siyoi koroi
Senior Member
- Sep 6, 2016
- 177
- 214
Kama mahakama ziko huru atupe njia ya kufuata ili kura za urais kati la Lowasa na Magufuli zihesabiwe upya.
Jaji mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma amaesema sio sahihi kufananisha mahakama zetu na mahakama za Kenya na kusema mahakama zetu zipo huru zaidi
Mh Jaji vipi sakata la Tanroads. Sesi amesha kwenda kutibiwa Muhimbili ka mahakama yako ilivyo amuru? Tufafanulie huo Uhuru ulio nao.Uku ni kujidhalilisha.
Baada ya kuukosa ujaji mkuu unaanza kujielewa bado dikteta atakushika saburi ndio uanze kubwatuka vizuriInategemea jaji Mkuu alimaanisha uhuru gani. labda alimaanisha uhuru wa kutafsiri sheria au wa uhuru wa kupanga mda wa kusikiliza kesi (kalenda) au uhuru wa kuajiri watumishi wa mahakama. Lakini kiukweli uhuru wa mahakama kwa tanzania ni neno la kusadikika.
Ni bora kabisa mahakama za mwanzo na mahakama za wilaya zina chembe chembe ya uhuru wa mahakama. Lakini ukifikia Mahakama za Mahakimu wakazi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa uhuru wa mahakama haupo. Ndio kuna kesi mahakimu na majaji wanaamua kwa utashi wao, tena bila kuhofia chochote. Lakini kuna kesi mahakimu na majaji wanaamua si kwa utashi wao wala si kwa kufuata misingi ya kisheria, bali wanaamua kwa misingi ya matakwa ya Serikali kuu (executive).
Kuna kesi nyingi sana tu (sitazitaja hapa kwa makusudi maalumu) mahakama ilitoa maamuzi hata kabla ya kusikiliza kesi hizo, kilichofanyika ni kutekeleza utaratibu tu ili kuonesha utaratibu umefuatwa. Nina mifano kibao ya kesi ambayo majaji (zilizokuwa mahakama kuu) na mahakimu (kwa kesi za mahakama za wilaya na mkoa) walifuatwa faragha na kuambiwa waharakishe kusikiliza kesi hizo, au zile walizoambiwa wacheleweshe usikilizwaji wa kesi hizo kwa makusudi, na zingine waliambiwa wafanye wafanyalo lakini uamuzi wa mwisho uwe na muelekeo fulani.
Hivi kuna anaejua kuwa hakuna kesi ambayo serikali (executive) ina interest nayo ambayo hupangiwa kusikilizwa na jaji au hakimu wa hovyo au wasiuyempenda? Ni utaratibu uliopo majaji hupangiwa kesi kulingana na yeye alivyo na mtizamo wake kwenye serikali, na mahakimu wanapangiwa kesi kulingana na kesi yenyewe.