Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kwa mara nyingine tena nimeshuhudia jinsi Wabunge wa CCM wanavyobishia mambo huku wakiwa mbumbumbu katika suala linalojadiliwa. Yaani inafedhehesha sana kuona jinsi mbunge anasimama kubishia kitu ambacho hana hata uelewa nacho!
Mbunge wa Mbeya, Sugu, alipendekeza kwamba serikali itafakari tena juu ya kuruhusu suala la uraia pacha.
Wakasimama wabunge wa CCM, na bila aibu wanabisha kwamba serikali isiruhusu uraia pacha kwa kuwa hao wanaotaka uraia pacha waliukana uraia wa Tanzania!
Halafu wengine wanasema diaspora ni raia kama Sugu alivyo raia kule Mbeya!
Hivi mbunge anaweza kuwa poyoyo kiasi hicho katika kuelewa maana ya uraia pacha? Unawezaje kusema diaspora hawahitaji uraia pacha kwa kuwa tayari ni raia kama una akili sawasawa? Nikakumbuka hata humu Jamii Forum kulitokea ubishi sana juu ya kuruhusu uraia pacha, na nilishuhudia watu wakibisha bila hata kuelwa utaratibu wa kuwa raia pacha.
Kwa faida ya hawa wabunge vihiyo na wengineo, ningependa kuainisha mambo ya msingi matano katika suala la uraia pacha. Ni wazi kwamba hawa waheshimiwa wabunge na watu wengi humu JF hawayaelewi na wamekuwa wakibisha kuhusu uraia pacha bila kujua uraia pacha unatolewa katika misingi gani.
Pili uraia pacha hautolewi kwa mtu asiye Mtanzania ambaye hajawahi kuishi Tanzania, na akiwa nje ya Tanzania. Raia wa nje kuwa raia pacha na Tanzania lazima awe ameishi kihalali Tanzania kwa muda usiopungua miaka mitano, kama nchi nyingi zinavyofanya.
Tatu, uraia pacha kwa Mtanzania hautolewi na serikali ya Tanzania bali na serikali ambako raia wa Tanzania anaishi kwa muda mrefu akiwa bado ni mTanzania na hajaukana Utanzania. Kinachotokea kwa huyo siyo Tanzania kumpa uraia pacha bali ni Tanzania kuruhusu yeye kuomba uraia wa nchi anakoishi sasa bila kuwa ameukana uraia wa Tanzania.
Hivyo natoa wito kwa Wabunge na wengineo kuacha kubisha juu ya uraia pacha kwa mihemuko bila kujua undani wa uraia pacha, au kwa kisingizio cha uzalendo wakati kilichowakaa akilini wengi wenu ni wivu tu usio na maana. Hili ndilo watu wanaita joka la mndimu - unakuwa joka kwenye mdimu unawazuia watu kuchuma ndimu wakati wewe huli ndimu na hutegemei kula ndimu katika maisha yako, na mbaya zaidi unawaambia watu kula ndimu ni kitu kibaya na hujawahi kuonja ndimu na wala hutegemei kula ndimu. Swali limeulizwa, ni nchi ngapi zilizoruhusu uraia pacha zimeathirka na kuruhusu uraia pacha na hata zikaamua kusimamisha uraia pacha?
Ni kiongozi asiyetumia akili peke yake ndiye atafikiri kwamba Mtanzania mwenye uraia pacha ni hatari zaidi kwa usalama wa Tanzania kuliko mtu aliyekua raia wa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, India, Pakistan, Oman, Somalia, DRC, Russia, Marekani nk ambaye amepewa uraia wa Tanzania kwa kuwa amesema ameukana uraia wa nchi yake.
Acheni kupotosha watu kwa hizi cheap propaganda dhidi ya uraia pacha.

- Uraia pacha si kwa ajili ya raia wa Tanzania ambaye aliukana uraia wa Tanzania na sasa anaishi nje ya Tanzania kama raia wa nchi nyingine. Ikiwa Mtanzania alishaukana uraia wa Tanzania na sasa anaishi nje ya Tanzania, ili aweze kuwa raia pacha inabidi kwanza arudi Tanzania, na labda aishi kwa kibali (residence/permanent permit) nchini kwa muda usiopungua miaka mitano, na ndio ataomba tena kuwa raia wa Tanzania na kumfanya awe raia pacha - ikiwa nchi ambayo ni raia wake kwa sasa inamruhusu kuwa raia pacha, na Tanzania itakubali kumpa tena uraia. Kwa hiyo ni vigumu kwa mtu aliyeukana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine kuwa raia pacha
- Uraia pacha unakuja kwa raia wa Tanzania ambaye anaomba uraia wa nchi nyingine kwa kuwa ameishi katika nchi hiyo kwa muda mrefu kwa residence/permanent permit, bila kuwa ameukana uraia wake wa Tanzania. Kwa hiyo uraia pacha kwa Mtazania hautolewi na serikali ya Tanzania kwa kuwa huyo mtu tayari ni Mtanzania, bali anakuwa nao mtu aliekubaliwa kuwa raia wa nchi anayokaa baada ya hiyo nchi kumruhusu awe raia wa nchi hiyo huku akiendelea kuwa raia wa Tanzania
- Uraia pacha hauji kwa raia wa nchi nyingine akiwa anaishi nje ya Tanzania. Mtu asiye raia wa Tanzania anakuwa raia pacha pale ambapo serikali ya Tanzania inamruhusu kuwa raia wa Tanzania kwa kuwa amekuwa akiishi Tanzania kwa residence/perment permit kwa muda mrefu kutokana na sababu kama kuoa/kuolewa, kuwa mwekezaji nk., na anaendelea kuwa raia wa nchi yake ya kuzaliwa
- Sio rahisi kuwa raia pacha, hata pale Tanzania ikiruhusu, kwa kuwa ili uwe raia pacha lazima uwe umeishi kihalali katika nchi nyingine kwa muda uisiopungua miaka mitano na nchi hiyo ikubali ombia lako la kuwa raia wake.Kwa hiyo hata Tanzania ikiruhusi uraia pacha ni watu wachache sana watakuwa raia pacha. Huwezi kuwa raia pacha kama ni raia wa Tanzania hujawahi kuishi nchi nyingine zaidi ya Tanzania au kama ni raia wa nchi nyingine hujawahi kuishi Tanzania kwa muda mrefu
- Hakuna kibali kinachotolewa na Tanzania au serikali nyingine kinaitwa "Raia Pacha". Uraia pacha ni hali inayokutokea kwa kuwa serikali mbili zinakutambua kuwa raia halali wa nchi hizo.