Mtoa mada yaonyesha umetumwa na NMB na wamekununua kwa bei rahisi sana. Mafanikio ambayo Dr Kimei ameyafanya kwenye nchi hii ni makubwa sana na ameonyesha uzalendo na mapenzi kwa nchi yake. Hivi karibuni Benki ya CRDB imepewa tuzo ya kuwa Benki namba moja Tanzania na Kusini mwa jangwa la sahara...
Usidhani wote waliishia darasa la saba kama ww. Nenda kasome ripoti ya kina Mwakyembe kuhusiana na Richmond utajua Richmond ni nani . Usiwe mvivu wa kusoma.
Taifa hili Lissu hawezi kuliongoza kama vile ambavyo EL hawezi kuliongoza na katu hatokuwa kiongozi wa taifa hili. Kwenye familia zao sawa , ila sio Taifa hili.
Uko nchi ipi kijana ? sukari kilo ni Tshs 2,200 jana nimenunua dukani. Na hata nenda supermarkets mbali mbali haizidi bei ya Tshs 2,200/=. Au wataka sukari ipi upewe ?
Watu kueleza hisia zao sio vibaya. Ni jambo lililo wazi kuwa Israel imekalia kimabavu ardhi ya Palestina. Hili halina ubishi na ni dhuluma ya wazi wazi dhidi ya taifa la Palestina. Kama kuna kikundi kimeamua kulisemea hili hakuna ubaya wowote ili mradi hawajavunja sheria za nchi.
Ben yanaposemwa ambayo huyapendi tulia na uyasikilize. Usiwe kila kinacho kuudhi basi kipuuzwe. Kwani Joyce sio mke wa kiongozi wa CDM ?. Penye ukweli kubali tu .
Mkuu kwenye masuala ya fedha hakuna fedha ndogo. Leo hii mhasibu akiiba hiyo Tshs 31.2m kwenye halmashauri si mtampeleka kortini kujibu mashitaka ya wizi, mbona hamsemi ni fedha kidogo tu ameiba akaachiwa ?. Hiyo hela yaweza kutengeneza madawati mangapi? hakuna fedha ndogo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.