Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

Jana rais magufuri alipokuwa simanjiro alitoa agizo la kushitukiza kuhusu ujenzi wa ngome ( fence) ya kisasa kuzunguka eneo lote la mgodi je ? hizo pesa zinatoka wapi ?? kwenye bajeti gani ?
zitajengwa kwa bajeti ya ulinzi wa nchi ya JWTZ au hukumsikia raisi alipoongea?
 
Nenda uganda ukapate history ya idd Amini au Ujerumani kwa Hittler au magogoni ukaonane nae
Wanaokutuma uje humu kuwahadaa watanzania yakuwa serikali yetu Ni ya kidikteta wanakupoteza njia acha kabisa Na usirudie tena pumbafu mkubwa kabisa
 
Ni wazo zuri kujenga ukuta,lakini nina wasi na idadi ya kuta zitakazojengwa kulinda madini, kwani nchi yetu kila jembe unalochimba unakutana na madini. Mwadui kuna ngome. Migodi ya dhahabu haiingiliki, kwa ngome. Kinacho kula madini yetu si ukosefu wa ukuta, ni sera sheria mbovu za madini. Hata tunapogundua kuibiwa tunanyamaza. India imeshamiri viwanda vya tanzanite, wakati haina shimo hata moja la kuchimba tanzanite. Tuna balozi huko miaka. Ni lini alihoji au kupeleka mashtaka mahakamani kwa niaba yetu? Kama nchi mbona hatujaenda UN kulalamika na kudai tulipwe fidia na mataifa hayo wezi? Bila sera na sheria, ukuta utajengwa, na viwanda vya tanzanite nje vitashamiri, kwani wezi ndio tunaopewa kulinda.
 


Habari waungwana,
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameshatua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Elisha Mngwira. Muda mchache ujao anatarajiwa kuzindua barabara ya KIA mpaka Mererani.

Fuatana nami kujua yanayojiri..
====

Magufuli: Adui yetu mkubwa ni maendeleo sio vyama, ninawashukuru sana kwa kura, nina uhakika hata Malya alinipa, nawashukuru sana wizara ya ujenzi na uchukuzi, TANROADS, wakandarasi na consultants ambao wamefanikiwa kumaliza hii barabara hii ya KM 26 kwa gharama ya bilioni 32.5 na fedha zote zimetokana na kodi za watanzania, nawapongeza sana watanzania wanaolipa kodi.

Barabara ambazo tumeamua kutengeneza zipo yingi, tumeanza na Km 26 lakini haiwezi kuishia hapa kabla haijafika makao makuu ya wilaya na Mkoa.

Nawapongeza sana kwa kumchagua Milya, amelelewa na CCM. Nchi hii ni tajiri na historia inazungumza wazi, tukapewa madini ambayo hayapo pengine kokote duniani, tujiulize haya madini yanatusaidia? Mungu ametupa madini lakini tunapata shida ndio maana nimefika hapa ila mtu analilia shida, Tanzanite tunayo lakini tunaitumiaje? Tulimkosea nini Mungu? Hilo ndio somo langu la leo.

Tanzania matatizo yetu sio vyama, matatizo yetu ni kwanini tunaibiwa? Wangepewa nchi nyingine, hapa pangekuwa kama Ulaya. Ripoi ya Tanzanite iliyoundwa na Spika, Tanzania haiwanufaishi hata wananchi wa hapa, pia haiwanufaishi watanazania. Tanzania inapata asilimia tano, ndio maana nasema nasema tuna changamoto.

Katika uongozi wangu nimeamua kuongoza hii vita, naomba tusimame pamoja kushinda hii vita. Tanzanite ina eneo la kilometa za mraba 81.99, kuna block zimegawanywa. Tanzanite zinaibiwa sana, ni shamba la bibi, nafikiri mabibi waliokufa miaka mingi sana.

Kuna wawekezaji ambao wana asilimia 50 lakini mali zinasombwa. Nimeamua lile eneo ili tuzuie wizi, block A mpaka D, naagiza JWTZ waanze kulijenga ukuta eneo lote, kazi ifanyike haraka. Wakimaliza wake fence na kamera, kutakuwa na mlango mmoja. Hata kama utameza Tanzanite itaonekana.

Serikali ipate pesa yake na mchimbaji apate pesa yake, tunataka soko la Tanzanite liwe hapa Simanjiro na wala sio Arusha. Wanunuzi wote waje kununua hapa Simanjiro, barabara ni lami.

Nimeona tuanze na hii hatua, nina hakika watu wa Tanzanite one na wengine watakaa na kutengeza mkataba wenye faida kwa serikali. Ni lazima tujipange vizuri, hili suala naona sasa linafika mwisho wake.

Biashara haijazuiliwa lakini tunaitoa kwenye biashara ya magendo kuwa biashara halali. Ukishapata mali yako ndani ya uzio, peleka kwenye duka lolote na wateja watakufata hapo hapo. Biashara hii unaondoka umeficha na unapeleka anakulalia kwa sababu anajua huwezi kuipeleka popote.

Benki kuu pia watengeze mkakati wa kushiriki katika kununua zawadi. Tuna madini kila maali lakini majamaa wamekuwa wakisomba tu, tunaendelea kubaki maskini.

Nafahamu katika hatua mlizoanza kuchukua, kuna wengine wamekimbia na hamtawaona kwa sababu ya waliochokuwa wanafanya.

Malya sio adui yetu, adui yetu ni yule anae tuibia. Barabara imejengwa na CCM lakini watapita watanzania wote, tunagombania nini? Wanasema kitunze kidumu, naomba mtunze hii barabara. Kuhusu suala la maji naomba mniachie, kuna mradi mkubwa wa bilioni 45 kwenda makao makuu ya wilaya, eneo hili ambalo halina vyanzo vya maji naomba mniachie.

Kaz nzuli magu
 
Wenzake wako UN huko kupanga mipango ya maana yeye kazi kutafuta majukwaa ya kupiga vijembe wapinzani. Watanzania tumekula hasara kwa miaka mitano.
Mheshimiwa endelee kukaza mtanyooka tu, UN haikumchagua Magufuli bali Watanzania ndio waliomchagua
 
Habari wakuu ...

Huu bado ni muendelezo wa kile tunachokilalamikia kila wakati kwamba pesa za wavuja jasho zinatumika bila mipango na hakuna wa kuhoji.

Tanzanite watu wameichimba yote yamebakia mashimo matupu yanayojaza maji kama mabwawa ya nini sasa kutumia pesa za watanzania kuzungusha ukuta kuzunguka mashimo ambayo hakuna madini yameshachimbwa yote na waliochimba wameshaondoka?

Naomba Rais asitishe hili zoezi ambalo halina maslahi yoyote kwa Watanzania na wananchi wa eneo husika na badala yake pesa hizo zitumike kuwapelekea wananchi maji, hospitali , umeme na huduma za msingi hapo atakuwa kafanya la maana.

Nawasilisha.
 
Habari wakuu ...

Huu bado ni muendelezo wa kile tunachokilalamikia kila wakati kwamba pesa za wavuja jasho zinatumika bila mipango na hakuna wa kuhoji.


Tanzanite watu wameichimba yote yamebakia mashimo matupu yanayojaza maji kama mabwawa ya nini sasa kutumia pesa za watanzania kuzungusha ukuta kuzunguka mashimo ambayo hakuna madini yameshachimbwa yote na waliochimba wameshaondoka?


Naomba Rais asitishe hili zoezi ambalo halina maslahi yoyote kwa Watanzania na wananchi wa eneo husika na badala yake pesa hizo zitumike kuwapelekea wananchi maji, hospitali , umeme na huduma za msingi hapo atakuwa kafanya la maana.

Nawasilisha.
Acha bange , kwani wewe unalala milango wazi usiki
 
Ndio kipaumbele cha awamu hii 5...vuruga uchumi kutokuwa kipaumbele...ubabe visasi ma mauaji ya raia.......mkono wa chuma!!!
 
Back
Top Bottom