Waziri Simbachawene: Mkurugenzi mkuu wa NIDA ajipime kama bado anastahili kuongoza taasisi hiyo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,803
Waziri wa mambo ya ndani mh George Simbachawene amemtaka mkurugenzi mkuu wa NIDA ajitafakari kama bado anastahili kuiongoza taasisi hiyo.

Simbachawene amesema NIDA wameshindwa kutoa vitambulisho vya taifa kwa wakati mfano mkoani Iringa vimetolewa vitambulisho 160,000 huku raia wengine zaidi ya 400,000 wakisubiri kwa zaidi ya miaka mitatu sasa

Source: ITV habari
 
Yeye kwani hatakiwi kujipima?
 
Waziri wangu wa mambo ya ndani hili suala tumia busara,tuanze upya kabisa pamoja na kwamba tumechelewa mno,anza kwa kuhakikisha kuwa watoto wote wanaozaliwa sasa hadi miaka 10 wote wamepata birth certificates zenye ID number,

Watoto hawa wakifikisha umri wa miaka 16 ndio waombe IDs kwa kutumia birth certificates zao(hizi number zao ni lazima ziwe kwenye system's ya nchi nzima)

walio na umri zaidi ya miaka 16 kwa sasa hadi miaka 35 waombe hizi IDs kwa kutumia informations zingine kama za wazazi,shule na kazi ,baada ya kukamilisha group hili ndio ushughulike na 35+yrs maana uzuri utakua umeshaweka msingi mzuri.
 
Waziri wa mambo ya ndani mh George Simbachawene amemtaka mkurugenzi mkuu wa NIDA ajitafakari kama bado anastahili kuiongoza taasisi hiyo.

Simbachawene amesema NIDA wameshindwa kutoa vitambulisho vya taifa kwa wakati mfano mkoani Iringa vimetolewa vitambulisho 160,000 huku raia wengine zaidi ya 400,000 wakisubiri kwa zaidi ya miaka mitatu sasa

Source: ITV habari
Mimi changu ni mwaka wa pili huu na sina dalili ya kupata..
 
Waziri asisahau kuwa Idara ya Zimamoto ilioshindwa kuzima moto uliounguza soko la Kariakoo iko chini yake. Kwa mantiki hiyo naye awe wa kwanza kujipima!
 
Vifaa vilikuwepo vya kutosha? nilisikia mwaka jana wana mpango wa kuagiza vifaa toka nje, lakini sikuwahi kuona kama viliwasili na vyakutosha ili kukidhi mahitaji ya nchi nzima.

Simbachawene asitoe tamko kisiasa tu ili aonekane yupo ofisini anachapa kazi, aangalie na upande mwingine wa shilingi.
 
Watumishi wa serikali siku hizi wanajiuzulu kama wanasiasa? Umbilikimo unaongezeka kwa kasi kubwa miongoni mwa wanasiasa wetu. Nadhani wengi wanapata madaraka ya kisiasa bila exposure ys kutosha katika kutumikia umma na uongozi.
 
Hili suala la vitambulisho vya nida ni Jipu
Na nadhani kuna hujuma zinafanyika kukwamisha zoezi la kutupatia vitambulisho
 
Hivi Vitambulisho vya Uraia sio uthibitisho wa Uraia 🤣🤣

Yarabi stara.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom