Recent content by Wateule

  1. Wateule

    Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

    Yeah, It all makes sense now. Serikali yake ilijawa na usiri mwingi, na sasa ni mengi tu mengine tutaanza kujasikia. Ingawa hili la maradhi ya moyo pia lilikuwa linasikika kama tetesi tu, na tetesi huwa zinakuaminika kichwa kichwa.
  2. Wateule

    Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?

    Hiyo itategemea umakamu wa rais ataupata nani. Kwakuwa huku bara idadi ya Waislamu na Wakristo ni nusu kwa nusu, inawezekana kabisa kukawa na shinikizo kwamba makamu wa rais awe Mkristo ili kubalance na rais ajaye ambaye ni "Muislamu." Tukumbuke kwamba marais watatu waliopita kuanzia Mkapa...
  3. Wateule

    Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?

    Ingawa katiba haikutaja dini, ila imetaka rais akitoka bara, basi makamu ni visiwani, na kinyume chake ni kweli. Kwa utamaduni wa CCM, hiyo ina maana pia kibarua cha waziri mkuu Majaliwa kimeshaota nyasi, kwakuwa rais atakuwa "mwislamu" basi waziri mkuu atakuwa "mkristo."
  4. Wateule

    Finally: Kateerero recognised in Oxford dictionary

    roselina john, roselina john , nimekuwa natafuta kamusi nzuri ya Kiswahili - Kingereza na kinyume chake. Kama hiyo hapo juu inaonekana ni nzuri, je una dondoo zozote namna ya kuipata?
  5. Wateule

    Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!

    Labda niongeze ufafanuzi kidogo ndugu yangu, hawa wanaodai mtu anatakuwa "hatari kwa usalama wa Tanzania" kwa kujua kwamba mtu akipata uraia na haki zake (kwa kawaida) zina ongezeka ndani ya Tanzania. Kwa mfano, haki ya kuchagua na kuchaguliwa, na ile ya kuteua na kuteuliwa pia. Hivyo basi...
  6. Wateule

    Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!

    Tatizo la CCM kwenye hii issue ya uraia pacha ni kuogopa tu ushindani utakaoletwa na Watanzania wa diaspora, ambao wengi wameelimika au kutokana na kuishi kwao kwenye nchi za kigeni zilizoendelea, wamekuwa na uelewa wa mambo ambao utaleta shida kwa viongozi wa CCM waliozoea kuabudiwa na wajinga...
  7. Wateule

    Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!

    Asante kwa kujitahidi kufafanua hili suala kwa ndugu zetu, ambao wengi bado hawaelewi au wengine wanapotosha kwa makusudi. Binafsi, napingana na hii dhana ya kusema kwamba mtu "ameukana uraia wa Tanzania", kitu ambacho si kweli. Watanzania wengi niwajuao mimi, nikiwemo na mimi mwenyewe...
  8. Wateule

    Kwa ulemavu huu aliosababishiwa Tundu Lissu, ninaichukia sana Serikali ya awamu ya tano!

    Because there is a (the) higher Boss than him, and that is why we still have Lissu today. May God continue to bless and protect Lissu, Amen!!
  9. Wateule

    Je, ni kweli kwamba yule kada wa CCM anayehusishwa Kuhamia ACT ni huyu?

    Babo nasubiri majibu kutoka kwa Mh., sijui nitafanikiwa....
  10. Wateule

    Je, ni kweli kwamba yule kada wa CCM anayehusishwa Kuhamia ACT ni huyu?

    Asante Mh. kwa majibu yako, ila hizo sifa zinazofanya mtu asiwe muoga kwenye siasa bado hazijanishawishi. Labda nikupe tafsiri yangu ya "mwanasiasa muoga" ndio labda tutaelewana vizuri. Mwanasiasa muoga ni yule anayekaa kimnya dhidi ya maovu ya kisiasa, kiuchumi, au kijamii kwenye nchi yake kwa...
  11. Wateule

    Je, ni kweli kwamba yule kada wa CCM anayehusishwa Kuhamia ACT ni huyu?

    Huyu mtu ni muoga sanaa, na amezoea vya bure na vya kutafuniwa. Hivyo basi, mikiki mikiki ya upinzani hawezi kabisa, na akienda upinzani basi atarudi chama dola kabla hata uchaguzi wenyewe wa 2020 kwisha, maana haitokuwa uchaguzi, bali ni ujambazi.
  12. Wateule

    Rais John Pombe Magufuli aelekea Afrika Kusini kushiriki sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Nchi hiyo

    Ni bora audhurie na kuondoka tu kwenda Namibia. Akipewa nafasi ya kuongea basi jiandaeni kabisa kisaikolojia. Huko Namibia pia aandaliwe speech maalum (kwa Kiswahili na mkalimani au Kingereza), na kusisitizwa sana kuisoma, vinginevyo akileta ule utaratibu wake wa kuseleleka "free style" pia...
  13. Wateule

    Makonda: Mchaga kusaidia walemavu na yatima ni jambo gumu sana

    KUHUSU DHIHAKA ZINAZOENDELEA BAADA YA JENEZA LA MENGI KUWASILI Hiyo ni njia ambayo tutapitia wote, endapo tutafia nje ya nchi, na kua na ulazima wa kuzikwa nyumbani Tanzania. Kitu ambacho naona ni cha ajabu kidogo katika suala hili ni kumtumia marehem mzee wetu Mengi kama mfano dhidi ya wale...
  14. Wateule

    Mdude Nyagali na lugha yake ya kiukosoaji katika mitandao ya kijamii

    Tunao ushahidi wa kimazingira kama yalivyo matukio mengine ya kutekana na kupigana risasi. Kama unasubiri "uhakika" basi utasubiri sana, kwasababu matukio kama haya huwa polisi hawatoi ushirikiano wowote kwani wanajua kinachoendelea na "mchunguzi, hajichunguzi."
Back
Top Bottom