Kwa ratio hiyo sioni tatizo hapo. Kumbuka kanda ya ziwa ndio kanda yenye mikoa mingi na watu wengi kwahivyo ata namba ya wahitimu lazima iwe kubwa kulinganisha na kanda zingine.
Sikatai ukanda ulikuwepo kwenye nafasi za uteuzi lakini kwenye ajira za utumishi wa umma hapakuwepo upendeleo wowote, watu waliajiriwa kwa usawa. Kwa hiyo hoja yako ya ukanda unataka kutuaminisha kwamba ajira zilizopita waliajiriwa wasukuma au watu wa kanda ya ziwa tu?
Usahihi wake uko wapi kwa sababu ukichunguza vizuri hoja aliotoa utagundua ana jambo lake analotaka lifanikiwe. Kwa kuthibitisha hilo leo bungeni amekataa wazi wazi walimu wa kike kupewa kipaumbele cha ajira. Maana yake nini kama sio kuwa ana majina yake mfukoni anayotaka yapewe kipaumbele?
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amepotosha umma mchana kweupe kudai ajira za ualimu zilizopita zilitolewa kwa misingi ya kikanda na ukabila kwa sababu ukiachilia mbali jina moja lililojirudia kila ukurasa, mchakato wa ajira zilizopita ulifanyika kwa haki...
Elimu yetu inahitaji mageuzi makubwa sana ili kuzalisha wataalam watakao tumia usomi wao kuendeleza miradi mikubwa ya nchi na kutumia raslimali zetu wenyewe badala ya kuzitapanya kwenda nje ya nchi. lakini yote haya yatabaki kuwa ndoto kama tutaendelea kukumbatia elimu na ualimu wa cheti ambao...
Haya yalisababishwa na mwendazake lakini kikwete hadi anatoka madarakani aliacha akiwa ameweka mfumo mzuri wa kuajiri walimu wote bila ubaguzi wa kielimu au upendeleo
Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji. Nyie endeleeni kupiga mayowe mama anapiga kazi na watanzania bila kujari itikadi za vyama vyetu tunamuunga mkono kwa 100%
Hadi tuone matokeo maana ufafanuzi wako unatuacha njia panda. Kwa nijuavyo mimi 6% ya VRF inajitegemea, 1% ya administration fee inajitegemea na 15% inayokatwa kama marejesho ya deni nayo inajitegemea kivyake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.