Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698


Habari waungwana,
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameshatua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Elisha Mngwira. Muda mchache ujao anatarajiwa kuzindua barabara ya KIA mpaka Mererani.

Fuatana nami kujua yanayojiri..
====

Magufuli: Adui yetu mkubwa ni maendeleo sio vyama, ninawashukuru sana kwa kura, nina uhakika hata Malya alinipa, nawashukuru sana wizara ya ujenzi na uchukuzi, TANROADS, wakandarasi na consultants ambao wamefanikiwa kumaliza hii barabara hii ya KM 26 kwa gharama ya bilioni 32.5 na fedha zote zimetokana na kodi za watanzania, nawapongeza sana watanzania wanaolipa kodi.

Barabara ambazo tumeamua kutengeneza zipo yingi, tumeanza na Km 26 lakini haiwezi kuishia hapa kabla haijafika makao makuu ya wilaya na Mkoa.

Nawapongeza sana kwa kumchagua Milya, amelelewa na CCM. Nchi hii ni tajiri na historia inazungumza wazi, tukapewa madini ambayo hayapo pengine kokote duniani, tujiulize haya madini yanatusaidia? Mungu ametupa madini lakini tunapata shida ndio maana nimefika hapa ila mtu analilia shida, Tanzanite tunayo lakini tunaitumiaje? Tulimkosea nini Mungu? Hilo ndio somo langu la leo.

Tanzania matatizo yetu sio vyama, matatizo yetu ni kwanini tunaibiwa? Wangepewa nchi nyingine, hapa pangekuwa kama Ulaya. Ripoi ya Tanzanite iliyoundwa na Spika, Tanzania haiwanufaishi hata wananchi wa hapa, pia haiwanufaishi watanazania. Tanzania inapata asilimia tano, ndio maana nasema nasema tuna changamoto.

Katika uongozi wangu nimeamua kuongoza hii vita, naomba tusimame pamoja kushinda hii vita. Tanzanite ina eneo la kilometa za mraba 81.99, kuna block zimegawanywa. Tanzanite zinaibiwa sana, ni shamba la bibi, nafikiri mabibi waliokufa miaka mingi sana.

Kuna wawekezaji ambao wana asilimia 50 lakini mali zinasombwa. Nimeamua lile eneo ili tuzuie wizi, block A mpaka D, naagiza JWTZ waanze kulijenga ukuta eneo lote, kazi ifanyike haraka. Wakimaliza wake fence na kamera, kutakuwa na mlango mmoja. Hata kama utameza Tanzanite itaonekana.

Serikali ipate pesa yake na mchimbaji apate pesa yake, tunataka soko la Tanzanite liwe hapa Simanjiro na wala sio Arusha. Wanunuzi wote waje kununua hapa Simanjiro, barabara ni lami.

Nimeona tuanze na hii hatua, nina hakika watu wa Tanzanite one na wengine watakaa na kutengeza mkataba wenye faida kwa serikali. Ni lazima tujipange vizuri, hili suala naona sasa linafika mwisho wake.

Biashara haijazuiliwa lakini tunaitoa kwenye biashara ya magendo kuwa biashara halali. Ukishapata mali yako ndani ya uzio, peleka kwenye duka lolote na wateja watakufata hapo hapo. Biashara hii unaondoka umeficha na unapeleka anakulalia kwa sababu anajua huwezi kuipeleka popote.

Benki kuu pia watengeze mkakati wa kushiriki katika kununua zawadi. Tuna madini kila maali lakini majamaa wamekuwa wakisomba tu, tunaendelea kubaki maskini.

Nafahamu katika hatua mlizoanza kuchukua, kuna wengine wamekimbia na hamtawaona kwa sababu ya waliochokuwa wanafanya.

Malya sio adui yetu, adui yetu ni yule anae tuibia. Barabara imejengwa na CCM lakini watapita watanzania wote, tunagombania nini? Wanasema kitunze kidumu, naomba mtunze hii barabara. Kuhusu suala la maji naomba mniachie, kuna mradi mkubwa wa bilioni 45 kwenda makao makuu ya wilaya, eneo hili ambalo halina vyanzo vya maji naomba mniachie.
 
Back
Top Bottom