UKUTA HAUNA CHAMA
Na Mbusule C.Shillu,
Katika nchi yoyote ile kunapoibuka vimelea vya Udikteta, kila mwananchi anawajibika kuukemea kwa nguvu na akili zake zote maana athari zitakazojitokeza kama matokeo ya Udikteta huo zitawakumba wote bila kujali dini, kabila, kanda wala mrengo wa Kisiasa...