Wateule
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 390
- 368
Asante Mh. kwa majibu yako, ila hizo sifa zinazofanya mtu asiwe muoga kwenye siasa bado hazijanishawishi. Labda nikupe tafsiri yangu ya "mwanasiasa muoga" ndio labda tutaelewana vizuri. Mwanasiasa muoga ni yule anayekaa kimnya dhidi ya maovu ya kisiasa, kiuchumi, au kijamii kwenye nchi yake kwa lengo la kulinda maslahi yake binafsi, haswa cheo. Kwa maana hiyo, niliposema wewe "muoga", nilikumbuka zaidi kisa cha Ndugu yetu Tundu Lissu kupigwa risasi wakati wewe ukiwa ni waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani.
Katika sakata lile, mpaka leo serikali ya chama chako imeshindwa kuhakikisha uchunguzi wa kweli unafanyika, washambuliaji wanafahamika rasmi (sio kwa ushahidi wa kimazingira tu, ambao tayari una mashiko), na haki inatendeka kwa Lissu. Pamoja na danadana hizi, ilishindwa kuwajibika kama waziri kwa kuwa mstari wa mbele kuonyesha kwamba kile kitendo hakikubaliki kwenye nchi yetu, na ingebidi hata kujiuzuru kulinda heshma yako. Lakini, hukufanya hivyo, na yaliyotokea baadae hatuna haja kurudia. Pamoja na hayo, mpaka leo, bado kuna watu wamepotea (Azory, Saanane, nk) na wengine wanaendelea kutekwa na kupigwa (Mdude), lakini wewe upo kimnya, kwanini??
Mfano mdogo wa "ujasiri wa kisiasa" ni lile suala la Nape, ambaye mbali na mapungufu yake, alijaribu kulisimamia suala la uvamizi wa "Makonda" pale Clouds, ili haki itendeke. Matokeo yake alikuja "kutumbuliwa." Wewe hukutaka kutumbuliwa kwa sakata la ndugu yako Lissu. Hivyo basi, tunapozungumzia ujasiri wa kisiasa, tafadhali kuwa makini sana na hiyo mifano yako binafsi iliyokuwezesha kufika hapo ulipofika kwani sisi wananchi tunataka kujua zaidi kuhusu ulichofanya kwenye siasa kwa maslahi mapana ya jamii ya Mtanzania, je umefanya nini?? Kutuambia tu wewe ni "self-made politician," haitoshi. Asante.
Babo nasubiri majibu kutoka kwa Mh., sijui nitafanikiwa....