huo !!.

    Mbona kama wee Mrema na Genge lako ndio mmeumia Kwa CHADEMA kutokusaini? CHADEMA ingeutaka uchaguzi huo , pasingekuweponna NORENE na Ingesaini Kanuni za TUME. Kinachokuuma nini?? Kwamba Unafurahi Msimamo wa Tume? Au Unatumia Kwa Msimamo wa CHADEMA ??. Kama kugombea, Hamia CCM, utagombea pia !!
  9. H

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 John Mrema atetea Maamuzi ya Tume ya Uchaguziji dhidi ya CHADEMA

    John Mrema, kwenye conference yake ya leo na wanahabari, kwa mtu ambaye hamjui, angedhani ni msemaji wa Tume ya ucjaguzi. Wale waliokuwa na mashaka na G55 unayoongozwa na John Mrema, leo wamepata jibu la wazi. Katika kikao chake na vyombo vya habari, Mrema ametumia muda wake mwingi kuonesha...
  10. M

    JamiiForums Tanzania Kwa hali hii hata CHADEMA hawatakubali

    1. Posho za wabunge 2. Posho na mshahara na maslahi ya Rais 3. Posho na maslahi ya mawaziri 4. Maslahi ya jaji mkuu 5. Spika na naibu wake 6. Wakurugenzi Kawaida Afrika akiingia mpya au chama kipya mfumo wote wa uongozi unabadilika. Mfano chadema ya Lissu , team Mbowe wote wanakula upepo na...
  11. JamiiForums Tanzania PreGE2025 UVCCM Tanga: CHADEMA amueni kushiriki Uchaguzi au la, si kuchochea vurugu

    Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga ndugu Ramadhani Ally Omary (Somo) amewataka viongozi wa chama cha maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kuwa na msimamo kwa wanachokitaka kama kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu au kutoingia. Mwenyekiti wa vijana amewasihi...
  12. M

    JamiiForums Tanzania Mbona CHADEMA baada ya uchaguzi walimtenga Kibatala? Hapa wamekosea

    Mkurugenzi na mwanasheria wa chama kwa sasa hawana mvuto ndani ya nje ya chama. Licha ya mwanasheria kuwa Phd from Havard University lakini ukweli katika kesi za kisiasa haziwezi. Uwasiliwashaji wake mbele ya jamii sio mzuri Sijui kwanini walimtenga kibatala ktk uongozi wa CHADEMA Kibatala...
  13. JamiiForums Tanzania PreGE2025 Rai Kwa Watawala: Acheni kupotezea watu muda—Iacheni CHADEMA ifanye shughuli zake kwa Uhuru; Otherwise, Ifuteni Kwenye Register ya Political Parties!

    Kisheria, chama chochote cha kisiasa ni legal entity. Kinaweza kufungua au kufunguliwa mashitaka kwa jina lake chenyewe (in its own right). Hivyo, ni upumbavu mtupu kuwakamata viongozi wa chama cha kisiasa (in their individual capacities) kwa official acts zao. “No Reforms, No Elections” ni...
  14. JamiiForums Tanzania Maslahi ya Katibu Mkuu CHADEMA

    Katibu Mkuu CHADEMA anastahili zifuatazo kwa Cheo chake, 1. Mshahara 7m TZS/mwezi (take home). 2. Usafiri/Gari SUV (4WD), dereva na posho ya mafuta. 3. Kutumia VIP Lounge akiwa airport. 4. Posho za safari nje na ndani ya nchi. **Sasa jichanganye bodaboda eti unaenda kwenye kesi ya Lissu wakati...
  15. M

    JamiiForums Tanzania Ndugu zangu CHADEMA juu ya madiliko haya kwa taifa la Marekani juu ya Afrika hata viongozi wa dini hawatasaidia zaidi ya kuweka tu

    Siasa Trump afikiria kupunguza balozi za Marekani barani Afrika Saleh Mwanamilongo Saa 2 zilizopitaSaa 2 zilizopita Marekani inapanga kupunguza kwa kiasi kikubwa mwelekeo wake wa kidiplomasia barani Afrika na pia kufuta ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje zinazoshughulikia mabadiliko ya hali ya...
  16. JamiiForums Tanzania PreGE2025 Songea: Viongozi watatu CHADEMA, Mwimbaji nyimbo za chama na Wanachama wawili wakamatwa na Jeshi la Polisi

    Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Kusini kimesemea viongozi wake watatu, mwimbaji nyimbo za chama na wanachama wawili wameshikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Songea Mjini. Taarifa ya awali iliyotolewa leo Aprili 21,2025 na CHADEMA makao makuu, imewataja viongozi hao kuwa...
  17. JamiiForums Tanzania PreGE2025 Bodaboda, Bajaji na Wajasiriamali Dar wagomea maandamano CHADEMA

    Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waendeshaji Bajaji, Bodaboda na Wajasiriamali Jijini Dar es Salaam wametangaza kutoshiriki maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yaliyopangwa kufanyika Aprili 24, 2025, kuelekea Mahakama ya Kisutu, ambako kesi ya Mwenyekiti wa...
  18. JamiiForums Tanzania Nani anaiharibu amani ya Tanzania ni Tundu Lissu wa CHADEMA au ni viongozi wa serikali ya CCM kwa maslahi yao binafsi?

    Katika hali isiyo ya kawaida kumekuwepo na sintofahamu ya kukamatwa Mwenyekiti wa Chadema Mh. Tundu Antiphas Lissu na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, swali ni je? nani anaharibu amani ya taifa letu Tanzania, anayetumia nguvu na kusisitiza uchaguzi uende anavyotaka yeye au yule Lissu anayesema...
  19. JamiiForums Tanzania Maaskofu kugeuza Ibada ya Pasaka kama jukwaa la kuisemea CHADEMA ni kujitoa ufahamu, mlikuwa wapi wakati Lissu anazungumza lugha za uchochezi?

    Friends and our Enemies, Kama kawaida yao, maaskofu wameendelea na maigizo yao ya kujifanya kuwa wao Wana uchungu zaidi na nchi hii kuliko viongozi wowote wale wa dini. Kinachoshangaza Episodes hizi hujirudia rudia zama baada ya zama,TENA hususan Kiongozi pale juu anapokuwa mfuasi wa Allahu...
  20. S

    JamiiForums Tanzania Marekani wanaweza kupitia CHADEMA

    Kila kitu wao wanaisifia Marekani ,wakati Nchi nyingi za Africa sasa zimeamka ,Hata Tanzania tumeipiga na chini Marekani. Hila za Mkoloni huyu huwatumia au kuvitumia vyama vya siasa na kuwarubuni ,tuseme huwaweka kama vibaraka. Na Chadema ni rahisi sana kurubuniwa na tumeona utayari wao wa...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…