Una uhakika na makosa waliyopatikana nayo ni ya uhujumu uchumi au ufisadi au unajiropokea tu. Hawajakutwa na kosa kama hilo hivyo sioni Sheria kama udhaifu. Acha chuki zisizokuwa na msingi. Watu wanateswa Kwa makosa ya kubambikiana tu
Ukisikia kumenoga sasa huku ndo kunoga kwenyewe, kaamua kusema ukweli. Hivi kama siyo kuwa zuzu kwa kinachoendelea sasa hivi kwa mtu mwenye akili timamu kuna haja gani ya kupoteza muda na nguvu huku ukijua ni kufanywa rubber stempu au stepping stone? Tafakari chukua hatua
mchezo ulioanzishwa na baadhi ya wakuu wa wilaya wa kutumia wanafunzi kuwapigia kura walimu wenye tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi ukome maana wanafunzi wanaweza kumpigia kura mwalimu anayewajibika na kuwachapa viboko huku mwalimu mzembe akionekana msafi.
Lakini pia mwalimu mwenzie au mtu...
Wewe ndo huna elimu na unaonyesha ujinga mbele za watu na kuwa mbaguzi mkubwa, huyo mzee wa watu kama angekuwa na njaa asingeweza kupata pesa ya kusafiri kwenda Nairobi kumuona Lissu. Njaa inakusumbua wewe si sheikh Ponda. Okay, Ponda anawatetea makafili je wewe unawatetea akina nani?
inaelekea polisi walijua kabla nini Sheikh Ponda angesema, haingii akilini kwamba yeye alipanga aongee saa nne na baadaye akabadilisha gear angani akawapigia simu wanahabari wachache kuongea kabla ya saa nne na polisi wakawepo. Ina maana alikuwa ameomba ulinzi wa polisi au polisi ni kati ya...
Ni makala nzuri sana iliyosheheni historia ya hili neno UCHOCHEZI lilivyoanza na linavyotumiwa na watawala. Pengine kosa nilipeleke kwa mlm Nyerere maana alijua nia ya hiyo sheria na kipindi alichokaa madarakani alitakiwa kuifanyia mabadiliko ili iwape uhuru raia kuhoji yanayofanywa na viongozi...
Kutowasema ni kutoitendea haki nafsi yako. Hao wanaofanya upuuzi baadaye mambo uwatokea puani. Hayo mahusiano ya vyuoni baada ya kumaliza masomo pair nyingi upotea. Tatizo huwa ni kubwa kwa mabinti maana wanaomjua hawakubali kumuoa.
Ikitokea kapata bwana na huyo bwana akajaribu kuulizia...
wakati mwingine tutumie akili ndogo tu. Hivi kama mtu amekubali kosa la wizi au ukiukwaji wa taratibu kinachofuata ni kukaa naye kwenye meza ya mazungumzo (negotiation)?. Kinafuata hapo ni kuomba msamaha na au kupokea masharti toka upande wa pili. Logic should prevail
Tatizo ni pale tunapojaribu kutibu dalili za ugonjwa badala ya chanzo cha ugonjwa. Huo ugonjwa hauponi ng'o bali inakuwa kama mtu unapoteza resources bure. Ukiyakamua majipu yanayosababishwa na staphylococci walio ndani ya mwili bila kumpa dawa ya kuwaua staphylococci ujue unafanya kazi bure
Binafsi natoa pongezi nusu hadi nione faida ya harakati zote hizi. Nimeshindwa kumuelewa zitto ambaye siku zote alikuwa mstali wa mbele kupiga kelele kuhusu mikataba mibovu, CCM haikumsikiliza halafu leo anakuwa wa kwanza kupongeza kamati hata kabla ya kuwakumbusha juu ya kutokuwa sikivu...
Nakubaliana na mapendekezo yako ila ongezea na pendekezo la CCM kuhusika na upotevu wote wa pesa hizi hivyo kama chama kijitathimini na kuachia ngazi. kama ni halali kujinadi na mazuri yaliyofanyika CCM ikiwa madarakani basi na huu ufisadi unawahusu. Wapo watu waliokuwa wakipiga kelele lakini...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.