zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,628
- 3,155
Hakuna alipokandamizwa raia katika kujumuika au kutoa mawazo yake. Na wala hakuna haki za kiraia na haki za binadamu zilizovunjwa na kiongozi yeyote wa Tanzania. Hayo mawazo siyo yenu, mmekuwa brainswashed kutumia vimisamiati vya kibeberu hivyo ili kupenyeza ajenda zao ambazo kwa bahati mbaya zimekuwa zenu.N
Hivi uimara wa kiongozi wa Tanzania ni kukandamiza uhuru wa raia kujumuika, uhuru wa mawazo, haki za kiraia, haki za binadamu, kuendekeza ubaguzi na kutumia dola kufanikisha hayo yote? Huu ni ujima mtupu.
Na ajenda za kibeberu zinajulikana. Wanataka nchi na watu wetu wafuate model yao ya kimaisha ili iwe rahisi kwao kufanya wanachokitaka bila upinzani wowote. Na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia programmes nyingi, walizowekeza fedha nyingi, za muda mrefu, za kuformat namna ya kufikiria kwa watu wetu.
Sisi tunamtaka kiongozi wa Tanzania afanye mambo haya yafuatayo, akusanye kodi, asimamie pesa yetu vizuri iisipotee hata senti kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na watu wake, ahakikishe usalama wa nchi na watu wake, alinde na kuisimamia amani ya nchi yetu.
Akifanikiwa hayo who cares about vimisamiati vya kibeberu. Frankly speaking ni lini hivi nimekatazwa kutoa mawazo yangu?
Kuhusu kukamatwa Mbowe na lile genge lake, kwanza anatumiwa ujumbe kwamba who is the boss katika nchi hii. Mama ndiye boss kwa sasa akisema no ni no, akisema yes ni yes. Hata mimi hapa nikiwaambia walio chini yangu kwamba hiki hapana wananisikiliza, seuze Rais wa nchi. Kwa kauli ya Rais hakuna cha haki zya kufanya unachojisikia, and there is a good reason kwa nini imewekwa hivyo.