Lo! nakumbuka nauli ya uda ilikuwa sh moja na magari binafsi yakaruhusiwa kutoza sh tano, wakati huo iliitwa dala (sijajua kama ililingana na dola). Makonda wa magari hayo ya binafsi wakawa wanatangaza hiyo bei ya sh tano, kuwa usiingie humu bila dala! Ili kuita abiria wakawa wanatangaza - Dala...