Hongera Rais Samia kwa kufuata nyayo za mtangulizi wako japo gharama yake ni kubwa kwa taifa

Sasa sisi dunia nyingine inatuhusu nini, wakijua au wasipojua? Nchi ni ya kwetu, tutaijenga sisi, na tutafia humu humu. Tunafanya kile kilicho sahihi kwetu tu full stop; uraia wangu hauna ubia na mkenya au mbelgiji.
Habari ndio hiyo. Endeleeni kumpa kichwa huyo mnayemtegemea. Alipita Jiwe na wengine watapita. Ubatili mtupu
 
Wewe unaiona nchi upande wa udikteta.
Mm naiona Tanzania inayotazamwa kwa sera zake za kiuchumi siyo DEMOCRACY
Ninaiona Tanzania iliyonzukwa na vibaraka ndani ya CCM na Upinzani kwa tamaa ya madaraka,mali,visasi na ujuaji.

Naiona TANZANIA kama yatima aliye na walezi wanafiki na wanaotaka kumchukua ndiyo zaidi ya mnafiki wa kwanza.
" Na hii hoja ikatunzwe katika makabati yote kwenye bara la Afrika "- Mkalimani's voice.....naunga mkono hii hoja...Tz viongozi wake wengi ni bad-faith actors
 
Mama hapaswi kufuata utawala wa mwendazake.Kilichompata marehemu lazima kiogopwe.hatujazoea utawala wa kihuni kwani gharama zake hazisemeki.
 
Hivyo vyombo vya kimataifa havijawahi report mema ya Samia hata siku mojamoja

Huyo mbowe yupo salama kabisa ila urais kwake ndio wasahau
Kiongozi kufanya mambo mazuri kwa nchi yake ni wajibu wake; hiyo siyo habari kwa vyombo vya kimataifa. Habari zenyewe ni pale anapfanya kinyume na matarajio; hiyo ni habari kubwa. Mwalimu Nyerere alitmia mfano wa kumpiga mke. Kwamba kila siku wanaume hupiga wake zao lakini haiandikwi na magazeti; siyo habari. Subiri siku Nyerere akimpiga mke wake! Hiyo itakuwa habari kubwa.
 
Habari ndio hiyo. Endeleeni kumpa kichwa huyo mnayemtegemea. Alipita Jiwe na wengine watapita. Ubatili mtupu
Sisi hatumtegemei mtu wala nini. Tunachoangalia ni misingi tu. Tulimtahadharisha mapema mama kwamba hii nchi haina ubia na taifa au mataifa mengine, itajengwa kwa mikono yetu wenyewe tu. Watakaotaka kutusaidia watusaidie kwa nia safi sio kwa ajili ya ajenda zao. Vinginevyo mama atapata tabu sana kuiongoza hii nchi maana wale wanaotaka awe dhaifu ni vibaraka, sisi tunaotaka awe na nguvu na kufanikiwa ndio tunaomtaka aangalie maslahi ya nchi kwanza na asicheke na kima yeyote mwenye vipaumbele vingine zaidi ya maendeleo ya nchi yetu.

Wanaotaka katiba mpya watwambie kipengele gani kwenye katiba ya sasa kinakwamisha maendeleo ya nchi na watu wake.
 
Huyu mama wakuhurumia sana, amewakumbatia wasiompenda na wasiomtakia mema, kundi lote la maggufuli halimtakii mema hata kidogo.
Wanatamani kumuona akifeli waweke mtu wao.
Pole kwake kwa uchaguzi mbovu
Ni kambi ipi ilitaka asiapishwe,nani alikuwa kinara wa mpango
 
Ukweli ni kwamba wote ni watanzania na hii nchi ni yetu sote siyo ccm wala chadema kama kuna hoja zinatolewa na Zina mashiko serikali na chama tawala jibuni hoja Kwa hoja dunia ya leo imebadilika sana jitahidini kwenda na dunia ilipo ubabe, kutumia polisi, usalama wa taifa na jeshi kujibu hoja za wananchi au wapinzani wenu huo ndo ushamba pure na kuwaamsha walio lala
 
N
Sisi hatumtegemei mtu wala nini. Tunachoangalia ni misingi tu. Tulimtahadharisha mapema mama kwamba hii nchi haina ubia na taifa au mataifa mengine, itajengwa kwa mikono yetu wenyewe tu. Watakaotaka kutusaidia watusaidie kwa nia safi sio kwa ajili ya ajenda zao. Vinginevyo mama atapata tabu sana kuiongoza hii nchi maana wale wanaotaka awe dhaifu ni vibaraka, sisi tunaotaka awe na nguvu na kufanikiwa ndio tunaomtaka aangalie maslahi ya nchi kwanza na asicheke na kima yeyote mwenye vipaumbele vingine zaidi ya maendeleo ya nchi yetu.

Wanaotaka katiba mpya watwambie kipengele gani kwenye katiba ya sasa kinakwamisha maendeleo ya nchi na watu wake.
Hivi uimara wa kiongozi wa Tanzania ni kukandamiza uhuru wa raia kujumuika, uhuru wa mawazo, haki za kiraia, haki za binadamu, kuendekeza ubaguzi na kutumia dola kufanikisha hayo yote? Huu ni ujima mtupu.
 
Back
Top Bottom