Mkuu, 613k take home unalia hivi? Nilianza kazi na take home ya 400k, nikamfungulia wife kitu kwa mkopo, wife akawa sasa ananisevu hivyo kutokana na kukopa take home yangu ikawa 180k. Nilikuwa nasomesha mtoto shule private lakini nilimudu. Kodi ya nyumba ninalipa 100k pia, bado kodi ya biashara...
Mkuu umenifanya nicheke 😂😂😂. Ila hongera kwa mipango huo. Mimi sina mpango wa V8 bado, huenda huko mbele, nikihitaji nitakuja tena nipate ushauri kabla sijanunua.
Ni muhimu kupata maelezo maana wapo watumiaji wengi wanaoona ipi afadhali kuliko kwenda kichwa kichwa.
Siwezi kwenda speed kubwa mkuu. Nitaenda kama nasindikiza Mheshimiwa Rais kwenye kusalimia halaiki wakati wa sherehe za Uhuru 😂😂😂. Kikubwa ninachoangalia ni mafuta, uimara na uwezo wa kutembea njia ya rafu na lami.
Asante Mkuu. Haitasumbua kwenye miinuko na milima? (Japo sipandishi sana milima ila kuna ka Kilima hapa Iringa kuelekea Mjini ukiwa unatoka Dar kama utakuwa ulishafika). Nawaza kwamba kukapita kila siku kunaweza kuwahi kuchosha engine.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.