Kazi yoyote halali nafanya, kazi za kutumia nguvu kiasi na za kutumia akili kiasi. Chamsingi zisiwe technical sana, zisiwe zile zinazohitaji ujuzi mwingi sana mpaka kusomea.
Habari za jioni wadau? Nina mengi ya kushare nanyi kuhusu safari yangu ya kutafuta maisha ndani ya mkoa wa Kagera niliyoianza mwezi wa nane mwaka huu 2022. Ila kwa ufupi naomba niseme tu kuwa safari yangu hii hatimae imenifikisha katika mji wa Ngara.
Hivyo basi, kwa wanajamiiforums mlioko huku...
Baada ya kuzunguka huku na kule ndani ya mkoa wa Kagera, hatimaye nimefika Ngara wadau. Hali ya hewa ya hapa ndiyo balaa. Jua linawaka kidogo sana, mvua inanyesha muda mrefu sana na baridi ni kali kwelikweli. Wadau mlioko huku nipeni ramani za ujenzi wa taifa ili nami niuanze mwaka 2023 vizuri.
Asante sana kwa ushauri wako mkuu. Hakika ntaufanyia kazi. Kama utaweza kunipa connection kwa namna fulani itapendeza pia. Namshukuru Mungu mpaka sasa naendelea vizuri japokuwa ugumu wa upambanaji bado upo sana tu kwani bado nafanya vibarua vya kuungaunga ila angalau nimekuwa na uhakika wa kula.
Salama tena wakuu!
Bado napambana hapa Bukoba mjini. Kwa siku mbili sasa nilikuwa nimepata kibarua cha kumsaidia mzee mmoja alikuwa anajenga banda la mabati maeneo zilipo ofisi za TANROAD na BUWASA. Malipo yalikuwa sh 5000 kwa siku. Namshukuru Mungu kwa 5000 hiyo kwani inatosha kabisa kwa...
Ni siku nyingine tena leo namshukuru Mungu nimeamka salama japo mfukoni sina chochote. Ningependa kuyafanyia kazi maoni ya wadau hapo juu ya kwenda Karagwe au Mtukula lakini kwa sasa sina hata nauli ya kunifikisha huko. Kwa wanabukoba naombeni tena mnipe kazi angalau niweze kupata nauli ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.