Kuna watu bado wanaamini wakishamtolea mwanamke mahari ni sawa na kununua Ng'ombe wanahaki ya kufanya watakavyo. Kwa akili za hivi, ndio maana wazungu wanatufananisha na gorilla.
Pole kwa unayopitia, mpaka Ile Imani ya kwamba kuolewa ni kustirika kwa mwanamke, itabaki kuwa jukumu lako kuilinda hiyo ndoa. Wabongo bado tunasafari ndefu katika sio tu kiuchumi bali katika ustaarabu pia hata ukisoma maoni ya wadau wengi humu utaona tulipo.
Wewe unapenda sana majanga, mtu una familia Yako, usitulie!! Unatafuta nini kwa ex?!! Unataka bahati mbaya itokee umsingizie shetani?!! Itapendeza kama atakutenda maana mwana kulitafuta.
Naona sawa tu kama inawasaidia kwenye biashara zao maisha yenyewe yashakuwa magumu. Maisha ni kusaidiana. Au kwani Kuna madhara makubwa naweza pata kama mteja zaidi ya kuvutika kwenye hiyo biashara?!!
Ooh, kumbe mjadala ni kuhusu Israel! Huku, sina ufahamu na yanayojili maana Mimi si muumini wao. Nilikuwa tu nakujibu hoja Yako juu ya kauli ya kanisa kuhusu wanasiasa.
Maana ya 'ukipigwa shavu la kushoto, geuza na kulia' ni kwamba usilipe kisasi. Hawajalipa kisasi, hawewi kufanya hivyo ni kinyume na Imani, "wametii amri ya mamlaka"
ULichokisema upo sahihi, dini haipaswi kupingana na mamlaka, wanatakiwa kutii mamlaka, na ndio maana wameanza na hili
.. wameambiwa wasichanganye/ wasifanye siasa kwenye nyumba za ibada hivyo basi wametii hiyo amri kwa kuwaweka katazo la wanasiasa kuongea kwenye nyumba za ibada. Hawajakatazwa...
Ni hatari sana kuwa kwenye mahusiano tu eti kisa huna pa kwenda ukiachwa maana umezalishwa, au kutegemea kuja kugawana mali mkiachana sijui.. Kuna ujinga mwingi hapo hata kufurahia maisha inakuwa kwa mbinde. Kama mahusiano yakibiashara yanaweza kuvunjika na Kila mmoja akaendelea kivyake kwanini...
Kabisa, Kila mtu anasababu zake. Sio wanaume tu ndio wakuogopa vifungo visivyo vya lazima. Kikubwa ubongo na moyo vifanyekazi kwa kujitegemea katika majukumu yake.
Mmh! Inategemea kwanini uko katika hayo mahusiano, kama ni kwa ajili ya ndoa, basi hakikisha ushauri wa mtoa mada unauzingatia haswa.. Ila kama ni kwa kwasababu zingine usiogope Kikubwa unajua unachokofanya
Unaweza kuwa na simu ya ziada, unaweka line ya bongo kama bado ipo active then unaruhusu roaming, utaendelea kupata sms za mtandao husika za matangazo au miamala, au ukitaka kupiga, kupokea au kutuma sms unanunua kifurushi Cha kimataifa..
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.