Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Nawasalimu waungwana wa JF,
Imekuwa hulka yangu kuzuia upotoshaji na ubabaishaji kuwahusu watu ambao nawafahamu hata kama ni kwa kiasi. Mmojawapo ni Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hii leo si mara yangu ya kwanza 'kumtetea' Prof. Kabudi. Sioni soni wala sina tashwishwi 'kumtetea' Prof. Kabudi kwakuwa si mtu anayezungumzwa azungumziwavyo.
Nimewahi 'kumtetea' kuhusu Uwakili wake na ujumbe wake Bungeni: https://www.jamiiforums.com/threads...ungumza-bungeni.1242547/page-20#post-28374171. Sitakoma 'kumtetea' kwakuwa namuamini, namheshimu na najua uwezo wake katika kulitumikia Taifa hili. Nafahamu kujitoa kwake kwa maslahi ya Taifa zima.
Mfano, gawio lililopatikana kutoka Airtel Tanzania kutokana na matunda ya Timu ya Majadiliano ya Serikali iliyoongozwa naye litasaidia katika utekelezaji wa miradi ya kiserikali itakayowanufaisha watanzania wengi kwa ujumla wao. Prof. Kabudi anapaswa kuombewa, kupongezwa na kutiwa moyo wa kuendelea na msimamo, uzalendo na utendaji wake uliotukuka. Pamoja na kuwa Wizara moja, amekuwa akifanya kila aambiwalo kulifanya kwa maslahi mapana ya nchi hii kwa weledi mkubwa.
Profesa Kabudi sasa amekuwa gumzo kufuatia kauli yake ya juzi pale Ikulu kuwa 'Mheshimiwa Rais amemtoa jalalani'. Wapo wanaoita hata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jalala. Wapo wanaoizungumzia kauli hiyo kwa kejeli na hujuma za kisiasa bila hata ya kujua mantiki na maana halisi ya kauli yake. Profesa Kabudi anaponzwa na kuzungumza kwa 'parables'. Anapozungumza anaamini kuwa ataeleweka. Inakuwa tofauti. Anatumia 'akili kubwa' kufikisha ujumbe wake.
Prof. Kabudi amekuwa mtumishi wa Serikali wa kawaida katika muda wote wa maisha yake ya kikazi. Kuanzia kuwa Mhadhiri Mkufunzi (Tutorial Assistant) hadi Profesa Mshiriki wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amekuwa mtumishi wa kawaida.
Kadiri nimjuavyo, hakuwahi kushika wadhifa wowote mkubwa wa kisiasa au kiserikali. Amestaafu utumishi wa umma mwaka 2016. Kutolewa kuwa mtumishi wa kawaida hadi kuwa Mbunge na baadaye Waziri Kamili ni jambo la kustaajabisha. Ni jambo la kushukuru. Hujikuta akishukuru kila mara-kwa Mwenyezi Mungu na kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli.
Kwa utumiaji wake wa maandiko matakatifu katika kuzungumza kwake, maandiko ambayo huitaji 'akili kubwa' kuyaelewa, Prof. Kabudi hujikuta akiwaacha solemba wasikilizaji wake kwa kuongea mambo yanayohitaji 'akili kubwa' kuyaelewa. 'Jalala' ni sehemu duni. 'Jalala' ni sehemu ya chini. 'Jalala' la Prof. Kabudi ni alipokuwepo kabla ya sasa kuwa Mbunge na Waziri Kamili. Ametolewa sehemu duni hadi yenye unafuu mkubwa. Kwanini asishukuru na kusema hatamsahau Mhe. Rais?
Narudia tena, kulingana na usomi wake na umahiri wake wa matumizi ya maneno ya kimaandiko na Kiswahili, Prof. Kabudi huponzwa na uficho unaozunguka hoja zake. Labda ajitahidi kuzungumza kwa lugha nyepesi na ya moja kwa moja ili kutowaacha wasikilizaji wake solemba na kumtafsiri kadiri watakavyo.