Kampuni ya TUKUZA (Tuenzi na Kutunza Rasilimali Zetu Adimu), inahusika na uchakataji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za chakula, vipodozi asili, na kuendesha MAFUNZO mbalimbali. Kampuni imefanya kazi hizi toka mwaka 2014 hapa nchini Tanzania. Bidhaa zetu zina ubora wa hali juu na zinafanya...
Na Constantine J. S. Mauki March 2025
Utangulizi
Asilimia 60 ya mwili wa binadamu ni maji. Ila kwa mtoto mchanga asilimia 80 ya mwili wake ni maji. Kiwango hiki cha maji hupungua kadri ukuaji wa mtoto unavyoendelea; na hatimaye hufikia asilimia 60, ambayo ndio wastani kwa watu...
Wageni wa Kimataifa Wasifunge barabara jijini Dar.
Hivi karibuni tumekuwa na neema ya kupata wageni, wakuu wa nchi za Afrika jijini Dar kwa ajili ya mikutano.
Helkopta zitumike kuwatoa wageni uwanja wa ndege. Tusifunge barabara! Au mikutano hii ifanyike jijini Arusha.
Wajanja wanaowahi wanakula pesa. Ukitaka kufanikiwa usiogope kupoteza. Kipi Bora, kubeti au hii pyramid? Muhimu kufanya uchaguzi juu ya uhalali wa hii fursa na kufanya maamuzi sahihi, badala kukurupuka na kusema huu ni utapeli!!
Kwa muda mrefu, nimekuwa natafakari juu ya tabia za watu (kama kiburi, uvivu, ulevi, wizi na kila aina ya utovu wa nidhamu) na athari zake katika familia zao na hata kwa Jamii, nikagundua kwamba mtu mwenye mafanikio ni yule anayewaheshimu Wazazi wake. Mtu anayewaheshimu Wazazi wake, haishii...
Ni kweli, ameshatimiza ndoto yake ya miaka mingi ya kuwa raisi wa Marekani. Sasa akubali kumuachia mgombea mwingine. Aige mfano wa Nelson Mandela wa Afrika Kusini, ambaye alitawala kipindi kimoja tu cha miaka 5, akamwachia kijiti Thabo Mbeki. Lakini amesalia kuwa raisi Bora duniani!!
Tatizo lililopo hasa katika nchi zinazoendelea, viongozi waliopo madarakani wanafurahia mifumo iliyoachwa na watawala wa kikoloni. Hii ni mifumo ya watu wachache kuhodhi madaraka makubwa na kuamua hatma ya watu wote katika mikoa, wilaya na hata vijiji ambako kuna kuna viongozi pia.
Mwaka 1990, na kuendelea serikali ilianza kupunguza watumishi wa umma, wakati huohuo ikisitisha ajira mpya, ikiwa ni pamoja na waalimu na watumishi wa afya (ambao hawajawahi kutosha); hii ilifuatiwa na kufungwa kwa baadhi ya vyuo vya umma vya kati, vikiwemo vya afya, kilimo na ualimu. Huu...
Kampeni ya matumizi ya nishati safi, itachangia kuboreka kwa hali ya rasilimali asili, ambazo ni muhimu kwa upatikanaji wa uhakika wa tiba asili na mbadala!
Kuna baadhi ya watu wanamiliki maradhi! Utasikia MTU anasema, hii ni presha yangu, naishi nayo. Kumbe angeweza kuidhibiti na kuitokomeza kabisa kwa kubadili tabia.
Kwa mtizamo wangu, wafanya biashara wote wapewe machine hizi bure, kwani kazi ya mashine hizi ni kusaidia kukusanya kodi, na hili ni jukumu la serikali kupitia TRA.
Serikali kuu igatue jukumu la kugharamia elimu, kwa serikali za mitaa, taasisi mbalimbali (za umma na binafsi). Kabla ya Uhuru vyama vya ushirika viligharamia elimu ya watoto wa wanachama wao kuanzia msingi hadi vyuo vikuu! Jambo hili linawezekana hata Leo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.