SoC01 Ondoa hofu, anza sasa kuthubutu

Stories of Change - 2021 Competition

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,462
JE, UNASITA KUFANYA KITU TOKANA NA WASIWASI NDANI YAKO?

Hofu/mashaka/ wasiwasi unatufanya tusiendelee mbele na unatudumaza tunabaki vilevile tungali masikini na unaleta umaskini ndani yetu na kubaki vilevile tu bila hata kudhubutu kutenda jambo kuu katika Maisha yetu. Tufanye nini sasa iili kuiondoa hiyo hofu/wasiwasi juu yetu?

HOFU NI NINI AU IMETOKANA NA NINI?

Hofu ni hali ya kuwa na woga/ kutokuridhika/ mashaka/utisho unaotokana na kushindwa kwa kitu au ulipatwa na kitu chenye utisho ukakuletea hofu.

Hebu tuangalie maana halisi ya wasiwasi/ hofu.

WASIWASI MAANA YAKE:
Wasiwasi unaweza kuelezewa kuwa ni mwitiko wa mwili wako wa vitu hatarishi kwa maisha yako vinavyokuja au unavyofikiria vinaweza kuja. Wasiwasi unahusiana sana na hofu ambayo ni mwitiko wa mwili wako kwa hatari halisi (hatari iliyo mbele yako) au inayofahamika kuja siku za karibuni. Hofu na wasiwasi ni miitiko iliyojengeka kwa binadamu na wanyama , na njia za kupambana navyo zinahusiana na kushindana navyo .

KWANIINI WASIWASI / HOFU INAKUPATA/UNAKUPATA?
Wakati mwingine unaweza usijijue kuwa una hofu ndani ya moyo wako mpaka inatokea kile ulichopanga kufanya unashindwa kukifanya kwa wakati huo. Je umeshajiuliza nini kinatokea? wasiwasi namashaka ni dhana mbaya sana inayokwamisha usifike lengo la yale uliyopanga kuyafanya. wasiwasi ni mlango wa ukwamishaji wa maendeleo yako/ yetu na hata ya taifa kiujumla.
Ni pazia ambalo limefunga mwelekeo mzima wa kujikwamua usitoke/ tusitoke katika hali tulizonazo . Je tufanyaje tuondoe hali ya wasiwasi/mashaka/ hofu kwetu.

1630604277721.gif

HATUA 3 ZA KUONDOA HOFU/MASHAKA/ WASIWASI NDANI YETU

1. KUWA JASIRI NA IMARA

a) Jiamini kuwa unaweza na kuwa imara katika kila hatua uipitayo jiweke kuwa unaweza kufanya hii ndio sababu pekee itakayokuondoa katika hofu ya kutodhubutu kufanya kitu ulichojipangia kutenda,
b) Tatua jambo ambalo lilikufanya ukwame kwa wakati huo huku ukiwa na uimara wa kujisemea moyoni unaweza kutenda kwa nguvu na uweza wa Mungu jambo hilo.

2. KUWA MSIKIVU
.Jijengee dhana ya kuwa msikivu kwa mambo muhimu yakupasayo kufanya/kutenda na sio kukuruka na kufanya bila hata kusikiliza kwa wengine walifanyaje wakapita hatua hiyo. Unapokuwa msikilivu unakufanya uweze kufanya mambo makuu.

Je kwenye jambo lililo mbele yako kitu gani kinahitajika? nini? Je hatua zipi ufanye ili uweze kuingia katika jambo hilo? Sikiliza na usiogope kuuliza maswali kabla ya kurukia jambo.

3. ANZA KUTEKELEZA KWA VITENDO

Watu wengi hudhani kuwa kesho ipo tu na wala hawajisumbui kwa siku ya kesho kwani huona inakuja tu, wengine hawana mwelekeo katika mstakabali wa maisha yao wao ni bora liende wakiamka na kulala ni hivyohivyo tu, hawana mawazo mpya ya nini wafanye kwa siku hiyo walionayo. Usiwe mmojawapo wa watu wa namna hiyo ambao hawana mwelekeo wa mstakabali wa Maisha yao Wewe anza kutekeleza lile jambo kwa vitendo kama ni kazi, biashara, masomo, kilimo au chochote kile kifanye kwa nguvu zako zote
ondoa dhana ya kushindwa kufanya kwani ndio hofu, mashaka hayo ambayo yanakufanya usitende kwa wakati.

1630604113301.png

ANZA KUTEKELEZA KILE ULICHOKUSUDIA KWA WAKATI
jambo lolote haliji hivihivi tu mpaka uwe umejituma, umejithatiti, umejiona kuwa waweza kulitenda hilo wazo lako, na waswalhili wanasema mambo mazuri hayaji hivihivi tu yaani wewe ukinge mikono kupokea bila hata kujishughulisha au kuchakalika upate.

Hebu jaribu kufanya kile ambacho umekiwaza kukifanya, Kama unataka kuwa na maisha mazuri yenye furaha ndani yake kwanini leo usithubutu kufanya kile ambacho unaweza fanya au tenda kwanini ushindwe kuthubutu kutenda ulichokusudia katika maisha yako, unasubiri nini? unangoja nini? unadhani kuwa muda unakusubiri wewe? kwanini usiamue kufanya maamuzi yenye busara na kufanya pale wakati muda ungalipo? Au unadhani muda unakusubiri La hasha muda ni mali inabidi kutekeleza Zaidi yale uliyokusudia

Tusidhani muda unatusubiri , kama hatutathubutu kufanya yale uliyojiwekea basi ujue uko hatarini kuporomoka na kuwa na stress nyingi pindi utakapokuwa mzee.
"Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" Wafilipi 4:13

File:African men at work 08.png - Wikimedia Commons

PICHA KWA HISANI YA MTANDAO​

HITIMISHO
Ondoa hofu na wasiwasi anza kufanya kile ambacho unapenda au tuanze kufanya kile ambacho tunataka kufanya kwa wakati hapo ndipo tutaweza kuvuka na kuwa jasiri, wenye kuthubutu kutenda kwa yeye atutiaye nguvu yaani Muumba Mungu wetu.

Rafiki yangu ndugu yangu na mwenzangu hapa jamiiforum kama utathubutu kuondoa hofu/ wasiwasi utatoka hapa ulipo

soma warumi 3:14. Nawatakia kila la kheri na mafanikio tele pale
utakapoamua na kuthubutu

Tafadhali rafiki yangu naomba nipigie kura hapo pembeni ya thread yangu na nipate kura kadri iwezavyo na vilevile usisite kuchangia hapa katika mada hii unapoisoma

WAPENDWA WANGU NAOMBA MSISAHAU KUNIPIGIA KURA ANDIKO LANGU HILI PLS
 
naomba msaada wako unafanyaje kuiotoa link hii na kuipeleka sehemu ingine nimeshindwa hapa msaada best

Copy the link
 
Wakati tukiendelea kuwapa KURA watu waweze kushinda....
Usisahau na wewe pia una nafasi ya kuwa mshindi, hata nje ya FURSA hii....

(Infinix, Oppo, Samsung, TECNO) Download & install, Ni rahisi sana kupitia link hii....

unaweza Kujipatia michongo, na Fursa nyingi tu...

HUWEKEZI CHOCHOTE
Hii sio ONLINE MARKETING
USIMTUMIE MTU YEYOTE HELA YAKO

Download app hiyo, jisajili kawaida (iko kwa kiswahili) ukikwama nipo hapa kusaidia hii fursa tuitumie Wote Jada vijana
asante sana umeshanipigia kura mkuu kwanza kabla ya hiyo? nipigie kura rafiiki
 
wadau zangu watu wa kale Watu8 , Mtambuzi , Lady doctor, Mentor The Boss , miss chagga , sosoliso , Arushaone , Madagascar , Masanja KakaKiiza waseinc Shangani , doysilanda Unforgetable , Calis10 MJG Come27 nahitaji kura zenu kwa wingi wadau

Kura ndio wanapiga wapi?

Halafu hili ni jukwaa jipya ama, na madhumuni yake ni yapi?
 
daddy angalia mwisho wa andiko langu kuna kasehemu unaweka tick
Bujibuji naomba mwonyeshe daddy hapop juu sehemu ya kupiga kura plsss

yes jukwaa ni jipya
 
Kuna ya kujifunza hapa hakika. Uoga umeendelea kuwa sehemu ya vizingiti katika kufikia matamanio yetu
 
Natumaini hamjambo

JE, UNASITA KUFANYA KITU TOKANA NA WASIWASI NDANI YAKO?

Hofu/mashaka/ wasiwasi unatufanya tusiendelee mbele na unatudumaza tunabaki vilevile tungali masikini na unaleta umaskini ndani yetu na kubaki vilevile tu bila hata kudhubutu kutenda jambo kuu katika Maisha yetu. Tufanye nini sasa iili kuiondoa hiyo hofu/wasiwasi juu yetu?

Hebu tuangalie maana halisi ya wasiwasi/ hofu.

WASIWASI MAANA YAKE:
Wasiwasi unaweza kuelezewa kuwa ni mwitiko wa mwili wako wa vitu hatarishi kwa maisha yako vinavyokuja au unavyofikiria vinaweza kuja. Wasiwasi unahusiana sana na hofu ambayo ni mwitiko wa mwili wako kwa hatari halisi (hatari iliyo mbele yako) au inayofahamika kuja siku za karibuni. Hofu na wasiwasi ni miitiko iliyojengeka kwa binadamu na wanyama , na njia za kupambana navyo zinahusiana na kushindana navyo .

KWANIINI WASIWASI / HOFU INAKUPATA/UNAKUPATA?
Wakati mwingine unaweza usijijue kuwa una hofu ndani ya moyo wako mpaka inatokea kile ulichopanga kufanya unashindwa kukifanya kwa wakati huo. Je umeshajiuliza nini kinatokea? wasiwasi namashaka ni dhana mbaya sana inayokwamisha usifike lengo la yale uliyopanga kuyafanya. wasiwasi ni mlango wa ukwamishaji wa maendeleo yako/ yetu na hata ya taifa kiujumla.
Ni pazia ambalo limefunga mwelekeo mzima wa kujikwamua usitoke/ tusitoke katika hali tulizonazo . Je tufanyaje tuondoe hali ya wasiwasi/mashaka/ hofu kwetu.

HATUA 3 ZA KUONDOA HOFU/MASHAKA/ WASIWASI NDANI YETU

1. KUWA JASIRI NA IMARA

a) Jiamini kuwa unaweza na kuwa imara katika kila hatua uipitayo jiweke kuwa unaweza kufanya hii ndio sababu pekee itakayokuondoa katika hofu ya kutodhubutu kufanya kitu ulichojipangia kutenda,
b) Tatua jambo ambalo lilikufanya ukwame kwa wakati huo huku ukiwa na uimara wa kujisemea moyoni unaweza kutenda kwa nguvu na uweza wa Mungu jambo hilo.

2. KUWA MSIKIVU
.Jijengee dhana ya kuwa msikivu kwa mambo muhimu yakupasayo kufanya/kutenda na sio kukuruka na kufanya bila hata kusikiliza kwa wengine walifanyaje wakapita hatua hiyo. Unapokuwa msikilivu unakufanya uweze kufanya mambo makuu.

Je kwenye jambo lililo mbele yako kitu gani kinahitajika? nini? Je hatua zipi ufanye ili uweze kuingia katika jambo hilo? Sikiliza na usiogope kuuliza maswali kabla ya kurukia jambo.

3. ANZA KUTEKELEZA KWA VITENDO

Watu wengi hudhani kuwa kesho ipo tu na wala hawajisumbui kwa siku ya kesho kwani huona inakuja tu, wengine hawana mwelekeo katika mstakabali wa maisha yao wao ni bora liende wakiamka na kulala ni hivyohivyo tu, hawana mawazo mpya ya nini wafanye kwa siku hiyo walionayo. Usiwe mmojawapo wa watu wa namna hiyo ambao hawana mwelekeo wa mstakabali wa Maisha yao Wewe anza kutekeleza lile jambo kwa vitendo kama ni kazi, biashara, masomo, kilimo au chochote kile kifanye kwa nguvu zako zote
ondoa dhana ya kushindwa kufanya kwani ndio hofu, mashaka hayo ambayo yanakufanya usitende kwa wakati.

ANZA KUTEKELEZA KILE ULICHOKUSUDIA KWA WAKATI
jambo lolote haliji hivihivi tu mpaka uwe umejituma, umejithatiti, umejiona kuwa waweza kulitenda hilo wazo lako, na waswalhili wanasema mambo mazuri hayaji hivihivi tu yaani wewe ukinge mikono kupokea bila hata kujishughulisha au kuchakalika upate.

Hebu jaribu kufanya kile ambacho umekiwaza kukifanya, Kama unataka kuwa na maisha mazuri yenye furaha ndani yake kwanini leo usithubutu kufanya kile ambacho unaweza fanya au tenda kwanini ushindwe kuthubutu kutenda ulichokusudia katika maisha yako, unasubiri nini? unangoja nini? unadhani kuwa muda unakusubiri wewe? kwanini usiamue kufanya maamuzi yenye busara na kufanya pale wakati muda ungalipo? Au unadhani muda unakusubiri La hasha muda ni mali inabidi kutekeleza Zaidi yale uliyokusudia

Tusidhani muda unatusubiri , kama hatutathubutu kufanya yale uliyojiwekea basi ujue uko hatarini kuporomoka na kuwa na stress nyingi pindi utakapokuwa mzee.
"Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" Wafilipi 4:13

File:African men at work 08.png - Wikimedia Commons

PICHA KWA HISANI YA MTANDAO​

Neno:
Ondoa hofu na wasiwasi anza kufanya kile ambacho unapenda au tuanze kufanya kile ambacho tunataka kufanya kwa wakati hapo ndipo tutaweza kuvuka na kuwa jasiri, wenye kuthubutu kutenda kwa yeye atutiaye nguvu yaani Muumba Mungu wetu.

Rafiki yangu ndugu yangu na mwenzangu hapa jamiiforum kama utathubutu kuondoa hofu/ wasiwasi utatoka hapa ulipo

soma warumi 3:14. Nawatakia kila la kheri na mafanikio tele pale
utakapoamua na kuthubutu

Tafadhali rafiki yangu naomba nipigie kura hapo pembeni ya thread yangu na nipate kura kadri iwezavyo na vilevile usisite kuchangia hapa katika mada hii unapoisoma

WAPENDWA WANGU NAOMBA MSISAHAU KUNIPIGIA KURA ANDIKO LANGU ILI PLS
Andiko ili au hili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom