CHAMA CHA MAPINDUZI kitakapobadili sera yake ya Muungano wa Serikali Mbili, sera yake mpya itakuwa sera ya Muungano wa Serikali moja. Chama Cha Mapinduzi chenye wanachama wenye akili, na ukweli, na ujasiri, hakiwezi katu kukubali sera ya serikali tatu, kikijua wazi wazi kwamba matokeo na shabaha...