Mkuu kuhusu hii bima yetu ya NHIF ni majanga tu. Ukitegemea pesa ya Bima kuendeshea kituo utakifunga tu. Malipo kwa sasa wengine inawachukua hadi miezi sita. Na malipo yanakuja pungufu wakidai kwamba kuna udanganyifu na makosa yalifanyika katika utoaji wa tiba.
Kipindi cha nyuma Bima...
Ila mkishastaaf ndio akili ya biashara inaanza kuja akilini mwenu. Ukiona kuna fursa ina maokoto zaidi ya udaktari kwanini usiupige chini. Hizo ni kazi za wito lakini kama unataka pesa unapoteza muda mkuu
Dhumuni la wewe kusoma udaktari ni kutibu na upate pesa. What if kama unaweza pata pesa kwa njia nyingine tofauti na huwa udaktari utaacha kufanya?.
Dhana ya "Jamii itanichukuliaje" imeua mioyo ya mabilionea wengi sana mtaani
Watu wanakariri sana. Mtu unashindwa kuwa versatile. Zama zimebadilika. Kuwa na degree ya udaktari haimanishi lazima utibu watu. Mbona watu tuna leseni za udereva na hatujajiriwa kama madereva.
Mi naambiaga watu soon hii fani inaanza kuwa kama fani ya Uwalimu(Elimu). Kazi ina shurba na lawama kibao lakini ndio hivyo mishahara ya ajabu sana.
Kitaa unaonekana daktari smart lakini moyoni una stress za madeni huku ukiangalia gharama ulizotumia kusomea huo udaktari miaka mitano na...
Mimi naona sababu kubwa kuwafanyia watu wa afya hasahasa MDs ni kutaka kujua walio na utayari wa kazi. Wengi wamekuwa wakipangiwa kazi chini ya TAMISEMI sehemu za mbali na wamekuwa hawaendi. Hii husababisha serikali kuingia kwenye database na kuajiri madaktari wengine tena
Ukiona mtu katumia...
😂😂😂umeua mwamba. Watu wanajua udaktari una pesa sana kumbe ni njaa tu. Mi mwenyewe niliamua kuachana na kazi ya udaktari(M.D) baada ya kuona pesa yote ya mwezi(take home 850,000/-)inaishia kulipia bills na kula tu ikifika mwisho wa mwaka huna hata akiba ya 1mil uliyosave.
Tatizo huku...
Hospital nyingi zinategemea mapato ya bima hasa bima ya NHIF. Kwa sasa bima wamekuwa hawalipi kwa wakati hivyo kupelekea hospitali kuchechemea. Ikumbukwe BIMA inasimama kama mtu kati kati ya mgonjwa na hospitali. Hivyo mtu anapopata huduma inatakiwa BIMA ilipe kwa wakati. Sasa unapochukua miezi...
Mkuu mi nakushauri kwa mkoa wa Kigoma kwa jinsi navyoujua biashara ya electronicsz na vifaa vya simu itakufaa. Pia ujitahidi uweke na vifaa vya SOLAR utapiga pesa.
Hapo Kigoma wanaouza electronics ni wachache kama watatu tu, WAZIRI ELECTRONICS, STAN ELECTRONICS na ZAHIR kule mjini. Kwahiyo...
Pambana sana mkuu. Kigoma kuna fursa sana japo watu wengi wanapadharau sana. Watumishi wengi au wageni wakijaga huko huwa hawataki kutoka mkoa huo. Vipi upo maeneo gani hapo Kigoma?
Hapo inatakiwa kuweka kifaa kinaitwa non-return valve. Kiwekwe kwenye mita ya maji au baada ya mita ya maji. Hiyo husaidia maji kwenda uelekeo mmoja
Sent from my MI 6X using JamiiForums mobile app
Kwenye biashara ni kufanya kitu unachokipenda na unachokielewa, lakini usifanye kwa sababu kuna mtu umeona anafanya. Utafeli mapema. Asante sana kwa somo zuri kiongozi
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.