Kuna mtu kakuandikia au ni wewe mwenyewe???!!! Ukianza kusoma alichoandika mleta mada hata kabla hujamaliza unagundua kwamba ametumwa au amejituma kubashiri kitakachosemwa na viongozi wa KKKT kama salamu za mwaka mpya. Nia ya bandiko lake ni ku discredit salamu hizo kabla hazijatoka ili zikitoka...
Hii ni janja ya walioharibu uchaguzi, huu uchomaji wanaufanya wenyewe,lengo ni kukwepa aibu na kuhalalisha urudiaji mzima wa hatua zote za uchaguzi pale upinzani utakapogoma kabisa kushiriki kwa njia yoyote kwenye huu uchaguzi wa sasa. Watajaribu kuvimba kwamba uchaguzi wa tarehe 24 utafanyika...
Contradiction, hawa watu kila mwezi wanavuka lengo, iweje tena nusu ya mwaka wakawa wamekusanya asilimia 62?!!! Au hesabu za asilimia zimebadilika siku hizi sio zile tulizokua tunafundishwa zamani
Jambo la msingi SGR ijengwe ili ionyeshwe kwa wapiga kura, tunataka kuwaumbua wapinzani, hilo ndio lengo kuu. Baada ya hapo tutatangaza tenda kwa ajili ya kuandika business plan ya kuendesha SGR. Hakuna linaloshindikana chini ya jua, hasa kwa serikali yetu hii sikivu. Kuhusu suala la kujiendesha...
Ambazo zitasaidia kulipa wakulima wa korosho, kuongeza mishahara kwa wafanyakazi, kuwapa ajira watu wote waliofukuzwa kazi, zitasaidia pia kurekebisha kikokotoo cha mafao, zitasaidia sana kuongeza bei za mazao yanayododa kwenye maghara kama vile mahindi, vilevile hizi Ea Basi zitapunguza kodi...
Tanzania mpya inakuja...ni kweli mkuu, hii ni Tanzania mpya kwerikweri haijawahi kutokea ulimwenguni, tutembee vifua(wazi) mbere kma tumepigwa ngumi ya mgongo. Tukipata nimonia bahati mbaya
Haya "Mabeberu" yatakua maongo. Yanatudanganya eti watoto wetu wakipata mimba hawaruhusiwi mashuleni, yanaleta uongo eti wapinzani wanalimia meno, bila aibu yanadanganya eti hakuna uhuru wa habari, mara katiba inasiginwa, haijaishia hapo inajaribu kutuaminisha eti tunawanyanyapaa wakosefu wa...
Ungejiridhisha kwanza na alichoandika pascal, haya uliyoandika mpaka naona aibu mimi. Kweli elimu inahitajika kwa kizazi hiki cha instagram. Pascal tafadhari uache sasa mambo ya sarcasm(kisengerenyuma), unawachanganya watu
Mi napenda huyu sisimizi aendelee kumvimbia tembo, tena natamani ajitutumue "kwerikweri". Hii itatuharakishia kifo cha " sisimizi". Baada ya hapo ni kazi na bata
Duuh, leo umeamua kufunguka kabisa, mara nyingi umejitahidi kutumia mzunguko mrefu wa uandishi wa kinyumenyume lakini leo umeona isiwe tabu, liwalo na liwe, hongera brother
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.