Na mbaya zaidi alisema kuwa "wabunge wasiwaogope wananchi kwani itakuwa kelele za mitandaoni tu". Yaani ni kauli ya dharau na bahati mbaya wenzake walimpgia makofi. Inasikitisha sana.
Dalili ya wazi kabisa ya wasaka-tonge kufilisika akili. Yaani katika changamoto ambazo zinalikabili taifa hili waowakaona hiyo ni mojawapo!? Tunasema basi "MWENDAZAKE". Sasa wafanye watakacho.
Msaka-tonge akiwa kazini. Mama ajihadhari na na komba-mwiko huyu, ni hatari.
Ni huyu alishauri JPM tusiwe tunapewa taarifa za maambukizi ya Covid-19 na tusishangae tukianza kutoa taarifa hizo akawa wa kwanza kusifu na kuuzodoa utawala uliopita. Unafiki ni moja ya kazi ngumu sana. Unapaswa...
Mama anajibainisha kama kiongozi asiyetaka mbwembwe! Wote wanaotaka mbwembwe wakaunde makundi ya sanaa za vichekesho kwani nayo ni shughuli halali na pia yenye kuelimisha jamii, lakini kutumia u-RC kufanya hivyo HAPANA.
By the way, Mama alimchelewesha sana huyu. Kati ya teuzi za Wakuu wa Mikoa...
Ndugu yangu Bunsen Burner, nakushauri usome historia kidogo kuhusu Waingereza. Utabaini kuwa walitawaliwa na Wafaransa, na katika kutawaliwa huko walioonekana wasomi na wastaarabu ni wale walioweza kuzungumza Kifaransa.
Baada ya mamia ya miaka ya utawala wa Wafaransa, Waingereza walianza...
Kama JPM alivyochukua maamuzi magumu kwa kutekeleza viporo vya maamuzi ya tawala za nyuma kama vile; kuhamia Dodoma, kujenga bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, kadhalika Mama Samia naye anaaswa kuweka alama yake kwa kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya kufundishia katika ngazi...
Najiona mwenye hatia nisipopongeza maoni yako! Asante! Ni Kiswahili kitakachowakomboa Watanzania na sio lugha ya kigeni. Tunaweza kujifunza lugha hizo lakini Kiswahili kikawa lugha kuu ya kufundishia kama tunavyokitumia kwenye mawasiliano.
Huyo Fred bungeni haongei na unaambiwa jimboni hakuna cha maana kinachoendelea. Akitoka zake Dodoma ni Dar...! Masaini aende kufanya nini huko? Na hata akiendea kampani yake ni ya wachapa kinywaji na hana muda wa kuonana na watu wa kawaida.
Kwa Monduli huyo ni mbunge-hasara tosha. Kwanza inasemwa ni chapombe wa kukata na shoka. Pili, huyo alibebwa na baba yake, hivyo maendeleo ya jimbo hilo yataendelea kutegemea ushawishi wa mzee huyo kwa watawala walio madarakani.
Wenye Monduli yao wanasema yule aliyeshika nafasi ya tatu kwenye...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.