Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 60,039
- 135,299
Wanabodi,
Kiukweli kitendo cha VP Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi kufutwa uanachama CCM, kimenipiga bonge la shock la mwaka na kunikata kabisa usingizi! ukijumlisha na kule kujiuzulu kwake, this is a double tragedy!.
Sijui kama kuna mtu yeyote amempongeza Dr. Nchimbi kwa uamuzi wake huu wa kishujaa wa kuamua kujiuzulu, ambao mimi nauita ni uamuzi wa kishujaa mkubwa, ila hili la kufukuzwa CCM, nalo halijakaa vizuri, kwasababu japo CCM inaweza kumfukuza uanachama mwanachama wake yeyote, ila ikitokea mwanachama huyo ni rais wa JMT, makamu wa rais, au spika wa Bunge, Viongozi hawa wana kinga ya katiba ya kutoshitakiwa popote, hivyo japo wamechaguliwa kwa ticket ya CCM, baada ya kuchaguliwa rais, VP na Spika, CCM haina uwezo wa kumfukuza kazi rais wa JMT, VP au Spika!, hivyo kufutwa uanachama wa Nchimbi, hakuathiri, u VP wake, hivyo uapisho wa VP mpya huku VP mstaafu hajakabidhi ofisi ni kinyume cha katiba ya JMT!.
Ushauri wangu wa bure kwa CCM, serikali yetu, kwa vile taifa hatujatangaziwa makosa yake, naomba makosa hayo yasifute mema na mazuri yake yote, aliyoitendea CCM, serikali, Tanzania na Watanzania.
Najua kesho/keshokutws
ubalozi wao pia utaondoka, na baada ya kufutwa uanachama wa CCM, ule umakamo wa rais wa hadi September 4 hauwezi kufutika kama alivyosema yule kilaza!, CCM haina mamlaka kumfuta kazi VP wa JMT!.
Lengo la bandiko hili, kwanza ni kumpa pole kwa maswahibu haya makubwa hivi ila pia kumpongeza kwasababu uamuzi huo ni kama amefuata ushauri wangu huu
Humo nilishauri
Hebu imagine tukio vifo vya mahabusu 4 tuu mikononi mwa polisi ile 1976, kuanzia Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, Rashidi Kawawa alishushwa cheo kuwa Waziri asie na wizara maalum.
Waziri wa mambo ya ndani, Ali Hassan Mwinyi aliwajibika kwa kujiuzulu.
Waziri wa usalama wa taifa Peter Siyovelwa aliwajibika kwa kujiuzulu
IGP Samuel Pundugu aliwajibishwa kwa kustaafishwa kwa manufaa ya umma
DGIS Emelio Mzena aliwajibishwa kwa kustaafishwa kwa manufaa ya umma
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Peter Kisumo alitenguliwa,
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mabawa alitenguliwa,
RPC, RSO, OCD, DSO wa Mwanza na Shinyanga wakipandishwa kizimbani Kesi ya Mauaji Mwanza na Shinyanga zikarindima.
October 29, wamekufa watu 518 lakini hakuna mtu yoyote aliwajibika!, ndio maana nasema kitendo cha Dr Nchimbi kuwajibika, kinastahili Pongezi za dhati!.
Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi, hii ni ajali ya kisiasa, ni ajali tuu kama ajali nyingine yoyote inaweza kusababisha majeraha, majeruhi na hata kifo, wewe sii wa kwanza na wala sii wa mwisho, hata Ali Hassan Mwinyi alipataga ajali akawajibika ile 1976 akaja kuwa rais wa JMT. Edward Lowassa alipataga ajali akajeruhiwa, Bernard Membe alipataga ajali akajeruhiwa, there is life besides politics. Yule YEYE ambaye ni mpangaji wa yote anaweza kulifanya hata lile Jiwe walilolikataa waashi wa CCM, likafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!.
Pole sana Emmanuel Nchimbi kwa kusimama na unachokiamini, Mungu akubariki, akupiganie!
Kama umeadhibiwa kwa kosa la kuwashauri Watanzania wapiganie katiba, then lipokee kwa mikono miwili kisha utashuhudia jinsi karma itakavyo washughulikia watu...!
Mungu Ibariki Tanzania.
Mzee Pasco

Karibu, Nipashe ya leo
Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni waumini wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, hivyo sii wengi wanaijua "karma" ni nini, kwasababu "karma" ni neno la lugha ya ki Hindi "Hindu" na linafundishwa kwenye dini ya Hinduism na Buddhism, mimi nilijifunza kuhusu "karma" wakati nikiishi jiji la New Delhi nchini India.
Huu ni wito kwa viongozi wetu, unapokosea hata kwa kujikwaa tuu ulimi, tujenge tabia ya kuwajibika kwa makosa yetu, tujitokeze kuomba radhi, na ikibidi kuwajibika!.
Kwa vile mimi ni mtu wa mastory story, na sii watu wote ni wapenda...

- Pascal Mayalla
- dhamana karma kupisha kuwajibika msamaha mzigo ombi utamaduni viongozi wito
- Replies: 41
- Forum: Jukwaa la Siasa
Hivyo hiki alichofanya VP Dr. Nchimbi cha kujiuzulu kwa heshima baada ya kupishana kauli na mamlaka yake ya uteuzi ni sifa adimu sana kwa ya uongozi kwa viongozi wetu wa sasa, ila huku kufukuzwa uanachama wa CCM, kama bado ana political ambitions, huenda kufukuzwa huku ni blessings in disguise ili litimie lile neno la mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM!.Wanabodi,
Huu ni wito kwa viongozi wetu, unapokosea hata kwa kujikwaa tuu ulimi, tujenge tabia ya kuwajibika kwa makosa yetu, tujitokeze kuomba radhi, na ikibidi kuwajibika!.
Hitimisho
Ni lini uwajibikaji kwa viongozi wa umma utarejeshwa kwa kiwango cha uwajibikaji wa enzi za Mwalimu?. Yaani kiwango cha uadilifu wa mke wa Kaisari?. Kiongozi wa umma ni mpaka afanye kosa kubwa kiasi gani ndipo awajibike?.
Wito kwa Viongozi Wetu
Viongozi wetu, cheo ni dhamana, ikitokea ukatuhumiwa tuu, tuhuma za wazi, hata bila uthibitisho, ama kanusha ama wajibika, hata mkapishana tuu kauli na mamlaka yako ya uteuzi, ukiona tuu hamko wamoja, jikalie pembeni, usisubiri kuwekwa pembeni!, msimponze bure mama yetu Samia kwa kumtwisha mzigo wa karma zenu, kama mlivyomponza yule mwingine na karma ikafanya mambo yake!.
Ukibebwa kwa mbeleko bebeka kwa kujiachia, lakini ikitokea mbeleko iliyokubeba imelegea, sasa wewe lazima ujibebe mwenyewe, danda na kushikilia kwa nguvu zako zote ili usianguke, na ikitokea wewe umeishiwa nguvu huwezi kushikilia tena, achia mwenyewe udondoke taratibu usiumie, hiyo maana yake ni umefikia kiwango chako cha mwisho cha kubebeka hivyo sasa wewe ni zigo, lisilobebeka tena, ni busara kuachia mwenyewe usipoachia, utabwagwa chini kama zigo na utaumia!, ukiumia karma inamrudia aliyekuumiza!, hivyo kujijutia kwako na maumivu ya kubwagwa, mtatuponzea bure na huyu!, wajibikeni wenyewe msituponzee bure Mama yetu kwa mi karma yenu!.
Safari bado ni ndefu.
Jumapili njema.
Wasalaam,
Paskali.
Update
Hata kilichotokea October 29, kuna watu hawakupaswa kusubiri matokeo ya Tume yoyote, walipaswa to take some political responsibility to step down, wakufa watu 518,na hakuna yeyote aliyewajibika!,CDF,IGP na DGIS bado mnasubiri matokeo ya tume ya Jaji Lila?。
P