Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Jeshi la Polisi limeonya wananchi kuhusu ukiukwaji wa sheria unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia ujumbe mfupi wa maandishi katika simu wakidai kutumiwa fedha, kuwasiliana na mganga fulani ama kushinda bahati nasibu.
Jeshi la Polisi kupitia taarifa yake iliyoitoa leo, Jumatano limewatahadharisha wananchi kupuuza ujumbe pamoja na simu wanazopigiwa kwani zina nia ovu ya kutaka kuwatapeli.
Katika taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limesema kwa yeyote atakayepata usumbufu wa ujumbe au kupigiwa simu hizo aripoti Polisi, na Kitengo cha Upelelezi na Makosa ya Mitandao kinaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua.
Hili swala limejadiliwa sana hapa. Zaidi soma=>Meseji (SMS) za dawa za Kiganga: Je, hawa ni matapeli? TCRA mko wapi? Namba wanatoa wapi?