KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Kazi ya kupambana na mabeberu si ndogo, inahitaji uthubutu wa hali ya juu kwa sababu ni watu wanaojua mbinu zako zote. Kitendo cha Rais magufuli kupambana na mabeberu, watu wenye nguvu kubwa ya kiuchumi ni kitendo cha kijasiri sana kinachohitaji kupongezwa na kuungwa mkono kwa Tanzania ya kesho.
Katika kipindi ambacho nchi zinazoendelea zikiwa na hofu ya kushindwa kupambana na hayo mabeberu, watanzania tumepata kiongozi ambaye anaitetea Tanzania kwelikweli dhidi yao. Mifano ipo mingi inayoonesha ni jinsi gani Magufuli amekuwa akiipigania Tanzania lakini mmojawapo ni udhibiti wa utoroshaji wa rasilimali zetu na upitiwaji upya wa mikataba hasa ya madini.
Yote anayofanya Rais Magufuli yanawastaajabisha mabeberu na sitoshangaa siku moja wakitengeneza sanamu za Rais Magufuli na kuziweka katikati ya majiji yao kama ishara ya kumkumbuka kiongozi huyo jasiri na mzalendo ambaye aliivusha nchi yake kwa uzalendo alionao.
Mtu ambaye kaweza kuirudisha nchi yake katika misingi , kaweza kudhibiti ufisadi na mtu wa maamuzi magumu na ya kizalendo ambaye kila leo anawaacha mabeberu kinywa wazi na kujiuliza anawezaje kufanya yote bila hofu yetu lazima wamkumbuke kwa kujenga sanamu yake.
Ujasiri wake Magufuli umeifanya Tanzania kuwa ni nchi ya mfano na yenye ukuaji mkubwa wa kiuchumi ila kwa hofu waliyonayo wanaanza kutoa taarifa za uongo juu ya ukuaji wa uchumi ambazo ni za kupika. Kwa kinywa chake Rais Magufuli kasema uchumi wetu unakua kwa 7% na si 4% ambazo wamezipika.
Wazungu wanaogopa kivuli cha Rais Magufuli na wanapata hofu Zaidi pale wanapoona kuna kila dalili Tanzania kukua kwa kasi kiuchumi tena bila hata masaada wao na hicho ndicho kitawafanya siku moja wajenge sanamu ya kumkumbuka nchini mwao wakimtafakari ni mtu wa namna gani.
Kuna kila dalili kuwa baada ya Mwalimu Nyerere kwa kizazi hiki, Rais Magufuli anaweza kuja kuwa kumbukumbu nzuri ya wazungu kwa misimamo mikali na uwezo wa kulinda rasilimali za Taifa kwa kiwango cha juu sana.