Kiza hutengeneza maumbo?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Ulishawahi kutembea kizani kwenye giza totoro? Ulishawahi kulala chumba chenye giza mwanzo mwisho? Ulishawahi kuona yale maumbo ya watu na viumbe vya ajabu?

Unatembea kwenye barabara yenye miti vichaka na majani unaona mbele yako au pembeni kuna vitu kama watu au wanyama tena vinatikisika au kutembea au kuongea kwa sauti ya chini

Au unahisi kabisa nyuma yako kuna mtu anakuja anakufuata unatamani ugeuke uangalie au utimue mbio nywele zinasimama kabisa moyo unaenda mbio mambo yanakuwa magumu kweli
Kuna story za vibwengo na vinyamkera vingi hujitokeza kwenye maeneo kama haya lakini si mara zote kila kitu ni hivyo viumbe

Waganga makanjanja wajanja sana hutumia giza na makaburini na sehemu zenye miti na misitu au vichaka kukupiga anakuandalia mazingira kabisa ya wewe kuwaona hao viumbe

Kinachofanyika na ubongo wako mwenyewe kupitia macho yako....unawaza kuhisi na kuhusu vitu vya ajabu kizani kisha unatengeneza picha zake automatically majani yakicheza tu kidogo ile sura na umbo ulivyoviumba akilini vitakujia live...hapa ndio ishu ya vinyamkera na vibwengo hujitokeza, akili yako ndio inakuchezea michezo kulingana na mawazo yako

Fanya jaribio hili usiku wa leo zima taa zote mpaka ile ya nje inayoingiza mwanga kupitia dirishani kisha anza kuwaza kuhusu vibwengo mashetani majini vinyamkera na mizimu nk ...wallah nakuambia utaviona live....

Makaburini kuna story nyingi sana za namna huyo lakini nyingi hazina ukweli na hata hao marehemu tunawasingizia tu
Maisha ni safari ndefu hujui ni lini na wapi unaweza kukutana na hili usibabaike wala kubabaishwa...matukio mengi ya namna hii ni own mind creations...
 
Kweli kabisaa , nilpo ona mwanzo wa uzi wako nikajua,hata wewe huogopa kwakiasihiki. kumbe uli jiuliza maswali alafu mwisho ukajijibu. Kwahapa mjini ningumu sana kuona vitu kama hivyo kwani kuna taa nakuna watu wengi, inakuwa sio rahisi mtu kuji tengenezea hiyo miji picha inayo tengenzwa na woga.

Ukiwa kwenye kijiji alafu sehemu iliyo tulia tulii. We wacha,kabisa unaweza kumuona, mtu mwenye pembe.
 
Benny..Tatizo umezaliwa huku mjini sana , hukuwai kuwa pekeyako kwenye kiza kinene??. Ukiwa kwenye giza kuna vitu una weza kuviona lakini vitu hivyo sio vitu halisi kabisa nipicha tu zinazo jijenga ndani yako kutokana na uwoga. Unaweza kufikiri una ona kitu kabisa lakini hakuna chochote, ila ni uwoga.
 
True Kaka Tunajitisha Wenyewe Kwa Kutengeneza Image Mbaya Kwny Fikra Zetu.
Hata baadhi ya ndoto mbaya na majinamizi hutokana na kulala kizani na kuwaza mambo ya kutisha
cfbb565ca8b105eddbc35f6601de4994.jpg
838d2be60ad9cdea59684992afa8dcfa.jpg
ndio maana mara nyingi watu wenye hofu na giza hushauriwa walale bila kuzima taa..kitu ambacho kwangu ni mwiko kabisa
2f852d1b71136aa5b98d472a0e7e4661.jpg
 
Hizo ndoto za majini na majinamizi sijawahi kuota. Tena nikiwa na ndovu kadhaa burdaani.

Hakuna vibwengo wala majini, ni kujitisha tu. Mara nyingi nalala peke yangu, kuna nyakati Mtu akinitembelea anashangaa "unalalaje peke yako hapa, huogopi?"
 
Ulishawahi kutembea kizani kwenye giza totoro? Ulishawahi kulala chumba chenye giza mwanzo mwisho? Ulishawahi kuona yale maumbo ya watu na viumbe vya ajabu?
Unatembea kwenye barabara yenye miti vichaka na majani unaona mbele yako au pembeni kuna vitu kama watu au wanyama tena vinatikisika au kutembea au kuongea kwa sauti ya chini
Au unahisi kabisa nyuma yako kuna mtu anakuja anakufuata unatamani ugeuke uangalie au utimue mbio nywele zinasimama kabisa moyo unaenda mbio mambo yanakuwa magumu kweli
Kuna story za vibwengo na vinyamkera vingi hujitokeza kwenye maeneo kama haya lakini si mara zote kila kitu ni hivyo viumbe
Waganga makanjanja wajanja sana hutumia giza na makaburini na sehemu zenye miti na misitu au vichaka kukupiga anakuandalia mazingira kabisa ya wewe kuwaona hao viumbe
Kinachofanyika na ubongo wako mwenyewe kupitia macho yako....unawaza kuhisi na kuhusu vitu vya ajabu kizani kisha unatengeneza picha zake automatically majani yakicheza tu kidogo ile sura na umbo ulivyoviumba akilini vitakujia live...hapa ndio ishu ya vinyamkera na vibwengo hujitokeza, akili yako ndio inakuchezea michezo kulingana na mawazo yako
Fanya jaribio hili usiku wa leo zima taa zote mpaka ile ya nje inayoingiza mwanga kupitia dirishani kisha anza kuwaza kuhusu vibwengo mashetani majini vinyamkera na mizimu nk ...wallah nakuambia utaviona live....
Makaburini kuna story nyingi sana za namna huyo lakini nyingi hazina ukweli na hata hao marehemu tunawasingizia tu
Maisha ni safari ndefu hujui ni lini na wapi unaweza kukutana na hili usibabaike wala kubabaishwa...matukio mengi ya namna hii ni own mind creations...
Mkuu Mshanajr unaweza kuongelea kuhusu majinamizi? Kuna wakati mtu ukiwa usingizini unahisi hali kama ya paralysis then kinachofuata unakua huwezi hata kujitingisha baada ya hapo unaona live unakabwa na dubwana ambalo huwezi kulitambua vizuri na unajiona unapiga makelele lakini hakuna anaesikia,hii inakuaje?
 
Acha kushiba sana usiku. Kula kiasi na acha uwoga. Hakuna jinamizi
 
Mkuu Mshanajr unaweza kuongelea kuhusu majinamizi? Kuna wakati mtu ukiwa usingizini unahisi hali kama ya paralysis then kinachofuata unakua huwezi hata kujitingisha baada ya hapo unaona live unakabwa na dubwana ambalo huwezi kulitambua vizuri na unajiona unapiga makelele lakini hakuna anaesikia,hii inakuaje?
Hyo hata mimi huwa inantokea sometymz hata kama ckuwa na mawazo ya kuogofya. Hilo naamini huwa ni kweli asee wala c mawazo.
 
Back
Top Bottom