Ujasiriamali 2: Usindikaji wa Mtindi (Sour Milk)

Food Scientist

Senior Member
Apr 29, 2017
102
183
Wakuu,
Kwanza mniwie radhi kwa kuchelewesha kuleta somo hili.
Kuna baadhi ya mambo yaliingiliana na hivyo kushindwa kuiandaa mada hii.

Nilikwisha leta mada ya Usindikaji wa Yoghurt kupitia uzi huu
Ujasiriamali: Usindikaji wa Yoghurt na Mtindi - JamiiForums

Nashukuru kuna watu waliweza fanya wenyewe na kuna baadhi tulionana na kuweza kufanya pamoja na wengi wanaendelea vizuri.

Leo nakuletea Jinsi ya kusindika Mtindi, moja ya zao la maziwa. Ikumbukwe kuna baadhi ya watu hudhani Yoghurt ndio mtindi.
Mtindi na Yoghurt ni tofauti kabisa kuanzia utengenezaji, ladha, texture(month feeling) na hata muonekano.

Utofauti ni kama ifuatavyo,
i. Yoghurt ni laini na nzito (viscosity yake ni kubwa) wakati Mtindi una vibongebonge na nyepesi (viscosity ni ndogo)

ii. Yoghurt ina Uchachu flani wakati Mtindi umepoa,

iii. Yoghurt inawezwa wekwa sukari na Ladha mbalimbali wakati Mtindi huwezi weka ladha wala sukari

iv. Starture culture wa Yoghurt ni Thermophiles (wanapenda joto) wakati wa Mtindi ni Mesophiles (room temperature)

Nimeambatanisha picha hapo chini ya yoghurt na Mtindi.

JINSI YA KUTENGENEZA MTINDI

Mtindi ni moja ya zao la maziwa ambalo hutengenezwa kwa kuchachisha maziwa. Maziwa haya huchahchishwa kwa kutumia Starture Culture (bacteria maalumu).

Hatua za kufuata
i. Hakikisha maziwa yako ni salama, hayajawekwa maji na wala kuchacha

ii. Chuja maziwa kwa kutumia Kitambaa chepesi cheupe

iii. Chemsha maziwa huku ukiwa unayakoroga mpaka kufikia nyuzi joto 85 Centigrade

iv. Pooza Maziwa Mpaka kufikia nyuzi joto kati ya 24-28

v. Baada ya kupoa katika joto hilo, weka starture Culture 1% ya ujazo wa maziwa (Kwa culture ya kiwandani unaweza weka 1g per 100L) koroga vizuri.

vi. Funika maziwa yako na uyaache kwa saa 18-20 katika joto la kawaida (room temperature)

vii. Baada ya kuganda, hifadhi mtindi kwenye freezer katika nyuzi joto 4-8 centigrade kwa saa 3

viii. Koroga Mtindi wako. Tayari kwa kunywa, waweza kupack kwenye vifungashio.

Note.
1. Unaweza kupack maziwa yako kwenye vifungashio baada ya kuweka culture ya kuyaacha yagande kwenye joto la room temperature kwa saaa 18-24 na baadae kuyahifadhi kwenye friji.

2. Maelezo mengi ya utangulizi na somo la maziwa kwa ujumla nimetoa kwenye mada ya yoghurt, hivyo wawepa pitia.

.
mtindi.jpg
yoghurt.jpg



Nakaribisha Maswali.
 
Mkuu kwa packaging ya namna hii kama Asas, unaweza kufanya biashara kwa mtaji wa milion ngapi the least?

Sent using Jamii Forums mobile app
Itabidi uwe na uzalishaji mkubwa wa maziwa ili cost zingine zijimalize...

Hiyo packing kutengenezewa itakuhitaji uchukue chupa kuanzia 25k....

Lkn waweza kupack kwenye chupa kama hv
IMG_20170914_120201.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom