Rais Magufuli akutana na mawaziri wa Elimu na TAMISEMI, apiga marufuku michango ya aina yoyote shuleni

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Rais Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu Dar es salaam Mhe.Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari.

Rais Magufuli: Tumesema elimu bure, elimu bure haiwezi kaja tena kwa mgongo mwingine ikawa elimu pesa. Tumeweka utaratibu kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari form four hakuna kulipa ada yoyote. Nimewapa maelekezo kwamba kuanzia leo iwe ni marufuku na wakalisimamie hili. Mzazi sitaki kusikia akilalamika mwanae amerudishwa shule kwa sababu ya michango.

Rais Magufuli: Na walimu wote wasishike mchango wowote toka kwa mwanafunzi, mchango kama kuna mwananchi anataka kuchangia apeleke kwa mkurugenzi, mkurugenzi kama anataka kutengeneza madawati atatengeneza na kupeleka kwenye shule inayohusika. Siyo mwanafunzi ameenda shuleni akarudishwa kwasababu hajatoa michango.

Rais Magufuli: Kwahiyo nimemweleza waziri na waziri mwenzake kwasababu ndio wanaoshughulikia elimu. Lakini kwa taarifa hii mkawaeleze wakuu wa mikoa, wakuu wa mikoa na wakurugenzi.

Rais Magufuli: Nikisikia kuna shule katika wilaya fulani ambayo mtoto anarudishwa kwasababu hajachangia michango huyo mkurugenzi hana kazi. Na hii waanze kutekeleza kuanzia leo. Maafisa elimu wote wakasimamie hili, wanalipwa kwa ajili ya kusimamia. Tunajua enrolment ya wanafunzi imeongezeka hizi ni challenge ambazo lazima tuzibebe sisi kama serikali lakini hii isiwe sasa ni demotivation nyingine ya kuwazuia watoto, sasa hivi watoto wameacha kwenda shule kutokana na michango hii inayotolewatolewa sasa waziri mkalisimamie hili.

Maagizo haya yanakuja ikiwa ni siku moja baada ya malalamiko ya mwanaJF kuhusu kutozwa sh 70,000 huko Butiama mkoani Mara, zaidi soma=> Mkanganyiko elimu bure: Huko Butiama wananchi walazimishwa kuchanga elfu 70, la sivyo unanyang'anywa kuku, sufuria, n.k.




magu.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuchukuliwa hatua dhidi ya viongozi na watendaji ambao shule za msingi na sekondari zilizopo katika maeneo yao zinawatoza wanafunzi michango mbalimbali kinyume na muongozo uliotolewa na Serikali wa utoaji wa elimu bila malipo.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo asubuhi tarehe 17 Januari, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Lazaro Ndalichako na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Said Jafo.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inatoa Shilingi Bilioni 23.875 kila mwezi kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa elimu bila malipo lakini inashangaza kuona bado kuna walimu wanaendelea kuwatoza michango ama kuwarudisha nyumbani wanafunzi ambao wanashindwa kutoa michango hiyo.

“Nawaagiza Mawaziri, sitaki kusikia mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa kushindwa kutoa michango, na fikisheni maagizo haya kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wote wanaohusika, nikisikia tena mahali jambo hili linaendelea hawa niliowateua mimi wataondoka.

“Haiwezekani tumefuta ada, halafu walimu wanaamua kuanzisha michango tena mikubwa ambayo watu masikini wanashindwa kusomesha watoto wao, na kama wazazi wanataka kuchangia kitu shuleni wapeleke michango yao kwa Mkurugenzi, lakini sitaki kusikia mwanafunzi anapewa sharti la kutoa mchango ndipo apokelewe shule” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya kupata taarifa kuwa zipo baadhi ya shule ambazo wanafunzi wanadaiwa michango mbalimbali tena kwa kiwango kikubwa ikiwemo chakula, maabara, madawati na ziara za kujifunza, hali iliyosababisha wazazi kushindwa kumudu.

Waziri Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ameagiza walimu na viongozi wa halmashauri kuwarudisha shule mara moja wanafunzi wote waliorudishwa nyumbani kwa kutotoa michango na pia kurejesha mara moja michango iliyokusanywa kinyume na mwongozo wa Serikali.

Waziri Mhe. Selemani Said Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwasilisha taarifa ya shule ambazo zimetoza michango kinyume na mwongozo wa Serikali ifikapo Ijumaa wiki hii (tarehe 19 Januari, 2018) ili hatua zichuliwe dhidi ya walimu na maafisa elimu ambao kwa makusudi wamekiuka mwongozo huo.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

17 Januari, 2018
 
Taarifa haijakamilika ila kwa maoni yangu binafsi Kuna kutokuelewana Kati ya rais Na watendaji wake. Rais anasema marufuku michango ya aina yoyote shuleni wakati huo watendaji Na wawakilishi wake wanachangisha michango kila Leo Na baadhi ya maDC wanahamasisha michango.

Na niliwahi kumsikia waziri wa tamisemi aliyepita bwana simbachawene anasema kilichoondolewa Ni ada Na Kama michango imekubaliwa na wazazi basi ichangwe na mzazi asiyechanga achukuliwe hatua.

naona Kuna watumishi wanataka kumchonganisha rais magufuli na wananchi wake au hawamwelewi rais au rais nae ndo walewale.

nilicheka siku moja rais kasema elimu bure waziri anasema sio elimu bure Ni elimu bila malipo sasa sijui tofauti Ni nini.
 
Ile habari iliyoletwa hapa jana JF huenda ndio chanzo.

Hata hivyo,marufuku hii inaweza kuwa ni ya kisiasa tu ili iripotiwe na vyombo vya habari na mkulu aonekane amechukua hatua lakini mambo yakawa ni yale yale tu.

CCM sio watu wa kuwaamini hata kidogo.
Ndio mjue Sizonje ana id yake humu anapitia kimya kimya pili ndio mjue kuwa jamiforums ndio mtandao wenye nguvu kwa Tz ukiacha mitandao ya wamarekani

Alafu anatokea jinga huko linasema samatta ana ushawishi

Jf idumu

Mexcence kama hawakuoni acha tu kazi yako ijitangaze yenyewe watakuja kushtuka asubuhi
 
s
Rais Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako Ikulu Dar es salaam Mhe.Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari.

Maagizo haya yanakuja baada ya malalamiko ya mwanaJF kuhusu kutozwa sh 70,000 huko Butiama mkoani Mara, zaidi soma=>
Mkanganyiko elimu bure: Huko Butiama wananchi walazimishwa kuchanga elfu 70, la sivyo unanyang'anywa kuku, sufuria, n.k.

View attachment 677768

Sasa wale waliotoa michango January wanawarudishia aMA kitu gani ?

waboreshe malipo ya waalimu ili watoto wapate elimu bora, maana hakutakuwa na maana yoyoye kuwapeleka wenetu shule bila ADA kisha wanatoka hapo hawajui lolote .....maana yake awape walimu malipo yao ili wawafunze watoto zetu inavyotakiwa.... kisha waalimu hao watakaofelisha wawajibishwe ikibidi waende jela!!!!

hivyo atakuwa kafanya la maana kinyume cha hapo hehehe hata shetani ataona aibu kwakweli
 
Jembekillo Moderator naomba mlinde heshima ya jukwaa hili. Dhihaka na Kejeli juu utu wa mtu haikubaliki kwa kiwango chochote.

Tutofautiane mawazo na hoja ndiyo sawa. Lakin hii ya kuzungumzia mwonekano na maumbile ya mtu kwa dhihaka kiasi hiki ni kitendo kinachouzi sana.
 
Back
Top Bottom