Recent content by Danisamweswa

  1. D

    RC Makonda aandika barua kuomba radhi kuwakejeli wabunge

    Ni kitendo cha kiungwana na kibinadamu kuomba radhi kwani binadamu siyo malaika wasikosee. Kutambua kosa ni jambo moja na muhimu kwa mwanadamu yeyote na kuomba radhi ni tabia ya kiungwana na ya kibinadamu kwa kweli. Nampongeza Mh. Makonda kwa hatua hiyo kama ni kweli. Mwanadamu hukosea na...
  2. D

    Maalim Seif avuliwa Ukatibu Mkuu CUF, Magdalena Sakaya apewa Ukatibu Mkuu

    Li Nina mashaka makubwa na uwezo wa Prof katika masuala ya siasa. Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF ni matatizo matupu tangu awe mwenyekiti amedumaza chama tu kwa kuwa siyo kiongozi kwani hana maono na wala hana na ya kupeleka chama cha CUF kwenye hatua yoyote ya ukuaji wa kisiasa. Wana CUF...
  3. D

    Rais Magufuli aamuru Ney wa Mitego aachiwe huru na wimbo wake upigwe vituo vyote redio na TV

    Rais kanipa raha sana kwa kuamuru mwanamuzi Nay aachiwe huru. Natamani kweli kufanya kazi na Mh JPM. Ananipa raha sana kwa maamuzi yake.
  4. D

    Ndalichako hawafahamu "MASKINI:

    Huo ndio ukweli. Watanzannia hawapendi kuambiwa ukweli haswa pale maslahi yao yanapoguswa. Mfumo wa elimu ya Tanzania ulikuwa mbovu kabisa. Sasa Prof. Ndalichako anaturudisha kwenye mstari tunalalamika. Mimi binafsi sitaki mwanangu asome katika mfumo huu wa kuunga unga. Watu wafuate...
  5. D

    Ndalichako hawafahamu "MASKINI:

    wenye elimu ya kuunga unga siyo maskini acha kusingizia maskini.
  6. D

    Ndalichako hawafahamu "MASKINI:

    Ama kweli watu wanapenda sana kulinda maslahi yao binafsi badala ya kuangalia maslahi mapana ya Taifa. Ukweli ni kuwa alichosema Ndalichako ni cha msingi kwa mustakabali wa elimu ya Tanzania. Tatizo wako watu wengi sana wenye elimu ya kuunga unga sasa wanaona Profesa Ndalichako anaweka wazi siri...
  7. D

    Jeshi la Polisi laondoa zuio la mikutano ya ndani ya vyama vya siasa

    i Ni vizuri kufanya hivyo kwa kuwa uzuiaji wa mikutano ya vyama vya siasa kimsingi ni ukiukaji wa haki za kisiasa kwa wananchi. Bado kuna sababu ya kuondoa zuio la kufanya mikutano na maandamano kwani hizo ni haki za kikatiba za raia wa nchi hii nzuri ya Tanzania nchi ambayo katiba ni sheria...
  8. D

    Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

    Wachumi wapo walichokisema kimesikiwa. Kati ya vitu ambavyo siasa haina nafasi ni Uchumi. Uchumi pamoja na kwamba ni takwimu hata mtu ambaye hajenda shule anaweza kujua kuwa hali ni nzuri au ni mbaya. Ninachoweza kusema ni kuwa kiasi cha mzunguko wa fedha ni kidogo mno kiasi kwamba baadhi ya...
  9. D

    NSSF waja na hoja tatu kuhusu fao la kujitoa

    Hivi na waliotumbuliwa watapata kazi nyingine wapi? Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
  10. D

    KILIO CHA AJIRA: Ukimya wa Rais Magufuli waleta hofu

    Kila sababu inaweza ikawa ni jibu sahihi ila tatizo hakuna maelezo yaliyotolewa zaidi ya kuwa uwepo wa wafanyakazi hewa ndiyo sababu. Ila ni kweli kuwa muda uliowekwa umeisha na hakuna tamko lingine. Katika mazingira kama hayo ni kusubiri tu na kuona jinsi serikali yetu inavyojipanga...
  11. D

    Amani ni tunda la Haki, tutimize wajibu isituponyoke

    Ninashindwa mara nyingi kujua watu wanapozungumza amani amani amani. Ninajua hakika kuwa amani ni tundu muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote. Jambo ninalozoea kusikia kwa wanasiasa ni kuwa tutailinda amani yetu kwa gharama yoyote. Jambo ambalo sijasikia ni kuwa Amani inalindwaje? Nimesikia...
  12. D

    Vyama vya upinzani Tanzania vijisahihishe kwanza vyenyewe

    Na hilo ni swali ambalo halitakiwi kujibiwa. Ila huyo Dr. Slaa alishindwa kirahisi na Kikwete kwa hiyo wanamlilia kwa kuwa wanajuwa ni mtu wa kushindwa kirahisi tu.
  13. D

    Kutoka Dodoma: Fred Mpendazoe atangaza rasmi kurudi CCM

    Ni vizuri kwa hao makada wa CCM kurudi nyumbani. Ila mimi binafsi siwafagilii hata kidogo watu wa namna hii wa kuhama hama vyama. Tabia ya namna hii haifai kwa watu wenye busara za kweli. Kimsingi kama waliweza kutelekeza chama wakati kikiwa vitani wanarudi wakati wa amani hawa ni njaa tu...
  14. D

    Kikwete alikuwa sahihi kumkata Lowassa

    Vichwa vidogo hujadili watu. Vichwa vyenye substance hujadili issues.
  15. D

    Waziri Mkuu: Tutakuwa tunatumia Kiswahili kwenye mikutano ya kimataifa, tutaajiri wa kututafsiria

    Hapo sasa. Wawepo wakalimani wa lugha zote hizo ili akisafiri kiongozi basi aende na mkalimani wa lugha ya wenyeji anakokwenda. siyo aende na mkalimani wa kiingereza alafu tena awepo mkalimani wa kutoka kingereza kwenda lugha ya wenyeji. Hivi hili litapunguza gharama kwenye msafara wa viongozi...
Back
Top Bottom