Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Mkuu, saidia jina la balozi mtajwa katika kadhia hii
UN ilikuwa kimya, US ilikuwa kimya, AU ilikuwa kimya. US, UN, Belgium na France walichofanya ni kuhakikisha watu wao waliondolewa salama.

US secretary of state wakati huo Warren Christopher alikaririwa akisema tumefanikiwa kuwatoa Americans safe na hilo ndio jambo la msingi, wanaopigana ni kina nani, Rwandans vs Rwandans, ngoja wauane coz they are foolish.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka hiyo 94 kuna dogo walipanga mtaani jirani ikatokea tukawa friends, basi vile ye mgeni ikawa siku naenda nae viwanja Siku coco Beach Pale mara ghafla kapagawa kaanza kuongea kilugha naona kafuata bonge la jiwe amtupie Jamaa (muhutu)

Yaani mpk namnyanganya namuuliza vp ww unamdai au,mnajuana?ndio anajibu interahamwe hawa ataniua nikimuacha.
Mi nikaona we acha mambo yenu huko huko uko hapa no hate.

Ahahahahah, nimecheka sana. Sada hawa watu ugenini wanaishi hivo..huko kwao wanaishije?

Ebu mkuu tupe stori kamili kidogo...vaadae hujamuuliza kwa nn wanachukiana?
 
Wako hivi yaani ni kuliana timming tu,ndo mana sa hivi PK ni kuwarundika tu ndani anajua akicheza wanaanza nae
 
Inaendelea...................... 49k viewers si mchezo.

Haya sasa tusonge mbele tarehe, saa, sekunde za malaika mtoa roho zikawadia 6/04/1994. Saa tisa usiku tukaashuhudia kitu kama kimondo kikishuka ardhini ila kikapotelea vichakani kwa mbali nje ya mji. kutokana na kishindo chake pale ubalozini kila mtu aliamka lakini hakuna aliejua hasa ni nini, tukachukulia kawaida tukajua ni yale yale kila siku si tumeshaanza kuzoea watu wakaendelea kuchapa usingizi nawanaume wakaendelea kulinda getini.
Asubuhi mapema tukashudia hali ya ajabu ambayo sijawahi kuiona katika maisha yangu, yani kukatokea kitu kama wingu hivi yanii mtu akisimama mitaa tano au kumi kutoka ulipo huwezi mtambua vizuri hadi awe karibu sanaa. Wenye redio wakafungulia redio zao kusikiliza , ikumbukwe kuwa kipindi chote wapiga mayowe wa propaganda redioni walikuwa hawaongee ulikuwa unapigwa tu muziki wa chama ila alfajiri ikasikika wimbo wa taifa ndo unapigwa watu wakabaki wanashangaa halafu unakuwa unajirudia .dalili ya kitu kibaya ikaanza kuhisiwa kigali yote kimyaa.....

Tukawa sasa tunaingia tarehe yenyewe 7/04/1994 harufu ya damu ikawa inasikika kigali nzima, makelele ya maumivu ya watu yakawa yanasikika kwa mbali kutoka hapo ubalozini ,balozi ndo akawa ametoka kututangazia kuwa sasa hali si nzuri rais habyarimana ameuawa ile kusema tu vile watu wote akili zilituruka wengine wakawa kama wanataka kukimbia hovyo wanaume ikabidi wafanye kazi ya ziada kwani kitendo cha kutoka nje ya ubalozi kingeleta maafa makubwa sanaa. Ila wote pale picha iliyotujia kichwani ni kwamba sasa tunakufa hakuna tena msalie mtume.

Swali likaja nani kamuua rais? Hakuna mwenye jibu. Aise kuna wimbo moja hivi ukiimbwa unakuwa kama vile unaomboleza unafanafana na ile ya Kimasai ukawekwa kwenye radio ukawa unapigwa huku unamtaja rais kuwa ameuliwa na Ng'otanyi(waasi wa kitusi) aisee vita ikawa imeanza rasmi hata balozi sasa akawa hatoki tena tukakaa wote mle ndani hakuna kutoka kufuata chakula wala nini.

Siku ya kwanza mitaa kelele kila upande, sasa interahamwe wakaanza kuvamia hadi balozi za jirani ambao walikuwa wameondoka walinzi wao wakakimbia watu wakazidi kuuawa. chakula pale kwa ni uji tu hakuna sukari wala nini, unajua kama upo vitani mara nyingi unakuwa husikii hamu ya kula na unajiona uko powa tu kumbe unazidi kuisha ( kama kuna mtu alipigana vita humu ya kagera atadhibitisha hilo) halafu unaweza shanga kumekucha ghafla kiza kimeingia ghafla usiku mnalala usingizi wenye wa mang'amung'amu tu.

Balozi zikawa zinaendelea kuvunjwa siku zinaenda magrounet yanarushwa hovyo hovyo risasi zinalia zikitulia labda nusu saa zinaanza tena,unajua rwanda ni milima sasa unaweza kaa usiku unaona roketi inarushwa kutoka upande moja kwenda upande mwingine vimulimuli tu vya moto hadi kuna kucha kelele na risasi zinaanza tena. Sasa ikawa dhahiri kuwa hakuna namna tumuachie mungu tu.

Lakini wakati huo balozi alikuwa kwenye chumba kimoja kati vile vyumba vya sili nilivyosema hapo awali sijui alikuwa anafanya nini , ikafika ya kumi sasa ikawa hakuna kitu tena njaa tupo katikati ya vita mjini umezungukwa na wanajeshi wanapigana live bila chenga jiona ya siku hiyo ndo wakaja wanajeshi wa rwanda ,na toka siku ile ndo niliwaona live wanajeshi wa rwanda majitu yamepanda sura ngumu macho mekundu wakaja na maroli yale 24 na ile defender nyeupe ila waliokuwa kwenye ile defender hawakushuka tukaitwa uwani ubalozini .balozi akatoa tamko akasema SAFARI YA KUWAONDOA KIGALI WATANZANIA NDO IMEFIKA NA KAMA HUNA PAPER ( PASSPORT ) TAFADHARI USIPANDE KWENYE ROLI UKIPANDA LIKALOKUTOKEA MBELE USILAUMU MTU. hii kauli aliitoa kwa uchungu na kwa msisitizo sanaa huwa siisahau maishani mwangu. .

Hapo sasa ndo ngoma ikawa ngumu kila mtu akamkimbilia balozi kuomba amsaidie mkewe na watoto wake, balozi akagoma kabisa wengine akawa anawajibu kama unampenda mkeo baki nae hapa aisee watu wakawa kama vile wamepagawa maroli yapo nje lakini unashindwa kwenda kulipanda paper huna , sasa kuna kisa kimoja kilichojitokeza sintokuja kukisahau.kuna mama wa kinyarwanda mtusi alikuwa na bwanake mtanzania amezaa nae ila yeye kipindi cha vita alikuwa ameleta mzigo tanzania ,hivyo ikabidi mama ajitoe mhanga akamuita balozi awachukue wale mabinti wake mapacha wawili walikuwa kama na miaka 14 hivi weupe pua za kitusi kabisa balozi akakubali mama akabaki ,sasa tutaona mbele walivyotaka kuleta kizaazaa nusu tuchapwe RPG kwa sababu yao.

Sasa tukawa tumejipakia kwenye roli wengine wasio na vibali wakawa wamebaki pale hapo ubalozini, hapo hakuna kusikitikiana mnapeana mkono wa kwaheri basi safari ikawa imeanza na escot ya wanajeshi wa rwanda ,vizuizi kibao tukifika kwenye vizuizi wanashuka wanaenda wanajeshi wenyewe wanavitoa tunapita ,cha ajabu vizuizi vingine vilikuwa havina hata watu sijui walikuwa wakajificha au vipi.

Sasa wakati vita imepamba moto Tanzania wakawa wamefunga mpaka wake na rwanda Ikatulazimu kupitia boda ya burundi sasa kimbembe ndo kikaanza hapo, kuna wilaya kama tatu inabidi upite ndo ufike boda ya Burundi na rwanda kama sijakosea kwa kutokea kigali lazima upitie province ya butare halafu ya Gitarama ya mwisho nimeisahau kitambo sanaa. Sasa province Butare (wenyewe wanaita) ili ufike lazima uvuke mto fulani mkubwa unaitwa Nyabarongo kuna daraja kubwa hivi linalounganisha kigali na hiyo wilaya hapo sasa ndo niliona mchezo wawale jamaa saba wa defender hapo tunaenda lakini magari yanakanyaga maiti barabarani maiti zimezaga kila kona. Ile tunashuka kilima kidogo inakaribia kuulifikia kama kilomita tatu hivi wale wanajeshi wa rwanda wakageuka na gari lao ghafla wakarudi nyuma moyo ukapiga paaahhh nikahisi kuna kitu si chakawaida unageuzaje gari ghafla unarudi kwanini usituache tuvuke ndo urudi aisee.

Mbele tena kidogo ile defenda ikasimama katika ya barabara hakuna gari kuendelea kupita magali yakawa yamesimama tu ile defenda ikawa inaendelea kusogea mbele sisi tumeambiwa tusimame hapo hapo hadi Difenda itakaporudi kutoruhusu tuendelee tukawa tu pale na madereva kila mtu kwenye Kibini wengine kwenye bodi nyuma kimyaaaaaa...

Kama lisaa hivi tukasikia risasi zinalindima vibaya Sanaaa yani ikawa dhahiri kama mbele yetu kama kilomita moja watu wanapigana lisasi live ila hatuoni tatizo la rwanda mapori na vichaka vingii ila risasi zikawa zinalia kama zipo chumbani nikasema sasa huu ndo mwisho wetu.

Mwisho lisasi zikakoma tumekaa kama nusu saa hivi defenda hairudi na risasi hazisikiki tena Mwisho balozi akaamuru tuendelee na safari bila defenda dahhh ile tunafika darajani maiti kibao zimelala hapo ila hakuna defenda tukawa tunaendelea na safari tu.

Sasa tukawa tunakaribia kuimaliza province ya Butare sasa hapo ndo kulitokea kizaazaa cha wale mabinti aise tulikuta bonge la kizuizi...... Na maenterahamwe mchanganyiko na wanajeshi wa rwanda aise........ Nikasema. Sasa tunakufa.................................

Itaendelea...........................................

Sent using Jamii Forums mobile app
@MK254 mwaswast Tony njooni mjifunze huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wako hivi yaani ni kuliana timming tu,ndo mana sa hivi PK ni kuwarundika tu ndani anajua akicheza wanaanza nae

Hawa jamaa siku tu PK akija kujisahau akafanya mistake, nakwambia watawamaliza ndani ya siku moja.

Hivi hawa jamaa kwa sasa wanaoleana kweli?
 
Boss nakuomba huu Uzi upeleke jukwaa la East Africa Kenya unawafaa sana maana na wao wapo kwenye ukabila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaa ..mkono wa chuma,kila ikifika saa kumi na mbili wanajeshi wanajipanga barabarani Kigali nzima kwa tofauti ya mita 100 hawasemi wala kumgusa mtu tembea na ID masaa 24 ,ikifika saa sita usiku wakikukamata adhabu yako nikutembea nao au kukaa nao hapo hapo Hadi kuche ndo wanakuachia hakuna kesi ya uzururaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasaidia swala zima la Ulinzi kwa muda husika. Kama hutaki bugudha hiyo hakikisha kabla ya saa sita usiku uko nyumbani kwako ukiwa umelala na familia yako.
 
Hawa jamaa siku tu PK akija kujisahau akafanya mistake, nakwambia watawamaliza ndani ya siku moja.

Hivi hawa jamaa kwa sasa wanaoleana kweli?
Kwa stories za wasimuliaji na walioshuhudia hayo mauaji mpaka sasa wanakiri kuwa uwezekano wa hiko kitu hakuna.
 
Haiwezekani kabisa, sidhani kabisa hao ni kuwaombea tu maana muhutu ni kunyooshewa vidole tu"killer" na wao wana back up wakiongea ongea jela inawahusu
 
Duh, wanasafari ndefu banyarwanda, ila wahutu waliwafyeka wenzao,,lazma hii chuki izidi kuku. Ukifuatilia historia watusi ndo walianzisha uhasama kwa kujimwambafai ilhal wao ni wachache. Sasa wenzao wakamaindi waktaka kujikomboa na utumwa na umwinyi wa hao jamaa. All in all mtusi ni mtata....mhutu nae ni mkatili sasa...ndo unataka umfute mwezako ktk uso wa ardhi.

Hahaahah duh, hao jamaa walijengewa makambi hko Ngara saivi ni wamefungua mashyle na mavyuo., ngara pale 40% ya wakazi ni wanyarwanda. Unamkuta kabisa anasikiliza redio rwanda...sasa unajiuliza huyu nimtz kweli?
Kwa stories za wasimuliaji na walioshuhudia hayo mauaji mpaka sasa wanakiri kuwa uwezekano wa hiko kitu hakuna.
 
Mkuu asante sana kwa kutupa huu mkasa, Ila swali ulilomuuliza yule dada kua kwanini isiwekwe sheria ya hayo makabila mawili kuoana.. Nadhani ndio ingekua suluhisho sahihi ya kuharibu na kumaliza chuki zao hata mara baada ya PK kuondoka madarakani (either kwa uzee au kifo)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa taarifa yako Sina taaluma yeyote ya uandisha mnisamehe kwa hilo

Sent using Jamii Forums mobile app

Dingii vipi!? Hakuna tumesema we una taaluma ya uandishi, na wala hakuna sehemu tumekwambia una makosa ya kiuandishi! Na hata kama unayo sijataona sababu sipo hapa kuchunguza hilo!!

Mfano hii stori ungekuwa umeiandika yooote! Halaf hapa unatupia tu tungepata stori yenye mambo mengi zaidi! Hapa kuna visa inawezekana hujavisema sababu tu ya uharaka wa kutuwahishia tusiboreke na uzi, stori yoyote inakuwa na matawi mengi mengi, kuna vitu ulikuwa unashindwa kwenda deep nadhani sababu ya muda!

Anyway wangu ni ushauri tu una hiari ya kufanya ama kuachana nao!

Ahsante kwa simulizi
 
Sasa mkuu, huyu PK mbona sasa imasemekana mkono wa chuma hadi kwa ndugu/watusi wenzake, anaogopa nn? Mfano huyu mwanamuziki wa gospel wa juzi, na yule mwanamama alietaka kugombea urais akafungwa kisha akasamehewa.
Hata wahutu wa msimamo wa wastani walichinjwa kinyama na wahutu wenzao .nadhani umenielewa? R.i.p kizito mihigo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom