Mtoa mada tafakari majukumu ya Hawa wakuu wa shule na walimu wakuu.Kuna mengi wanapitia wakati mwingine Hadi kukopa ili tu mambo ya shule yaende vizuri.Serikali ilifanya vizuri kuwapa hizo posho.Hizi posho hazina uhusiano na kukosa ajira.
Sheria ipo Hadi Leo.Muislam akiamua kuwa akifa mali yake igawanywe kiislam itagawanywa. Endapo familia yake ikiamua kuwa mirathi igawanywe kiislam pia itagawanywa.Serikali haijawahi kuingilia mambo yanayohusu Imani kukwepa kuvunja ibara ya 19 ya Katiba ya Tanzania.
Inategemea mirathi imegawanywa kwa utaratibu gani. Wapo waislam ambao hugawa mirathi kwa utaratibu Wa kiserikali au kimila.Ila kwa Sheria ya kiislam mtoto Wa nje ya NDOA hapati chochote.
Umekasirika sana!
Samahani sana kwa kukukosea, ni aula sana kufanya mijadala na watu waliokuwa na busara na hekima kubwa kama wewe. Nilidhani kuwa Kuna kundi ambalo limependelewa na wengine wakaachwa kulingana na maelezo yako ya awali na hata haya.Kumbe si hivyo nimekosea nisamehe bure maana...
Suala hapa siyo Kodi,mtoa mada uwe wazi unahofu na Hilo box.Nami nimekuelewa hapo kuwa unahofu na matokeo ya wale watakao fundishwa hasa upande Wa pili.Usipige chenga kusingizia Kodi kwani hao wengine hawalipi Kodi. Masomo ya dini zote yanafundishwa acha watoto wanaotaka wasome.Wengine hawana...
Bado Sijapata mantiki ya hoja ya kupinga tahasusi mpya.Ina maana mwanafunzi anaposoma Somo la dini na masomo mengine mawili tena Kwa hiyari yake ni madhara gani hutokea?.Mbona wanapoenda vyuo vikuu zipo shahada zinazohusu dini.Nilidhani labda watakosa maarifa ya awali wanapoanza shahada zao...
Mwalimu umeghadhibika.Maneno yako yanakuondolea Haiba ya kiualimu.Kukiri kosa siyo udhaifu,unajirekebisha mambo mengine yanaendelea.Hata walimu wanaofanya kazi kizembe siyo wote ni baadhi tu.
Sheikh Kishk ni Sheikh anayeona mbali.Wangekuwepo mashekh wengine kama yeye Jamii ya kiislam ingebadilika.Tatizo wapi wachache Wa aina yake na hawapewi nafasi kuongoza Jamii ya waislamu Wa Tanzania.
Jambo Hili la DP World linafunzo kubwa sana kwa mtanzania aliye makini.Kwa namna yoyote ambavyo litaisha tayari limeshaacha dosari na maswali mengi kwa watanzania.
Sasa hapo wakulima ndiyo tunao umia.Kama bei zikishuka maana yake kurudi shamba inakuwa ngumu lazima uzalishaji upungue.Sababu ni kuwa kilimo kitakuwa hakina maana tena.Kama ni tahadhari hamna shida.Sisi siyo vibarua wakuzalishia chakula watu wengine bila kupata kitu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.