Duuuh, nimepitia hilo tangazo lao yaani eti kama wangetumia viwango hivyo vipya kwenye matokeo ya 2012 ufaulu ungepanda kutoka 43% hadi 93%.Ama kweli hii ni nchi ya miujiza ikizingatiwa kuwa hata hiyo 43% ilipatikana kwa njia ya mazingaombwe ambapo awali ilikuwa ufaulu wa 35%..
Ama kweli TZ...
Vituko vya elimu lazima mwaka huu vitaingizwa kwenye maajabu ya dunia nashindwa kuelewa hao wanaopanga madudu ya namna hiyo wanatumia ubongo au vichwani kwao kuna nini?
Big up rakesh uliona mbali hukukubali kudhalilisha taaluma yako kwa kufanya kazi chini ya uenyekiti wa prof asiyejua lolote kuhusu elimu. Nchi hii bwana! Maprofesa wote wa elimu wanaonekana hawafai hadi mwanasheria ndiyo anakuwa mtendaji mkuu kwenye elimu? Tuna kazi kubwa ya kufanya ili taifa...
Alichofanya Mchome na Bhalalusesa kutangaza huo UPUUZI inaonesha jinsi gani kuwa na elimu kubwa haina maana kuwa una maarifa na busara ya kupambanua lipi linafaa na lipi halilifai. Ni aibu sana kwa taifa. Naona Mungai ni afadhali kuliko Mchome, ukiangalia Maprofesa ndiyo wanaleta sera za...
Nami nasema Bravo sana Prof Mchome na Prof Bhalalusesa maana tuna uhakika wa watoto wetu wote watakaongia kwenye chumba cha mtihani kuwa watakuwa tayari wameshafaulu kwa hata alama 0 yaani 0-19 inaonesha UFAULU dhaifu sana. Cha msingi ni kuwa hata kama mwanafunzi akipata alama 0 maprofesa...
MKUU KUWEKA MAMBO WAZI NI KUWA HAYO NI MATUNDA YA KAZI YA VIGOGO WAFUATATO WA WIZARA YA ELIMU.
1. DR. SHUKURU KAWAMBWA - WAZIRI WA ELIMU
2. PHILIPO MULUGO - NAIBU WAZIRI WA ELIMU
3. PROF. SIFUNI MCHOME - KATIBU MKUU
4. PROF BHALALUSESA - KAMISHNA WA ELIMU.
Hao ndiyo wametufikisha hapa...
Mkuu utabiri wako umetimia Movie inaendelea sasa kila mtu anafaulu ila tu mwingine inaridhisha mwingine anafaulu hafifu. Zombi mwaka huu watapeta sana. HA HA HA HA, KILIO CHA WANANCHI KIMESIKIKA. MNATAKA WAPEWE 0 ILI WAJINYONGE! HAPANA BWANA HAO WAKO JUU SANA DARAJA LA V
Udhaifu wa Mulugo na Kawambwa ni mtaji kwa vyama vya upinzani. Kama wataendelea kuwepo hadi 2015, watapaisha sana kura za wapinzami. Huhitaji kujua kusoma na kuandika ili uweze kung'amua udhaifu uliokithiri wa uongozi katika elimu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.