Lipumba aonja joto ya jiwe la ACT-Wazalendo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Wimbi la wanachama wa CUF wanaomuunga mkono aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, limemtisha mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba.

Kufuatia hali hiyo, Profesa Lipumba amewaangukia wanachama wa chama hicho kutoondoka, badala yake wabaki ili wajenge chama na kutibu majeraha yaliyotokana na mgogoro wa kiuongozi uliodumu kwa miaka mitatu.

“Msifuate Maalim Seif, bakini tuijenge CUF, tumetoka mbali hasa wanachama wa Pemba. Maalim Seif ni mharibifu na ameangukia ACT-Wazalendo ambayo ipo mahututi,” alitoa wito huo jana wakati akizungumza na wanahabari katika ofisi kuu ya makao makuu ya chama hicho Buguruni, Dar es Salaam.

Maalim Seif tayari ametimkia ACT-Wazalendo ambako amekabidhiwa kadi namba moja ya uanachama pamoja na wafuasi wake wakiwamo waliokuwa viongozi wa juu wa CUF upande wa Zanzibar.

Profesa Lipumba aliwataka wanachama wa CUF hasa Zanzibar kuacha kufuata mkumbo kwenda chama kingine akiisema Maalim Seif alikidhoofisha chama hicho na kusababisha mgogoro na ndio maana wamemfuta uanachama.

“Wananchi, wanachama wa CUF hasa Zanzibar hiki ni chama kimoja, endeleeni kukiunga mkono na tutibu majeraha.

Tumetoka mbali katika kudai haki nchi hii, CUF ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kudai haki ya kupata Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi na utawala bora,” alisema.

Profesa Lipumba alisema, “hiki ni chama cha watu siyo mtu mmoja, msikubali kushawishiwa na mtu yeyote kwenda chama kingine na kuacha uwekezaji mlioanzisha wa kudai haki sawa kwa wote. Wazanzibar mmejitahidi kwa kipindi kirefu kupigania haki zetu, Seif Sharif asitugombanishe.”

Mbali na hilo, Profesa Lipumba alisema licha ya kumfukuza uanachama Maalim Seif, mkutano mkuu uliomalizika Machi 15 uliazimia pia kuwafukuza viongozi wengine ambao ni Ismail Jussa, Salim Bimani, Issa Kheri, Mohammed Nuru na Said Ali Mbarouk wote kutoka Zanzibar pamoja na Joran Bashange, Mbarara Maharagande na Abdallah Katawi wa Tanzania Bara kwa madai ya kushabikia na kuongeza kesi za CUF.

Katibu mkuu mpya wa CUF, Suleiman Khalifa Suleiman alisema kubadilisha ofisi na kupeperusha bendera za ACT-Wazalendo katika majengo yaliyokuwa yakitumiwa na CUF ni kinyume cha utaratibu kwa kuwa ofisi hizo zilijengwa kwa nguvu ya wanachama na siyo mtu.

Khalifa ambaye pia ni mbunge wa zamani wa Gando - Pemba, alisema kinachofanywa na watu wanaodaiwa kumuunga mkono Maalim Seif si sahihi, lakini wao watatumia utaratibu wa kisheria kuzirejesha ofisi hizo.

“Hatutatumia nguvu katika suala hili, bali tutafuata utaratibu wa kisheria kwa sababu kinachofanyika ni uhuni. Seif anataka kuiba ofisi hizi, lakini hatafanikiwa,” alisema Khalifa.

Katika hatua nyingine, Hamidu Bobali, mbunge wa Mchinga jana alitangaza kurejea kumuunga mkono Profesa Lipumba. Awali, mbunge huyo alikuwa upande wa Maalim Seif. “Nawaomba mnisamehe kwa yaliyotokea nimerudi kukijenga chama chetu,” alisema Bobali.
 
Nadhani lipumba akiona hii bendera anapata degedege kwa kutwa mara tatu
Screenshot_20190320-075828.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa bana.. Hawa hawa wanaomfata Maalimu..baada ya muda utasikia wanarudi kwa Lipumba.
Kwani huyo Lipumba ana mnato?? Kwa nini mnavaa miwani ya mbao huku mnataka leseni ya udereva?? Hupewi ng'oo. Ndivyo ilivyo kwa Lipumba. Watu woote weshaona anavyo bebwa na huyo mwenye hiyo mbeleko ndiye hawamtaki.
Watu wapo tiyari kulichagua hata gogo kuliko mtu wa jinsi yake
 
Siasa zinabadilika badilika kama upepo,,

leo upepo wa kaskazini mara kesho upepo wa mashariki ya pwani ya visiwani,,

,mara upepo wa unaelekea magharibi ziwa tanganyika palipo ungua shoka mpini ukabaki,""ZZK full bright brain,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upinzani kumenoga sasa.. bora chadrama hakiongelewi tena.. ni vituko vya karne na drama zaidi tunasubiri.. muwe tayari kupata viti vichache Bungeni.

Haya wadau 2020 kama kawa tutamshangilia JPM kwa furaha tele atakapo pita kwa kura nyingi zaidi ya 2015.
 
Upinzani kumenoga sasa.. bora chadrama hakiongelewi tena.. ni vituko vya karne na drama zaidi tunasubiri.. muwe tayati kupata viti vichache Bungeni.

Haya wadau 2020 kama kawa tutamshangilia JPM kwa furaha tele atakapo pita kwa kura nyingi zaidi ya 2015.
Umeanza fujo mkuu!
 
Back
Top Bottom