Wanaaamini ni wakati wao wa kuongea, wanaamini ni wakati wao wa kusikilizwa, sioni ubaya wa kutetea ndugu zao ikiwa wao angalau wana nafasi ya kusikilizwa zaidi.
Jiaminishe hivyo wewe ambae sio bure, unaweza kuelekezwa vigezo ni vipi lakini usiwe navyo hivyo vigezo......mara ngapi unasikia kuna nafasi ya kazi lakini kigezo uwe na uzoefu wa miaka kadhaa, lakini kwa vile huna hivyo vigezo kazi unawaachie wengine.
Madam President kwa speech ya leo ni wazi atapiga chini hilo wazo la kuifanya Chato Mkoa, ile kauli leteni mapendelezo tuyapitie, imetosha kabisa kwamba hakuna tena cha Mkoa wa Chato.
Watu wa CCM kuasi ni jambo la kawaida baada ya makundi yao kushindwa, ninachofahamu for sure pamoja huo uasi unaosema lakini busara ilitumika kumpa ubalozi badala ya kumfukuza kutokana na umuhimu wake ndani ya Chama.
Kama mzee Mangula ni lazima apige vema basi sioni kikwazo kwa Nchimbi maana hao ndio walikuwa CCM kindakindaki, wanakijua chama na wakati wa uongozi wao hapakuwa na hizi habari za ukanda na MATAGA PRAISE TEAM.
Binafsi nilikuwa namuona January kwenye hiyo nafasi ila tangu wadau wanitolee macho kuwa jamaa haitawezekana kutokana na dini, basi karata yangu nairusha kwa Nchimbi, hata nikititazama utendaji wake alipokuwa kiongozi wa UVCCM na jinsi anavyokijua chama, hapo naona kabisa anaweza kupata nafasi.
Mzee Mwinyi amejua kunifurahisha aisee, japo hotuba yake inakwama kwama lakini kaongea kama mtu mzima, huyu ni babu wa Taifa, full utani kila mtu kicheko.
Ajifunze kwa Mbowe huyu huyu mliyesema mlevi mpaka akavunjika mguu, leo hii mnaomba Lissu aandike mapambio baada ya kumdhihaki Nchi haiwezi ongozwa na mlemavu. Acheni hizo wakuu, tumalizeni msiba salama. JPM apumzike tumpe mama Samia nafasi ya kututoa hapa tulipokwama.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.