Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

chadomoo mwaka huu roho zitawatoka.

go go go magufuli go go go.
 
sidhani kama kuna jambo ambalo mkuu atafanya muache kulipinga,sijaona hata moja ;
-kuanzisha vuguvugu la makinikia mmepinga
-swala la almasi nalo mmelipinga
-vyeti fake nalo mkapinga
-tumbua tumbua ya watumishi wasiona ueledi wa kazi mkaoinga
-ununuzi wa bormbider nao mmepinga
-jamani ujenzi wa ukuta mererani nao mnapinga ndugu zangu?
Lipi alifanye huyu mzee ili muweze kumuelewa ? Sidhani kama upinzani wapaswa kuwa hivi ,sidhani kabisa
 
Naona kila afanyalo bwana mkubwa sio jema. Ama kweli urais ni zaidi ya mzigo!
 
Naona kila afanyalo bwana mkubwa sio jema. Ama kweli urais ni zaidi ya mzigo!
QUOTE]
sijui tu tatizo gani sisi wapinzani aseee yaaan watu wanataka afanye wanayotaka wao
 
QUOTE]
sijui tu tatizo gani sisi wapinzani aseee yaaan watu wanataka afanye wanayotaka wao
Hata akifanya wanayotaka afanye bado wanampinga tu. Rejea kauli ya mh.Msigwa kuhusu serikali kugharamia matibabu ya mh.Lissu
 
Hata akifanya wanayotaka afanye bado wanampinga tu. Rejea kauli ya mh.Msigwa kuhusu serikali kugharamia matibabu ya mh.Lissu
hawa watu wana matatizo ya akili mkuu
 
Ni wazo zuri kujenga ukuta,lakini nina wasi na idadi ya kuta zitakazojengwa kulinda madini, kwani nchi yetu kila jembe unalochimba unakutana na madini. Mwadui kuna ngome. Migodi ya dhahabu haiingiliki, kwa ngome. Kinacho kula madini yetu si ukosefu wa ukuta, ni sera sheria mbovu za madini. Hata tunapogundua kuibiwa tunanyamaza. India imeshamiri viwanda vya tanzanite, wakati haina shimo hata moja la kuchimba tanzanite. Tuna balozi huko miaka. Ni lini alihoji au kupeleka mashtaka mahakamani kwa niaba yetu? Kama nchi mbona hatujaenda UN kulalamika na kudai tulipwe fidia na mataifa hayo wezi? Bila sera na sheria, ukuta utajengwa, na viwanda vya tanzanite nje vitashamiri, kwani wezi ndio tunaopewa kulinda.
Ukuta utajengwa juu lakini madini yanachimbwa chini, hapo inakuwaje??
 
mererani kusema ukweli madini yamepungua mno kujenga ukuta ni upotevu tu wa pesa za watanzania
 
Habari wakuu ...

Huu bado ni muendel ezo wa kile tunachokilalamikia kila wakati kwamba pesa za wavuja jasho zinatumika bila mipango na hakuna wa kuhoji.

Tanzanite watu wameichimba yote yamebakia mashimo matupu yanayojaza maji kama mabwawa ya nini sasa kutumia pesa za watanzania kuzungusha ukuta kuzunguka mashimo ambayo hakuna madini yameshachimbwa yote na waliochimba wameshaondoka?

Naomba Rais asitishe hili zoezi ambalo halina maslahi yoyote kwa Watanzania na wananchi wa eneo husika na badala yake pesa hizo zitumike kuwapelekea wananchi maji, hospitali , umeme na huduma za msingi hapo atakuwa kafanya la maana.

Nawasilisha.
Wewe uko Mererani? Usiongee usilolijua
 
Back
Top Bottom