Kiukweli mimi sio mtu wa kuonyesha haya 'makea artificial' kwa mke wangu, nikizingatia kuwa akiyazoe ntakuwa 'sina jipya' alafu atanchoka.
Sasa siku moja tulitinga harusini na my beloved wife, na kwa kuwa siku hiyo tuliunganisha functions, tulifika tukiwa tumechelewa kidogo. Ile kuingia ukumbini tukakuta inaporomoshwa misebene ya nguvu, na kwa kuwa sisi ni 'walevi' wa sebene, tulichofanya tuli-identify meza ya kukaa, tukakuta moja waliokuwa wamekaa famili friends wetu ina nafasi, wife akakabidhi kimkoba tukajimwaga jukwaani kusakata muziki. Tuliunganisha sebene kama tatu, kwa bahati mbaya kiatu kimoja cha mke wangu kikafyetuka soli, ikalazimika tukakae. Tulipofika tukakuta wale wenzetu pale mezani na meza za jirani wameshaenda kuchukua msosi pamoja na waliokuwa meza za jirani ambao wengi walikuwa office mates.
Kwa hiyo ikabidi kwenda kuchukua chakula, but kwa kuwa mke wangu kiatu kilishafyatuka, (watu walikuwa hawajagundua), nikamwambia "Kaa tu mamaa, umechoka, ngoja nikakuletee msosi"... Binafsi niliisema tu ile sentensi kiutani kwa kujua kuwa hataweza kwenda kuchukua chakula na kiatu chake kile. Kumbe nilipoenda huku nyuma nikaacha gumzo kwa watu wakifagilia 'nilivyo na makea'... kwamba ninavyomjali mke wangu nimeenda kumchukulia msosi..., kwamba kwa kuwa alikuwa amecheza amechoka (kweli mke wangu anayarudi masebene (ila hanizidi... ata ye anajua)), eti nimemuacha apumzike.. Niliporudi pale na sahani zangu mbili nikashangaa 'hongera' zinamiminwa kutoka kwa watu kadhaa, mi nikadhani ni kutokana na umahiri wa kusakata sebene. Naweza kusema lile tukio la kufyatuka kiatu lilinisababisha nikapewa misifa ambapo baadhi ya watu hasa office mates waliendelea kunichukulia hivyo (mtu wa makea) hata baada ya harusi. Ilikuwa haina tofauti na jinsi bao la mkono la Henry lilivyoipeleka France Sauz mwaka 2010...