Mahakama Urusi yapiga marufuku Mashahidi wa Yehova

Mahakama Urusi yapiga marufuku Mashahidi wa Yehova

Wazee wa Amkeni.

Hawa jamaa misimamo yao huwa siwaelewi, Kuna dada mmoja alikuwa Mtangazaji wa Redio Country alifariki kwa sababu ya misimamo ya Kanisani kwako, Ni marufuku kwenda hosptali wala kuongezewa damu. Ni mwendo wa kuombewa tu hivyo ukipona usipopona ni Kazi ya Yehova.

Na pia ni marufuku kujihusisha na Masuala ya Siasa wala Upigaji wa kura, na ndio Lililokuwa Dhehebu la Mke wa Kwanza wa hayati Mandela na ndio kisa cha Ndoa yake kuvunjika.

Haya jamaa Hapana aisee! hata tuseme ni Uhuru wa kuabudu.
 
Mkuu kuna jambo moja umelisahau hawa watu huwa hswasherekei Christmas's, wala Pasaka
Krismas imeandikwa wapi kwenye bibilia? Hiyo ni moja wapo ya tofauti na madhehebu mengine.
Nikisema nipe andiko kuhusu krismas ntakua nimekutoa nduuki utaishia kusema ilibuniwa tu.
 
Sio Urusi tu. Mbona hapa Tanzania walikuwa hawaruhusiwi wakati wa Rais Mwl J.K Nyerere. Ni Rais wa awamu ya pili ndio alitoa ruhusa waanze kufanya shughuli zao hapa nchini. Nakumbuka ilikuwa ni kosa ukikamatwa na gazeti la watch tower. Kule maeneo ya mpakani na Zambia watu wengi walikamatwa kwa kukutwa na gazeti hili lililokuwa linaletwa toka Zambia.
Acha uongo Nyerere ndiye aliye toa luhusu baada kujiridhisha na huduma yetu alituma watu walituchunguza na kupeleka ripoti
 
Acha uongo Nyerere ndiye aliye toa luhusu baada kujiridhisha na huduma yetu alituma watu walituchunguza na kupeleka ripoti
Sio uwongo. Issue ni kwamba Nyerere aliwafungia na nakumbuka ilikuwa ni kosa kusoma gazeti la watch tower. Tatizo ni kwamba wakati wa siasa ya ujamaa na kujitegemea hapa nchini, Jehovah Witness (JW) hawakutaka kushiriki kwenye shughuli za kiserikali wakidai kuwa serikali yao iko mbinguni na si duniani. Pili hawakutaka kushiriki kwenye mafunzo ya kijeshi kama JKT na mgambo wakidai kuwa inakatazwa na biblia. Pamoja na mambo mengine kama ya kukataa baadhi ya matibabu kama kuongeza damu kwa mgonjwa. Mengi nenda hapa ukasome https://www.thegospelcoalition.org/article/9-things-you-should-know-about-jehovahs-witnesses.Mbona zipo na nchi nyingine Africa walizofungiwa kama Malawi na Eritrea. Hata baadhi ya nchi zilizoendelea kama marekani, spain na ujerumani waliwahi kuwafungia huko nyuma hasa wakati wa vita ya 2 ya dunia. Kwa habari Zaidi nenda ukasome hapa
Persecution of Jehovah's Witnesses - Wikipedia
 
Mambo mengine wapo sawa kabisa. Hayo maua kwenye msiba yana faida gani? Birh day zimeletwa na wazungu na wala hazina maana yoyote ile.
Wako sahihi kutosheherekea Christmas naomba niambiwe ni Nani aliyethibitisha hyo tarehe 25 Dec kama ndio yesu alizaliwa???? Mm sio shahid wa yehova lkn sisheherekei Christmas
 
hawa wapo kundi moja na wasabato, huwa siwaelewi. wanameza sana vifungu lakini haviwasaidii. wanasoma sana Bible lakini hawamjui Mungu, hawana Mungu na hawatakuja kumwona kwasababu ni shetani ndiye alianzisha madhehebu yao kupitia waanzilishi wao. kuwafutia sio sahihi kwasababu ya uhuru wa kuabudu, lakini ni watu ambao kwangu hata wakifutiwa siwezi kusikitika kwa hapa tz.
Biblia inasema usihukumu....sasa we unafanya nn hapo??? Haupaswi kuhukumu kuhusu kuuona ufalme wa mungu
 
_95468833_witnesses4-jpg.498991


Chanzo: BBC Swahili
Kwa picha hii naanza kuelewa kwa nini kundi limepigwa marufuku!
 
Watanzania wavivu sana wa kujifunza halafu wanajifanya wajuaji, kama hujafanya research huna haki ya kuzungumza, hawa jamaa wapo free kuliko jamii zote zitowazo elimu zao, kwa ratiba zako binafsi mahali upapendako hata baa wanakuja. Waulize lolote ambalo unahisi uko na mashaka nalo, lolote hata kubwa lenye kukuogofya kiimani kulijua, watakusaidia kulijua.

Mi nilishawahi kuitumia muda wangu nao, kama unavuta fegi, unawaomba katkt ya somo ukavute, kwa upendo kabisa wwanakuruhusu,na baadaye sana watakuandalia somo kwa unyenyekevu athari ya kuvuta sigara....

KAMA KWELI UKITAKA KUJUA ANGALAU KIDOGO KUHUSU MASHAHIDI WA YEHOVA SOMA HAPA CHINI

Mkuu nimesoma maoni yako hapo nikaona wewe ni mtu wa busara sana. Na mimi ningependa niwatendee haki, kama vile tu yule mhalifu aliyesurubiwa pembeni ya Yesu alivyomtetea Yesu dhidi ya shutuma za uongo kwa Yesu toka kwa mhalifu mwenzake. Huenda Nikakumbukwa kwa hili, kama ambavyo Yesu alivyoahidi kumkumbuka yule mhalifu aliyemtetea.

Kuna wengi humu JF na kwingineko mnaweza kuja kuhukumiwa kwa kutoa tuhuma za uongo juu ya Mashahidi wa Yehova wakati hamuwajui wala kuelewa imani yao.

Ukweli ni kwamba ulimwengu mara nyingi sana umewahukumu Mashahidi wa Yehova pasipo haki, na mtu yeyote mwenye akili anapaswa kujiuliza sana juu ya hiki kikundi kidogo lakini chenye maadili sana.

Watu watu wanasahau kwamba ushabiki wa kijumuia ndio ulisababisha watu wachague kumsurubu Yesu badala ya mhalifu Barnabas. Leo hii watu wanafanya kosa lilelile juu ya Mashahidi wa Yehova, wakipaza sauti kwa nguvu sana "Wasurubiwe, wasurubiwe!!" huku wakiona makundi mengi ya kidini yenye kukumbatia uuaji, ufisadi wa kila namna, uasherati na hata ushoga ndani ya imani zao kuona yako sawa na ni bora kuliko Mashahidi wa Yehova. Ni dini ngapi hazijali na kuvumilia maovu yanayofanywa na waumini wake japo yanajulikana wazi, na kuwakumbatia kwa sababu ya umaarufu wao, utajiri wao, vyeo vyao, ukuu wa kisiasa, au tu kwa kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaokuja kanisani au kutoa michango ya pesa hata kama ni pesa za uovu?

Mtu yeyote mwenye akili, jambo la kwanza atakalofanya akikutana na Mashahidi wa Yehova, jambo ambalo mie nilifanya, ni kuomba ufafanuzi na kuelimishwa juu ya yote wanayotuhumiwa. Ukifanya hivyo utakuta kwamba wanaonewa sana, na hata unaingia woga kwamba je inawezekana hiki kikundi ndicho kikundi pekee cha Wakristo duniani kinachokubalika na Mungu kama waumini wake wa kweli?

Suala la vita na kuwa jeshini. Kwa mfano - ni wangapi wanajua Mashahidi wa Yehova waliuwawa na Hitler kwa kukataa kushiriki vita ya pili ya dunia - wakimwambia wazi Hitler hakuna sababu yeyote duniani itakayofanya iwe halali kwao kuwaua wanadamu wengine? Jiulize - je ilikuwa halali kwa Mkatoliki wa Jerumani kumuunga mkono Hitler na kumuua Mkatoliki wa Uingereza kwa sababu ya vita, au kwa sababu Hitler kaagiza? Amri ya Hitler ilihalalisha kukiuka amri ya Mungu ya kutoua? Na baada ya vita je, Mkatoliki wa Ujerumani alipaswa kurudisha undugu wake wa kikristo na Mkatoliki wa Uingereza na kudai wapendane kama Wakristo wa dhehebu moja? Hicho ndicho Mashahidi wa Yehova walimkatalia Hitler, na ikawa ni dini pekee ya Kikristo Ujerumani iliyokuwa na ujasiri wa kumpinga Hitler, sio kwa sababu za kisiasa, bali kwa sababu za kikristo.

Hitler akawatia gerezani (concentration camps) na kuwaua. Leo hii kila mtu anamlaani Hitler. Je Mashahidi wa Yehova walikosea? Je tumesahau dini nyingine zilivyokuwa mstari wa mbele kum-support Hitker kule Ujerumani na kumwambia awamalize Mashahidi wa Yehova kwa usaliti kwa Ujerumani? Leo hii suala ni lile lile. Kwa hiyo wao wakikataa kujiunga na jeshi ili kuepuka kumpiga risasi na kumuua Mkristo mwenzao au binadamu mwenzao tofauti na amri ya Mungu ya usiue, tuwalaumu? Watu wanasema mbona Waisrael walipigana vita kwa support ya Mungu - na kusahau wakati huo Israel lilikuwa taifa pekee teule la Mungu wakipigana na watu wa "mataifa" wenye miungu ya uongo, tofauti na sasa ambapo kila binadamu duniani ni sehemu ya taifa la Mungu hakuna tena taifa teule, na kivyo huruhusiwi kuua mtu yeyote ndani ya taifa la Mungu kwa sababu yeyote ile, au amri ya mwanadamu mwenzako. Huwezi kumwambia Mungu niliua kwa sababu ya kuamriwa niue na kiongozi wangu kwa hiyo sina kosa mbele zako wewe Mungu! Kama wewe ni Mkristo wa kweli jiepushe au jiondoe katika mazingira ya kuamriwa kuua mwanadamu mwenzako - ndicho Mashahidi wa Yehova wanafanya.

Mashahidi wa Yehova na mauaji ya Rwanda. Tuje hapa jirani Rwanda. Leo hii Kagame pamoja na yote yanayosemwa juu yake, humwambii kitu dhidi ya Mashihidi wa Yehova. Anawatetea mno. Kwa nini? Kwa sababu wakati wa mauaji ya Rwanda, genocide, wakati Wakatoliki Wahutu wakiua Wakatoliki wenzao Watutsi hadi ndani ya makanisa yao, Mashahidi wa Yehova Wahutu waliwahifadhi na kuwaficha Mashahidi wa Yehova Watutsi na hata Watutsi wasio Mashahidi wa Yehova ili wasiuwawe. Walifanya hivyo na hata baadhi yao kuuwawa na Wahutu wenzao walipogundulika kuwaficha Watutsi waliokuwa wakiuwawa na Wahutu wenzao! Sasa nani alikuwa jirani wa kweli kati ya Mkatoliki Mhutu na Shahidi wa Yehova Mhutu wakati wa genocide Rwanda? Nenda kwa Kagame atakueleza.

Suala la siasa. Tuje hapa Tanzania. Mashahidi wa Yehova wamesema wazi hawako tayari kuwa upande wowote wa siasa, au hata kujihusisha na siasa, kwa sababu huu utaratibu wa kibinadamu unaleta migongano ya kijamii. Je ni uongo? Wao wanapenda kuishi kwa amani na kila mtu, bila kujali chama chake, kabila lake nk. Mara ngapi hata viongozi wa siasa wametamka wazi na hata kuwatendea watu wa chama kingine kama maadui, bila kujali kwamba wanasali kanisa au dini moja? Ni wangapi walioko CCM wanamuona mtu wa Chadema kuwa adui japo wanasali kanisa moja au wako dini moja? Je Mahahidi wa Yehova wakisema hawajihusishi na siasa kuepuka hili wanakosea? Ni nani mwanasiasa mkereketwa ambaye bado utamwona ni Mkristo wa kweli mwenye kupenda watu wote na hata wa vyama vya upinzani bila kuwasema vibaya au kuwazushia uongo? Leo hii tunadai Mashahidi wa Yehova wanafanya kosa kuimarisha upendo wao wa Kikristo kwa kuhakikisha hawagawanywi kulingana na itikadi za siasa? Je unaona mtu wa dini yako anaekubagua, kukutukana na hata kukudhuru kwa sababu za kisiasa ni Mkristo bora kuliko Shahidi wa Yehova aliyesema hatajihusisha na siasa ili aishi kwa amani na kila mtu, kama Wakristo wanavyotakiwa kuishi pamoja?

Tuje suala la Krisimasi na Easter. Hata wachungaji wa dini nyingine wasio Mashahidi wa Yehova wanajua Christmass ina chanzo cha kipagani na iliingizwa kwenye desturi za Kikristo karne ya nne na Waroma. Kwa hiyo leo nani ni Mkristo wa shaka - Shahidi wa Yehova anaekataa sikukuu za kipagani silizopakwa sukari ya ukristo au yule anaefurahia kumdanganya Mungu kwa kuhalalisha sherehe ya kipagani kuwa ya Kikristo kwa sababu inampa kiki au nafasi ya kufanya sherehe? Kuna shahidi wa Yehova aliniuliza swali - hebu niambie, katika siku ya kawaida na ile ya Krisimass, unadhani ni ipi ambayo Mungu akiwa huko mbinguni anasikitishwa sana na matendo ya binadamu hapa duniani? Ni wazi ni siku ya Krismasi.

Hivyo swali likawa, sasa ikiwa wewe unataka kuwa Mkristo wa kweli, unadhani ni busara kuwa sehemu ya siku ambayo ilianzishwa tu na wanadamu bila maagizo yake Mungu, na siku ambayo kila mwaka inamsikitisha sana Mungu kwa sababu inafanywa kwa kivuli cha kuzaliwa Yesu, ikigubikwa na matendo mengi ya uovu na hata wanadamu kupoteza maisha yao, na wewe ukaona ndio siku ya kufurahi na kusema ni maalum kwa Mungu, ukijua wazi ni siku inayomhuzunisha sana? Akauliza, hebu jiulize, unafikiri Mungu anaweza kukuhukumu kwa kutosherehekea Krismasi, kitu ambacho hakuagiza kifanyike na siku ambayo inamhuzunisha sana? Na jiulize pia, unafikiri Mungu anaweza kukuhukumu kwa kusherehekea Krisimas, kitu ambacho hakuagiza na siku inayomhuzunisha sana?

Hata suala la sikukuu ya Easter watakuonyesha lina chanzo cha kipagani ndio maana hawajihusishi. Watakuuliza, hivi unafikiri suala la sungura na mayai kuhusiana na Easter lina uhusiano na kifo cha Yesu? Watu tunapokea kadi za Easter zenye mayai na sungura na hata kula chocolate za sungura na mayai wakati wa Easter bila hata kujiuliza - Mashahidi wa Yehova wakikataa vitu hivi tunaona wao ndio wasiojua Ukristo! Mungu tuhurumie katika ujinga wetu.

Tuje suala la damu. Mashahidi wa Yehova wanakataa blood transfusion. Hiyo ni kweli. Waulize kwa nini, watakuonyesha maandiko yaliyo wazi yanayosema Mungu haruhusu watu kula damu, au anasema wajiepushe na damu. Ukisema blood transfusion sio kula, swali wanalouliza ni je, kula maana yake ni nini? Je kula lazima kuhusishe kupitisha kitu mdomoni? Kula dawa za kulevya lazima uzitie mdomoni? Au mtu aliepata majeraha mabaya na hawezi kutumia mdomo kula, analishwaje ili aendelee kuishi? Hapo ndipo wanakuuliza, Mungu alipotoa amri ya kukataza kula damu, alisema usile damu kwa mdomo tu, na ni sawa kula (kuingiza kitu mwilini) kwa njia nyingine? Je ukiambiwa usile dawa za kulevya, utajitetea mie sikula kwa sababu zikuzitia mdomoni? Na je, wewe unataka kuwa mshauri wa Mungu kwa kumwambia hukuniambia nisile kwa kutumia mishipa? Na swali ljingine - ni halali kukiuka amri ya Mungu kwa sababu uhai wako uko hatarini? Je Yesu hakusema anaetaka kuiponya roho yake ndie ataingamiza? Alimaanisha nini kama sio kusema hata ikibidi ufe kwa ajili ya kutii amri ya Mungu ni sawa?

Maswali zaidi wanayouliza kuhusu damu ni kama haya; Je mtu akikuambia ili upone ugonjwa fulani utakaokuua ni lazima ufanye tendo ambalo unajua linakiuka amri ya Mungu, kwa mfano, ule kibudu cha jogoo mweusi, utalifanya ili usife kwa ugonjwa unaokusumbua? Kuna wakati inakuwa halali kuvunja amri ya Mungu ili ujiokoe uhai wako?

Suala la bendera; Mashahidi wa Yehova wanaichukulia bendera kama ni ishara ya kitaifa ambayo wanaelewa inapaswa kuheshimiwa, lakini heshima isifike kiwango cha kutukuzwa au kuabudiwa. Kumbuka kwamba Mashahidi wa Yehova hawajiweki katika misisimuko ya kuhusudu au kutukuza ma-celebrity kama wanamziki kwa sababu kama hizo - kwamba watu wengine hufikia kama kuwatukuza ma-celebrity. Ndio maana wako makini sana na mambo ya bendera. Wanasema mara nyingi bendera inafikia kutukuzwa kufikia kiwango cha kuhatarisha kuwa namna ya ibada ya sanamu. Wanasema wanaheshimu bendera kama ishara ya taifa, na hata inaposhushwa au kupandishwa watasimama kwa heshima, lakini wana heshima isiyopita mipaka kuhusu bendera. Wataiheshimu kama alama ya kitaifa, ila hawataitukuza.

Wimbo wa taifa. Tatizo lao hapo ni moja. Wanauliza, je wimbo wa taifa ni sala? Nadhani utajibu ndio. Wimbo wa taifa ni ujumbe kwenda kwa Mungu; Mfano, Mungu ibariki Tanzania, na watu wake...nk. Sasa hapo ndipo linapokuja tatizo. Wao wanasema wazi kwamba Biblia imetoa utaratibu ulio wazi kabisa wa jinsi ya kuongea na Mungu kwa njia ya sala. Sasa kama tunataka kutoa sala kwa Mungu basi tufuate utaratibu unaokubalika na Mungu. Kwa mfano, ikiwa wimbo wa taifa ni sala kwa Mungu, na wao kama Wakrsto wanatambua sala lazima ipitie kwa Kristo Yesu, kwa nini basi wimbo wa Taifa haumalizii kwa kusema tunaimba kwa jina la Yesu? Kwa hiyo msimamo wao ni kwamba kama tunakiri wimbo wa taifa ni ujumbe kwenda kwa Mungu, au sala, basi kuuimba inakuwa ni namna ya ibada. Basi kama tunafanya tendo lolote la ibada, basi lifanyike kwa uratibu wa kiibada ambao Mungu ataukubali, sio utaratibu uliopangwa na wanadamu na kumlazimisha Mungu aukubali - upo hapo!!! La sivyo wao wasingependa kujihusisha na ibada ambayo Mungu hataikubali kwa kuwa tu wanadamu wameukubali kama sehemu ya shughuli za taifa. Watakukumbusha msimamo wa kima Meshack, Shedrak na Abednego katika suala kama hilo.

Pia kuna suala la kuwasingizia kuwa hawaendi hospitali. Huu ni uongo mkubwa. Mashahidi wa Yehova ukiumwa hawaombei - wanakuambia uende hospitali, upate dawa, na pia umwombe Mungu abariki dawa utakazopewa ili zikuponye. Wapo Mashahidi wa Yehova ambao ni madaktari.

Na kuhusu shule - ni uongo mwingine juu yao. Kama hawaendi shule hayo magazeti tunayosoma na kuyapenda nani anawachapishia? Nani anawafanyia hizo research? Wapo Mashahidi wa Yehova ambao ni maprofessor wa chuo kikuu, wanasheria, mainjinia nk.

Biblia waliyoichapisha. Je, mnajua kwamba ulimwengu wa wasomi wasio Mashahidi wa Yehova ulikuja kukiri kwamba tafsiri ya Biblia iliyo sahihi kuliko zote ni ile iliyotolewa ya Mashahidi wa Yehova inayoitwa "The New World Translation of Holy Scriptures"? Kuna mtu alifanya research ya PhD juu ya jambo hili. Jaribu ku-google "the most accurate bible translation" utaona hili!

Kwa hiyo wana JF, jiepusheni sana na kuwatuhumu Mashahidi wa Yehova kwa uwongo, au kurudia tuhuma ulizosikia wa wengine kama kasuku. Wapo barabarani kila siku. Chukua muda jaribu kuongea nao. Ni watu wanaojiheshimu sana, na wanachotaka ni amani na kuishi vema na kila mtu kwa upendo, kitu ambacho katika dini nyingi sana siku hizi kakithaminiwi tena. Usije ukakuta Mashahidi wa Yehova ndio dini pekee inayokubalika na Mungu kumbe na wewe ulihusika katika "kuwakataa watumishi wa kweli wa Mungu", kama alivyotabiri Yesu (kadiri mlivyowakataa hawa ndivyo mlivyonikataa mimi).

Hadi leo kuna kampuni kadhaa ukisema wewe ni Shahidi wa Yehova unapata kazi mara moja! Nasikia kuna wakati fulani huko Zambia raisi wao alisema watu wa kufanya kazi fulani wawe Mashahidi wa Yehova tu. Hivyo, je ni kweli Mashahidi wa Yehova ni wabaya kama wanavyosemwa au ni kampeni za shetani dhidi yao, ambazo tunajikuta tunaziunga mkono kama ilivyokuwa kwa Yesu dhidi ya Barnabas, na kuitikia "Mashahidi wa Yehova wasurubiwe, wasurubiwe!"

Tuwe waangalifu sana tusije tukajifanya maadui wa Mungu bila kujitambua. Mashahidi wa Yehova ni watu ambao watu wengi wamekiri kwamba wana roho ya Mungu wa kweli. Ukienda website yao www.jw.org utajifunza mengi sana.
 
Nafikiri umeamua kuwatuhumu pasipo ushahidi. Hakuna kwenye Biblia panapotajwa utatu labda uniambie ni biblia gani yenye utatu ni andiko gani. Pia historia ya huyo mwanamke aliyeenda mbele za Yesu kwa tuhuma za uzinzi haijaondolewa iko kama ilivyo. Kilichofanyika ni kutafsiri katika lugha inayoeleweka kuliko ya awali kwani nia kuu ni kuufikisha Ujumbe.

Hata unaposema wanaruhusu ushoga unakosea sana mkuu. Sijui hizo tuhuma unazitoa wapi? Hilo jambo haliruhusiwi ndani ya Mashahidi wa Yehova maana hata Biblia inakataza na ukigundulika unatengwa na ushirika. Tuhuma nyingi dhidi ya Mashahidi wa Yehova ni za mtaani zaidi kuliko uhalisia.
1Yoh5:8 tafuta King James version.New age church yote ni cult,,,na mnatofautiana maajabu tu,,Nyie Jw mmeedit bible,,Mormon na Presbyterian church wameruhusu Ushoga kanisani pasipo na branch ya Africa kujitenga na West jambo lililoonyesha hawafai kuwa Africa kabisa,,Anglican nawapongeza wamekataa ujinga wa Ulaya.Mimi nimesoma bible zote za kutunga kwa hio sibahatishi ninachokuambia.
 
Bodi ya watu inakaa inasema biblia fulani ndo sahihi kwa vigezo gani?? Biblia ya kwanza imewekwa pamoja miaka ya 1500 then bodi ije ikae miaka ya 1900s iseme biblia ilioeditiwa 1940 kutoka vyanzo vile vile ndio sahihi??? It is Utter Nonsense.
 
Putin anajua trick zao zote na anajua kuwatibulia. Alifanya hivyo Crimea

 
Hiyo picha inahusiana nini na kupigwa marufuku? Umesoma hayo maneno yanayoambatana na hiyo picha na kuyaelewa?
Haufuatilii kinachoendelea mashariki ya Kati ndiyo maana unashindwa kuunganisha vidoti doti.
 
Injili haiwezi kuzuiwa kwa njia kama hiyo,wao waendelee kuomba Mungu wanayemuomba ataipa pigo nchi hiyo na uongozi wao.Rais anapokuwa mbishi nchi ndiyo hupigwa.Rejeeni farao na waisrael.
 
1Yoh5:8 tafuta King James version.New age church yote ni cult,,,na mnatofautiana maajabu tu,,Nyie Jw mmeedit bible,,Mormon na Presbyterian church wameruhusu Ushoga kanisani pasipo na branch ya Africa kujitenga na West jambo lililoonyesha hawafai kuwa Africa kabisa,,Anglican nawapongeza wamekataa ujinga wa Ulaya.Mimi nimesoma bible zote za kutunga kwa hio sibahatishi ninachokuambia.
Hao Mormon na Presbyterian mbona umewakazania sana. Hoja yako ni kuhusu Mashahidi kuruhusu ushoga. Je una ushahidi wowote unaodhirisha Mashahidi wa Yehova wanaruhusu ushoga? Au umeamua kuwachafua tu.

Kuhusu tafsiri za Biblia iko hivi; Mashahidi wa Yehova wamefanyia tafiti tafsiri zote kutia ndani original scriptures za Kiebrania na Kigiriki ambazo ndio zilitumika na watu wengine kwenda kwenye lugha nyingine kama kiingereza. Baada ya utafiti wa mda mrefu iligundulika kuwa kuna mambo yaliongezwa au kupunguzwa kwa makusudi au bila kukusudia hivyo ilihitajika kurudisha uhalisia wa kimaandiko. Na pia sehemu ambayo ilikuwa na lugha ngumu kuelewa kuwekwa lugha rahisi. Kwa mfano baadhi ya biblia unaposoma Mhubiri 9:5&6 na 10-11 unakutana na maneno sheoli au abiso kwa sehemu zingine. Sijui kama unafahamu maana ya maneno hayo kwa kiswahili kama ilivyo kwa kiebrania na Kigiriki. Maana maneno hayo Mawili yametoholewa toka lugha hizo mbili na kuwekwa kwenye biblia kama yalivyo ijapokuwa Kuna neno husika la kiswahili.

Hata hivyo Biblia ilipitia hatua mbalimbali za kiswahili hadi unaipata hiyo unayoiamini ingawa bado kulikuwa na mapungufu. Ukiisoma tafsiri ya kwanza ya kiswahili hutaelewa kabisa, maana ina kiswahili kibovu kupita maelezo.
 
Back
Top Bottom