Recent content by Sandinistas79

  1. S

    Marufuku ya misongamano isiyo ya lazima. Je, kirusi kinaogopa misongamano ya lazima?

    Kwa kifupi dhamira ya kutekeleza afua muhimu za kudhibiti uviko haipo. Vinginevyo hata hili la kudhibiti mikusanyiko lingekuwa limeanza siku nyingi. Hata ufafanuzi wa mikusanyiko ya lazima na isiyokuwa ya lazima hautolewi. Mikusanyiko iliyolengwa ni ya kisiasa; husasan vyama vya upinzani.
  2. S

    Uonevu dhidi ya Mbowe: Viongozi wa dini toeni kauli ya kitume

    Kweli. Viongozi wa kiroho hawahitaji kutolea kauli maigizo ya wanasiasa kama haya. Badala yake wanastahili kutolea matamko mambo ya msingi yanayotatiza taifa kwa kipindi hiki. Ukweli ni haya maigizo ni mkakati wa watawala wetu kuzima madai ya katiba mpya. Tunajua kuwa viongozi wa kiroho waliunga...
  3. S

    Uonevu dhidi ya Mbowe: Viongozi wa dini toeni kauli ya kitume

    Viongozi wa kiroho waliunga mkono kwa dhati rasimu ya katiba mpya ya Tume ya Warioba. Haya ya ugaidi dhidi ya Mbowe ni mbinu ya kuzima moto mpya wa katiba mpya. Njia mojawapo ya viongozi wa kiroho kunusuru taifa letu sasa ni kuonyesha kuwa bado wanaunga mkono rasimu Tume ya Warioba ya katiba...
  4. S

    Hongera Rais Samia kwa kufuata nyayo za mtangulizi wako japo gharama yake ni kubwa kwa taifa

    Baba wa Taifa mwenyewe alituhakishia kuwa katiba yetu ilikuwa inamwezesha kuwa dikteta! Pamoja na hayo hakuwa dikteta kwa sababu mbali na kuwa na elimu nzuri pia alikuwa na karama kubwa ya uongozi. Waliomfuata nao walikuwa na elimu nzuri, karama ya kutosha ya uongozi na pia kwa sababu walifanya...
  5. S

    Hongera Rais Samia kwa kufuata nyayo za mtangulizi wako japo gharama yake ni kubwa kwa taifa

    N Hivi uimara wa kiongozi wa Tanzania ni kukandamiza uhuru wa raia kujumuika, uhuru wa mawazo, haki za kiraia, haki za binadamu, kuendekeza ubaguzi na kutumia dola kufanikisha hayo yote? Huu ni ujima mtupu.
  6. S

    Hongera Rais Samia kwa kufuata nyayo za mtangulizi wako japo gharama yake ni kubwa kwa taifa

    Kiongozi kufanya mambo mazuri kwa nchi yake ni wajibu wake; hiyo siyo habari kwa vyombo vya kimataifa. Habari zenyewe ni pale anapfanya kinyume na matarajio; hiyo ni habari kubwa. Mwalimu Nyerere alitmia mfano wa kumpiga mke. Kwamba kila siku wanaume hupiga wake zao lakini haiandikwi na...
  7. S

    Waziri Simbachawene: Mkurugenzi mkuu wa NIDA ajipime kama bado anastahili kuongoza taasisi hiyo!

    Watumishi wa serikali siku hizi wanajiuzulu kama wanasiasa? Umbilikimo unaongezeka kwa kasi kubwa miongoni mwa wanasiasa wetu. Nadhani wengi wanapata madaraka ya kisiasa bila exposure ys kutosha katika kutumikia umma na uongozi.
  8. S

    DC wa Ikungi amepiga marufuku mijadala ya Katiba

    Katika hali ya kawaida huyu asingekuwa DC; alishtakiwa kwa kumuomba rushwa mtumishi wa serikali. Hata kama alishinda kesi hakustahili kupata uteuzi; mke wa kaisari hapaswi hata kuhisiwa. Alipata uteuzi kwa sababu katika awamu ile kigezo kikubwa haikuwa uadilifu bali ukatili na ukichaa! Sijui...
  9. S

    Maandalizi ya kutawala mpaka kifo yalikuwa mengi

    Na propoganda machinery yake ilifanikiwa sana; kama ile ya Nazi. Sijui kama viongozi wa sasa waliojiapiza kulinda "legacy" yake wanajua kitu wanachofanya. Wanamjenga na kujidhoofisha wao wenyewe. Propaganda ya kipindi kilichopita iliwalenga wananchi wa kawaida wasiokuwa na uelewa wa kutosha na...
  10. S

    Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

    Huo ushahidi wa kupigiwa simu na IGP ukihitajika TCRA wanaweza kutoa. IGP mwenyewe anafanya mzaha tu. Tukio kubwa hivi polisi wanatoa majibu mepesi kiasi hiki? Nchi hii imeharibikiwa sana. Bahati mbaya kuna watu wanajidanganya kuwa nchi ikiharibikiwa hivi wao wanafaidika! Wasubiri waone. Si...
  11. S

    Fatma Karume: Nchi isiyoheshimu Haki za Msingi za Binadamu ni Nchi ya Kishenzi tu

    Halafu hao wanaozungumza kuua watu hupata uteuzi.
  12. S

    Warioba: Wananchi tunaowaita Wanyonge ndio wenye nchi, Katiba ni kipaumbele hata kwenye marekebisho Bungeni

    Nadhani Rais hana tatizo kubwa sana; kikwazo ni ccm mpya ya shujaa. Ndani yake wamejaa walinzi wa "legacy" siyo walinzi wa imani na ahadi za ccm pamoja na ustawi na umoja wa taifa la Tanzania.
  13. S

    Nani anastahili kujengewa sanamu ya kumbukumbu kati ya Mzee Nyerere na Magufuli?

    Wamjengee tu huyo wanaetaka kumjengea lakini tunachoamini wengi ni kwmba within our lifetime hiyo sanamu itaangushwa!
Back
Top Bottom