Recent content by Kwelea

  1. K

    Rais Magufuli asema Serikali haitolipa deni la Manispaa ya Temeke kwa CRDB, amwambia Mbunge watalibeba wenyewe

    Yupo sahihi . Km mradi ulikuwa wa manispaa, ilikuwaje hawakujiandaa na km mradi ulikuwa wa Serikali Kuu, value for money ilizingatiwa?
  2. K

    Balozi Kijazi alipaswa kustaafu 2017 lakini akaongezewa mkataba mara mbili kwa sababu hakuonekana wa kumrithi

    Uongozi bora ni ule unaoandaa viongozi bora wajao. Binadamu hatuna hati miliki ya uhai wetu hapa Duniani. Watanzania takribani milioni 60, hakukuwa wa kaliba yake! Kauli tata hii.
  3. K

    TEC: Mipasuko kwenye jamii Husababishwa na Watu fulani kujiona bora zaidi na wako juu ya Katiba na sheria

    Siasa na imani vyote huilenga jamii husika, huwezi kuvitenganisha . Ustawi wa jamii hutegemea siasa safi na uongozi bora ukichagizwa na imani thabiti katika kumcha Mwenyezi Mungu. Siasa hujenga mwili na Imani hujenga roho ya mwanadamu katika maisha yake hapa Duniani.
  4. K

    Serikali inavyowakomoa walimu

    Km utakuwa umenielewa vizuri, maadili ni kipengele kidogo kati ya factors nilizoainisha. Si suala la kulamba miguu ya bosi wake ili apate haki yake, la hasha. Matatizo ya walimu yapo tangu nchi ipate uhuru na yanaendelea kuongezeka kila uchao. Kimsingi kada hii naweza kusema ndiyo kada dhaifu...
  5. K

    Serikali inavyowakomoa walimu

    Upo sahihi . Mimi ni mdau wa elimu na mzoefu wa masuala ya elimu kuanzia ufundishaji darasani, utawala wa elimu na masuala ya upandaji wa madaraja kwa walimu. Ningeweza kuandika mengi tu kwa faida ya wanajamvi lakini nahofia nitawachosha. Kwa kifupi sana km aliyoandika Bwana Malisa ni ya kweli...
  6. K

    Rais John Magufuli amteua Profesa Shukrani Manya kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Madini, baada Francis Ndulane kushindwa kuapa

    Km anamwamini Mwenyezi Mungu, wala asihofu , hayo hayakutokea kwa bahati mbaya. Kila limtokealo mwanadamu hupangwa na hutokea kwa wakati wake. Huenda ameepushwa na jambo kubwa ambalo ni afadhali ya alivyoshindwa kuapa. Hajapoteza ubunge wake, wala hakutarajia kuwa atateuliwa uwaziri, amshukuru...
  7. K

    Chonde Chonde CHADEMA, pelekeni wabunge bungeni. CCM wanajuta hata kuwapa hizo idadi ya kura iliyowafanya mpate nafasi 19

    Hapana. Lengo letu la kufuta upinzani limefanikiwa kwa 97% . Ni bora sana wapinzani wakakaa pembeni, wasitukwamishe. Kwanza walikuwa wasimbufu Bunge lililopita. Kwani wana umuhimu gani wa uwepo wao kwa wakati huu bungeni kiasi makelele yawe mengi hivi?. Mtuache na Bunge letu, wapinzani hanna...
  8. K

    GE2020 Viongozi wa CHADEMA hatua mlizochukua zitawatia aibu kubwa

    Mkuu, ni vyema ukajitafakari halafu uamue aidha ukae kimya au uuseme ukweli wa moyo wako. Hii Dunia tunapita tu. Huenda unatetea maslahi ya tumbo lako, si vibaya Ila ukumbuke wengine wameachana na tumbo, wanatetea roho zao.
  9. K

    GE2020 John Mnyika: CHADEMA haijakaa na Tume ya Uchaguzi(NEC) na haina mpango wa kuteua wabunge Viti Maalum

    Mbona kelele km zote mkuu. Kwani tatizo ni nini hapo. Uchaguzi umeisha, washindi wametangazwa. NEC wamefanya kazi yao vizuri kabisa na kupongezwa. Bunge la kijani ndilo lilikuwa takwa la msingi na limetimia. Sasa NEC kutuhumiwa kughushi , tena kwa niaba ya waliokataliwa na wananchi inakuwaje...
  10. K

    GE2020 REDET: Uchaguzi ulikuwa Huru na wa Haki

    Sijui kushuhudia uongo kwa mambo ambayo yalikuwa wazi kiasi cha kutia aibu ya kitaifa yanalenga nini katika mustakbali wa taifa hili. Morali ya wananchi kupiga kura itaendelea kushuka sana sana km kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu zitaendelna kupakwa rangi na kuonekana ni za...
  11. K

    Sheria zinasemaje kuhusu Polisi kuvamia ubalozi na kukamata mtu bila ruhusa ya balozi husika?

    Upo sahihi . JF ni darasa tosha kwa wale walio makini. Tatizo ni pale ufahamu wa mtu katika jambo husika unapopambanishwa na ushabiki wa kiitikadi. Hapo lazima kiswahili kigeuke kichina.
  12. K

    Sheria zinasemaje kuhusu Polisi kuvamia ubalozi na kukamata mtu bila ruhusa ya balozi husika?

    Kwa ufahamu wako wa maswali na majibu upo sahihi. Labda tu kwa kukusaidia hizo nyaraka za uongo ulishazithbiitisha?
  13. K

    Sheria zinasemaje kuhusu Polisi kuvamia ubalozi na kukamata mtu bila ruhusa ya balozi husika?

    Exactly. Polisi kuingia ubalozini kwa lengo la kumkamata mtu ni sawa na kuivamia nchi husika. Wamekosea na ndiyo maana wamemwachia bila masharti yoyote ndani ya muda mfupi sana.
  14. K

    UK statement following the Presidential Elections in Tanzania

    Hawatakosa, ni watu muhimu sana hao. Jiandae kushangaa zaidi kwa dua na maombi yatakayotolewa siku hiyo.
Back
Top Bottom