DC wa Ikungi amepiga marufuku mijadala ya Katiba

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Haya ni maneno machache ambayo DC @jerrymuro1980 ameyatamka huko Ikungi -Singida ,mengi zaidi ameyasema katika Audio inayosambaa akiwa anazungumza na viongozi na wananchi huko Ikungi.

Moja ,ni hili la kupiga marufuku mijadala ya katiba na kupinga mikusanyiko.

Mbili,Akitamka yeye ndio mkuu wa wilaya wa Ikungi na mwenyekiti wa ulinzi na usalama ana mabomu,Askari na majeshi.

Tatu,Anatishia wananchi wenye malengo ya uongozi,kwamba kama unataka udiwani au uenyekiti anza kuleta mbao , Cementi au jenga madarasa.

Nne,Anatamka katiba inasaidia nini ? katiba ni karatasi tuu inaandikwa.

Tano, Kutamka huu sio wakati wa kufanya siasa ni wakati wa maendeleo ,sidhani kama anajua tafsiri ya siasa.

Sita,Kutamka kwamba watu wenye nia ya kunitengenezea ni kwame ,watakwama wao ,nawajua msipobadilika leo nitawavuruga.

Haya ndiyo maneno kadhaa aliyotamka DC wa Ikungi mpya @jerrymuro1980 .Mimi leo nitajikita kumpa elimu kidogo kuhusu mamlaka ya kiongozi na mamlaka ya wananchi ili akiwa anaongea na wananchi awe na nidhamu kubwa.

Kwa @jerrymuro1980 na viongozi wengine wa umma, lazima mfahamu wananchi ndio mabosi zenu wakubwa (Sovereign) ndio wenye mamlaka ya juu/makubwa na ya kudumu (Supreme and permanent Authority) hivyo mnapoteuliwa kwenda kumsaidia Rais kazi ya kuhudumi wananchi hampaswi kujiona nyinyi ni wakubwa zaidi ya wananchi. (Above Popular Sovereignty).

Hakuna kiongozi mwenye mamlaka juu ya wananchi kuanzia Rais hadi mwenyekiti wa kijiji wote wanapewa mamlaka na wananchi (Soma katiba ibara ya 8 (1) a,b,c,d .Hivyo wananchi wanapaswa kuheshimiwa kwa kiwango cha juu sana na hata unapoongea na wananchi unapaswa kuwa mnyenyekevu sababu wao ni principal wewe ni Agent wao.

Hupaswi kutisha wananchi,hupaswi kujiweka juu zaidi ya wananchi,hupaswi kujikweza mbele ya wananchi,hupaswi kujidemshademsha mbele ya wananchi,hupaswi kukejeli wananchi ,hupaswi kuwadogodesha wananchi . Kazi kubwa ya kiongozi anapaswa ashawishi ili kuongoza gurudumu la kufikia maendeleo. (You have to influence the people/citizens ) ili kufikia maendeleo yanayokusudiwa sio kutisha,kujikweza ,kuamulia watu No ,No, No, BIG NO.

Nyerere aliwahi sema "No Tanzanian has the right to say l know what is good for Tanzanians and others must do it ,but all Tanzanians have to make decisions for Tanzania" .

Huwezi pangia wananchi kama watoto wako kipi cha kufanya, huwezi tishia wananchi kama watoto wako wakutii na kukuogopa wewe, na huwezi kemea wananchi kama watoto zako.

Anasema katiba ni karatasi tuu haileti chakula, kama katiba ni karatasi kwanini alipoapa kuwa DC alitamka katika kiapo "Nitafanya majukumu yangu kwa kuzingatia katiba" ? . Viongozi wasioelewa maana ya viapo vyao hawapaswi kuwa viongozi, viongozi wasioelewa mamlaka ya wananchi hawapaswi kabisa kuwa viongozi.

Mtu mwenye akili timamu hawezi kuhoji mahusiano ya katiba na maendeleo, katiba mbovu na umaskini, Katiba na mlo wake sababu ni mambo ambayo yapo wazi kabisa.

Kwa yeyote, pata kusoma kitabu cha John Elster 1994, kinaitwa "Impact of Constitution on Economic Performance " ameelezea vyema sana namna katiba inavyoharakisha maendeleo ya kiuchumi.

Anasema " The constitution doesn't generate economic wealthy directly , but structures the political outcomes which in turn affect the economic performance ". Na political outcomes zinazokuwa structured na kutengenezwa katika katiba ni,

1.Misingi ya uwajibikaji (Values of accountability) mfano,leo hii Mbunge anayechaguliwa na wananchi hawezi kuwajibishwa asipowajibika madhubuti katika kuwakilisha wananchi wake,leo hii viongozi wa Tume ya uchaguzi wanateuliwa na Rais hawawezi kuwajibika ipasavyo ili kuwa na uchaguzi huru na haki.

Leo hii katika wilaya zetu kuna ma Rc na Dc wateule kama Muro wasio na hofu na wananchi sababu ameteuliwa tuu hawezi hivyo wajibika ipaswa mfumo huu wa unitary System of government haufai bora Federal system of Government (Provincial system) ,leo hii matokeo ya urais hayapingwi mahakamani hakuwezi kuwa na uwajibikaji imara kwa chama kilichopo madarakani sababu wao wanaamini milele watatawala hivyo uwajibikaji hakuna.

Leo hii katibu wa muhimili wa Bunge anateuliwa na Rais hakutakuwa na Bunge imara lenye kuwajibika kuisimamia serikali,leo hii viongozi wa umma wanatenda watakavyo sababu hatuna misingi,maadili na miiko ya viongozi wa umma iliyoelezewa kwa umaridadi na kuweka mipaka (Soma ibara ya 13,20,21 na 22 katiba ya Warioba),leo hii Rais,Makamu,Waziri mkuu hawashtakiwi hatuwezi kuwa na viongozi wanao wajibika ipasavyo,leo hii Mbunge sifa yake ni kusoma na kuandika hatuwezi kuwa na wabunge imara wenye kuelewa majukumu yao haswa katika kuisimamia serikali.

2.Misingi ya uimara wa taasisi ndani ya Serikali na nchi (Stable institution in the country and government) ,leo hii jaji mkuu na majaji wa Mahakama wanateuliwa na Rais ,CAG mlinzi wa fedha zetu anateuliwa na Rais bila masharti,Tume ya uchaguzi inateuliwa na Rais bila masharti ,Bunge= katibu wa Bunge huteuliwa na Rais,Rais aweza vunja Bunge lisipopitisha Bajeti ,DPP kuteuliwa na Rais bila masharti.

3.Misingi ya ubashiri (Value of Predactibility) yaani kuwa na viongozi watakao ongoza kwa kufuata taratibu zilizopo na sio kufanya maamuzi kulingana na alivyoamka asubuhi.Mfano tuliwahi kuwa na Kodi ya Nyumba na Mabango kukusanywa na Halmashauri (Serikali ya mtaa ) Sababu tuna katiba ambayo hailindi D by D (Decentralization by Devolution) hakuna masharti , Serikali kuu ikakwapua hizi kodi matokeo yake Halmashauri zikapata shida sana kutekeleza miradi yake baadaye wakarejesha tena Halmashauri.

Tuwe na nchi ambayo itakuwa na mifumo imara tuondoke kutegemea kuongozwa kwa utashi wa kiongozi aliyejuu ila misingi na taasisi imara , katika misingi hii ndio tutaona maendeleo ya kiuchumi. Maendeleo ya kiuchumi hupitia katika mchakato wa misingi ya uwajibikaji na uimara wa taasisi ambayo chanzo cha haya ni Katiba ya wananchi.

Hivyo sitarajii kiongozi kama DC kutoona mahusiano ya katiba na maendeleo ya kiuchumi ya wananchi .

Hili la kusema hataki siasa , nitatolea uelewa siku nyingine ili ajue maaana ya siasa na mahusiano ya siasa katika maisha yetu ya kila siku.

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana- Act wazalendo Taifa.

IMG_20210716_113559_649.jpg
 
Tunakuja kupiga kambi wilayani kwake na wimbo ni katiba mpya, akiweza atukamate, atufunge , vile tu ataamua, kwani sii makosa kuzungumza, zaidi kuhusu Katiba, katiba ina tupa Uhuru huo.
 
Hivi huyo mkuu wa Wilaya ana akili timamu au kuna wakati huwa anapatwa na uwendawazimu?

Huo uDC anadhani umemfanya yeye kuwa mtanzania zaidi na mwanadamu zaidi? Kama kweli kayatamka hayo, Mh. Rais amwondoa kichaa huyo kwenye hiyo nafasi haraka. Aende akapate matibabu. Mtu mwenye magonjwa ya akili, huwezi kujua atafanya nini kesho au keshokutwa. Tusije tukaja kujilaumu kwa kutochukua hatua mapema shidi yake.
 
Hivi huyo mkuu wa Wilaya ana akili timamu au kuna wakati huwa anapatwa na uwendawazimu?

Huo uDC anadhani umemfanya yeye kuwa mtanzania zaidi na mwanadamu zaidi? Kama kweli kayatamka hayo, Mh. Rais amwondoa kichaa huyo kwenye hiyo nafasi haraka. Aende akapate matibabu. Mtu mwenye magonjwa ya akili, huwezi kujua atafanya nini kesho au keshokutwa. Tusije tukaja kujilaumu kwa kutochukua hatua mapema shidi yake.
Huyu ni chizi kabisa amelaaniwa, alimsaliti mzee Mengi kwa Manji na Manji akamsaliti kwa dikteta/Makonda
 
Ahamishiwe huko Iringa akatamke kwa dharau kama mwenzake Happy akajikuta anatowa matamko makaburini
Nasikia alidharau wastaafu
 
Muro bado yupo enzi za mwendazake.
Hawa ni watu wasio jua kuwa mamlaka aliyo nayo juu ya jeshi letu, kuwa yametokana na katiba. Wazazi wake hawakuwahi kumpa nguvu juu ya jeshi letu, katiba ikibadili hili, yeye atakuwa hana kauli juu ya hao wananchi pia katiba isipomlinda, hata kuuwawa anaweza kuuwawa na wananchi hao hao.
Yeye anafikiri nguvu alizo nazo aidha alizaliwa nazo au amepewa na aliye mteua toka katika ukoo wake.
 
Hivi huyo mkuu wa Wilaya ana akili timamu au kuna wakati huwa anapatwa na uwendawazimu?

Huo uDC anadhani umemfanya yeye kuwa mtanzania zaidi na mwanadamu zaidi? Kama kweli kayatamka hayo, Mh. Rais amwondoa kichaa huyo kwenye hiyo nafasi haraka. Aende akapate matibabu. Mtu mwenye magonjwa ya akili, huwezi kujua atafanya nini kesho au keshokutwa. Tusije tukaja kujilaumu kwa kutochukua hatua mapema shidi yake.
Katika hali ya kawaida huyu asingekuwa DC; alishtakiwa kwa kumuomba rushwa mtumishi wa serikali. Hata kama alishinda kesi hakustahili kupata uteuzi; mke wa kaisari hapaswi hata kuhisiwa. Alipata uteuzi kwa sababu katika awamu ile kigezo kikubwa haikuwa uadilifu bali ukatili na ukichaa! Sijui kama SSH naye anawataka watu wa aina hii. Laikini alituahidi kuwa atakuwa anaangalia mabega!
 
Back
Top Bottom