Habari !
Ni kweli kuwa inawezekana ikatokea mmoja wa mwenza katika ndoa au mahusiano kuwa na maambukizi (seropositive) na mwingine akawa negative. Kitaalamu hii inaitwa discordant couples.
Na habari njema ni kuwa kuna mamia kama sio maelfu ya discordant couples kwenye mahusiano hata ndoa...
Habari za jioni,
Band cells ni chembechembe changa za seli nyeupe za damu ''white blood cells i.e Neutrophils''. Kazi kuu ya seli nyeupe ya damu ni kupambana na magonjwa. Kwahiyo hizo band cells zikionekana kwa wingi inaweza kuwa dalili ya mwili unapambana na ugonjwa japo sio mara zote. Ni...
Bado inasoma juu sana. Hata kama unajisikia vizuri bado upo kwenye hatari. Naona tatizo hapo ni aina ya dawa. Rudi kwa daktari na kama unaweza muone daktari bingwa.
Habari yako ndugu, pole kwa ugonjwa na hongera kwa kugundua tatizo na kuanza matibabu. Ugonjwa wa shinikizo la damu ni ''silent killer'' na huweza kuchukua muda mrefu kabla ya kuanza kuonyesha dalili ila kipindi chote uharibu viungo vya mwili taratibu. Kitakwimu ni asilimia 40 ya wagonjwa wa...
Moderator YinYang naomba kubadili kichwa cha habari kiwe kwa herufi ndogo. Kisomeke Chanjo, Teknolojia ya Kiafrika na Simulizi ya Onesimus, mtumwa wa kiafrika aliyeiokoa dunia
Shukran
Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1700, mji wa Boston, Massachusetts kama ilivyokuwa kwa dunia nzima kipindi hiko, ulikumbwa na ugonjwa mbaya wa Ndui uliosababisha vifo vya watu wengi. Inakadiliwa watu zaidi ya milioni 300 walifariki kwa ugonjwa wa Ndui duniani kote.
Ugonjwa wa Ndui kipindi hiko...
Habari yako Ndugu,
Pole sana na tatizo linalo kusumbua. Kutokana na maelezo yako ni kwamba unasumbuliwa na kutokwa kwa damu kutoka sehemu ya chini ya njia ya chakula kwa kitaalamu Lower Gastrointestinal Bleeding (LGIB)
Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha tatizo hili, nitaeleza kwa...
Huo ni ugonjwa wa ngozi unaitwa "Keloids". Kwa kifupi ngozi yako inashida katika kutengeneza kovu pale inapoumia. Kuna uwezekano mkubwa umerithi ugonjwa huu.
Kwanza epuka na kuumiza ngozi yako "minor injuries" mfano unapochana nywele au unaponyoa. Ugonjwa wako ulipofikia inabidi upate dawa ya...
Jibu la haraka ni huwezi kujifungua kwa njia ya kawaida kwa sababu :
Unapojifungua kwa njia ya upasuaji inabidi ukae angalau miaka 2 ili kidonda kipone ndio unakuwa na uwezo wa kubeba mimba na kujifungua kwa njia ya kawaida.
kidonda cha upasuaji chenye umri chini ya miaka miwili tunakiita...
Asante kwa mchango wake. Ila kwa hiyo kesi ya nasal polyps haiwezi ikawekwa kwenye kundi la hypehidrosis kwa sababu, sababu ya mwili kutengeneza jasho iko wazi kabisa... Kwamba mgonjwa anatumia nguvu nyingi kuvuta pumzi kuliko kawaida ni sawa sawa kabisa na unapofanya mazoezi ya viungo..
Pia...
Hyperhidrosis ni ugonjwa wa kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida. Kutokwa na jasho ni hali ya kawaida kwa binadamu na wanyama na kazi kubwa ya jasho ni kupoza mwili unapopata joto kubwa. Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutengeneza wastani wa lita moja ya jasho kila siku.
Kiwango cha jasho...
Hii sio tetesi ni habari ya uhakika. Jana katibu wa wizara ya afya kaongea Na wafanyakazi wa hospitali ya bugando na kawapasha hiyo habari ! Pia mfanyakazi akienda masomoni sasa anatakiwa kuchukua likizo bila malipo Yani mshahara utakoma mpaka utakapomaliza masomo
Source: Mimi mwenyewe
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.