Hadithi: Bruno the Fisherman

Kweli aisee jamaa atoe ratiba mda WA kuitembelea ii thread ili tukure mambo mazur
 
Bruno The Fishman

Mtunzi.Nyemo

Episode4


Hilo lilikuwa jambo gumu ambalo lisingeweza kufanyika. Kitendo cha kumpa mwanaume huyo namba ya siri ya kadi ile ilimaanisha kwamba wangekwenda kuchukua kiasi chote cha pesa ambacho kilikuwa kikubwa mno.
Bruno hakutaka kukubali, kwake, zile pesa zilikuwa kila kitu, alizitaka na ndiyo maana aliamua kumpambania mzee Todd kumfikisha salama alipokuwa akipataka yeye lakini si kuona akipoteza pesa zile.
Jamaa huyo aliona kama alifanyiwa kiburi kwa kutopewa namba ya siri ya kadi ile, akachukua bastola yake na kuwanyooshea huku akitaka aambiwe kuhusu namba hizo.
Wakati kila mmoja akijua kwamba walikuwa wakipigwa risasi, ghafla mlango ukafunguliwa na wanaume wawili kuingia humo. Mmoja alikuwa yule kiongozi wao aliyekwenda kuitwa kwa lengo la kuja kuwaona watu waliokuwa wamewakamata.
Kiongozi huyo alipofika hapo, akawaangalia watu hao. Ghafla, akashtuka, hakuamini kumuona mtu huyo mahali hapo. Hakuwa mzee Todd, bali alikuwa Bruno.
Akamsogelea na kumwangalia vizuri. Alimfahamu mtu huyo japokuwa ilipita miaka kumi hawakuwa wameonana. Bruno alibaki akimshangaa mtu huyo, hakumfahamu na aliona kabisa kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kumuona mbele ya macho yake.
“Bruno!” aliita mwanaume huyo kitu kilichomfanya Bruno kushtuka, si yeye tu bali hata watu wengine waliokuwa mahali hapo.
“Who the hell are you?” (wewe nani?) aliuliza Bruno huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Niangalie! Hunijui kweli?” aliuliza mwanaume huyo kwa Kiswahili kilichomfanya Bruno kugundua kwamba mtu huyo alitoka Afrika Mashariki.
Bruno alimwangalia, hakuweza kumkumbuka mwanaume huyo, kwake, alionekana kuwa mgeni kabisa. Aliyaangalia mavazi aliyokuwa ameyafaa, yalimuonyesha jinsi alivyokuwa katili na mtemi katika mtaa huo.
“Bruno! Umenisahau Ibrahim Onyango! Kiongozi wa watoro shuleni!” alisema mwanaume huyo.
Alipolitaja jina la Onyango tu, kumbukumbu za Bruno zikaanza kurudi nyuma. Akamkumbuka mwanaume huyo, aliwahi kusoma naye sekondari mpaka pale walipomaliza shule na kufeli vibaya huku yeye akianza kazi ya uvuvi.
Onyango alikuwa kiongozi wa watoro shuleni kwao, hakupenda kusoma, kila siku aliwaambia wazazi wake kwamba shule ilimkataa na ilikuwa ni lazima kuondoka Kenya na kuelekea Afrika Kusini kutafuta maisha.
Wazazi wake walizungumza naye sana, walikuwa ni wazazi waliokuwa na uuwezo mkubwa, walimpa kila kitu lakini Onyango hakutaka kukubali, mali zile alisema ni za wazazi wake na yeye ilikuwa ni lazima kutafuta mali zake, hakuona sehemu ambayo angepata maisha mazuri zaidi ya kwenda Afrika Kusini.
Alitoroka Kenya na kuelekea Afrika Kusini. Watu walishangaa lakini yeye aliamua kuwa na maisha yake. Miaka zaidi ya kumi ilikuwa imepita, leo, Bruno alikutana na Onyango Afrika Kusini huku akiambiwa kwamba huyo ndiye alikuwa kiongozi wao.
“Unafanya nini huku?” aliuliza Onyango huku akimwangalia Bruno.
“Ni habari ndefu sana! Tunaweza kwenda sehemu kuongea nje ya hapa manake hizi bunduki zinanikosesha amani kabisa,” alisema Bruno.
“Haina noma!”
Bruno hakutaka kubaki peke yake, aliamini kwamba kama angemuacha mzee Todd ndani ya chumba kile basi angepigwa mikwara na kutoa namba za siri za kadi, alichokifanya ni kuondoka na mzee huyo kwenda uani na kuanza kuzungumza na Onyango.
Waliongea kwa furaha, walicheka na kukumbushiana mambo mengi ya nyuma. Muda wote huo mzee Todd alikuwa akiwasikiliza tu, hakuelewa Kiswahili, alibaki kimya huku mawazo yake yakiwa yanaifikiria familia yake tu.
“Ikawaje?”
“Washikaji wakanitosa baharini! Mtu wangu nilipiga mbizi mpaka nikaokolewa na Warusi,” alisema Bruno.
“Na huyu mzee vipi?”
“Nilimkuta kwenye meli hiyo, wana walitaka kumuua, ila nilipotoroka, nikatoroka naye!”
“Wewe ninja! Yaani ulitoroka kwenye meli, wewe ninja mchizi wangu,” alisema Onyango huku akitoa tabasamu pana.
Waliendelea kukaa uani na kuendelea kuzungumza. Wakati mazungumzo yakiwa yamepamba moto, wakaanza kusikia kelele kutoka mtaani, hawakujua kulikuwa na nini. Wakati wakiwa wanajiuliza, wakaanza kusikia milio ya risasi, ilikuwa ni kama milio ya majibizano.
Kila mmoja akaogopa, Onyango akachukua bunduki yake, akapanda ukuta na kuangalia kwa nje kuona kulikuwa na nini. Macho yake yakatua kwenye gari moja jeusi, lilikuwa jipu, kulikuwa na Wazungu wanne waliovalia suti ambao walikuwa wakipambana na vijana wake.
“Kuna nini?” aliuliza Bruno huku akiogopa.
“Wazungu! Wamekuja kupambana! Sijui kuna nini!”
“Tufanye nini?”
“Njooni huku!”
Aliwachukua na kuwapeleka katika mlango mwingine wa kutoka ndani ya eneo la nyumba hiyo na kuwaambia wakimbie kwani hawakujua watu hao walikuwa wakina nani na walihitaji nini.
Hilo halikuwa tatozo, wakaagana na kuanza kukimbia mahali hapo. Milio ya risasi iliendelea kusikika kila kona. Wazungu wale walikuwa hatari, walikuwa na shabaha kupita kawaida, kila risasi iliyokuwa ikitoka, ilitoka kwa malengo na kumpata mtu.
Japokuwa Soweto kulizoeleka kusikika milio ya risasi lakini siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti. Soweto ilibadilika na kuwa kama uwanja wa mapambano. Watu weusi wengi waliuawa na hakukuwa na mtu aliyejua sababu iliyowafanya Wazungu hao kufika humo na kuanza kushambulia.
Bruno na mzee Todd waliendelea kukimbia, hakukuwa na mtu aliyesimama, kila mtu alikuwa akiokoa maisha yake. Wakakimbia mpaka mlimani na kuanza kuangalia kwa chini kwa mbali.
Waliwaona watu wakipambana, milio ya risasi iliendelea kusikika kwa sauti kubwa huku watu wengine wakikimbilia kule walipokuwa.
“Mungu wangu! Nimesahau kadi ya ATM kwa yule jamaa,” alisema Bruno mara baada ya kujipekua mifukoni kuangalia kadi ile.
“Unasemaje?”
“Kadi na simu! Tumesahau ndani ya nyumba ile,” alisema Bruno huku akionekana kuchanganyikiwa, kwake, ilikuwa ni afadhali kusahau simu lakini si kadi ya ATM.
“Tuondoke! Achana navyo! Tuondoke!” alisema mzee Todd, kwake, pesa zilizokuwa katika akaunti aliyofungua Bruno kilikuwa kiasi kidogo sana cha pesa.
“Haiwezekani!”
“Bruno! Tuondoke!”
“Siwezi kuondoka na kuacha kadi ile. Ni lazima nirudi!”
“Urudi?”
“Ndiyo!”
“Kule kwenye mapambano?”
“Hukohuko!”
“Haiwezekani!”
“Siwezi kuendelea mbele pasipo ile kadi. Kuna hela nyingi sana, hatuwezi kuacha kadi kiholelea,” alisema Bruno.
Walikuwa wakivutana, mzee Todd alimwambia Bruno kwamba walitakiwa kuondoka lakini kijana huyo hakutaka kuelewa kitu chochote kile. Alichomwambia ni kwamba amsubiri pale na yeye kwenda kule kuchukua kadi.
Alikuwa akikimbia kuteremka mlima. Alipishana na watu waliokuwa wakipandisha, kila mmoja alikuwa akimshangaa, wao walikuwa wakikimbia risasi lakini ndiyo kwanza Bruno alikuwa akizikimbilia. Walimuona kama mtu aliyechanganyikiwa lakini mwenyewe hakuwa tayari kuona akirudi nyuma, kwake, kadi ile ilikuwa muhimu kuliko kitu chochote kile.
Milio ya risasi iliendelea kusikika lakini hakujali, alipofika, akaanza kupita kwenye vichochoro. Alikuwa peke yake, watu wengine walikuwa wamejifungia vyumbani mwao na wengine kukimbia.
Hakukumbuka mahali nyumba ile ilipokuwa lakini baada ya kukumbuka kwamba ndipo mahali watu wale walipokuwa wakipambania, akaanza kufuatilia milio ya risasi hiyo.
Alitembea harakaharaka kwa kujificha mpaka alipofika mahali ilipokuwa nyumba ile. Hakutokea kule ilipokuwa nyumba ile bali alipotokea ni nyuma ya gari la Wazungu wale waliokuwa wakipambana. Akawaangalia vizuri Wazungu wale, jinsi walivyokuwa wakipambana na hata kukwepa risasi, akagundua kwamba hawakuwa watu wa kawaida hata kidogo, mafunzo waliyokuwa nayo yalikuwa hatari mno.
“Who the hell are these people?” (hawa ni wakina nani?) alijiuliza swali alilokosa jibu, kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka mfululizo.
***
Mawasiliano yakafanyika haraka sana kutoka nchini Marekani, maofisa wa CIA waliokuwa nchini Afrika Kusini walitakiwa kwenda kule simu ilipopigwa ambapo wakaelekezwa na kuelekea huko. Walipofika katika kituo cha treni jijini Johannesburg ambapo ndipo mzee Todd alipokuwa amepiga simu, hawakuweza kumuona mzee huyo.
Haraka sana wakawapigia simu maofisa waliokuwa nchini Marekani na kuwaambia kile kilichokuwa kikiendelea kwamba mwanaume huyo hakuwa mahali hapo. Hilo halikuwa tatizo, kwa kutumia satalaiti yao kwa mfumo wa GPS, wakaweza kuiunganisha simu ya mzee Todd na wao kuweza kuona jinsi simu ile ilipokuwa kipindi hicho.
Waliona ikiwa inatoka sehemu moja kwenda nyingine, hawakutaka kubaki mahali hapo kwani kutoka katika kituo hicho mpaka mahali simu hiyo ilipokuwa hakukuwa mbali. Wakaondoka na kumfuata mahali alipokuwa kwani simu ile ilionyesha kwamba ilikuwa katika Mtaa wa Soweto.
Hawakuchukua muda mrefu wakawa wanakaribia kuingia katika mtaa huo. Walipoangalia tena kifaa chao wakaona kwamba simu imetulia sehemu moja kitu kilichowafanya kujua kwamba ilikuwa imewekwa ndani, sehemu fulani na watu hao kutulia.
Waliijua Soweto, walijua tabia za watu wa huko kwamba hawakuwa na mchezo hata mmoja, walizijua chuki zao kali dhidi ya Wazungu, walijua kabisa kama wangekwenda kimama basi ilikuwa ni lazima kuuawa.
Wakakaanda bastola zao na kuingia ndani huku wakiwa na gari lao ambalo vioo vyake havikumruhusu mtu wa nje kuona ndani. Walipofika katika eneo ambalo halikuwa mbali na mahali simu ilipokuwa, wakasimamisha gari lao.
Nyumba iliyokuwa mbele yao ndiyo ambayo ilikuwa na mtu waliyekuwa wakimtafuta, nje ya nyuumba ile kulionekana vijana mbalimbali wakifanya mambo yao, wengine walikuwa wakipiga stori na wengine kujitenga pembeni huku wakivuta bangi.
“Tufanye nini?” aliuliza jamaa mmoja.
“Tukavamie!”
“Ila tuwe makini kwanza, tunaweza kufa na mbaya zaidi hatujui wale jamaa wana nini,” alisema mwingine.
Wale vijana waliokuwa nje ya nyumba ile walionekana kulishuku gari lile, lilikuwa limekuja mahali pale na kusimama, hawakujua kulikuwa na kitu gani kilichokuwa kikiendelea lakini wakahisi kabisa kwamba watu waliokuwa humo ndani hawakuwa watu wema.
Wakachukua bunduki zao na kuanza kulisogelea. Maofisa wale wa CIA walipowaona wanakuja, wakaziandaa bastola zao kwa lengo la kushambuliana kwani walijua kwamba kama wale vijana wangejua kwamba ndani ya gari lile walikuwemo wao, Wazungu basi ilikuwa ni lazima kuwamaliza.
“Paa!” ulisikika mlio mmoja wa risasi, jamaa mmoja wa pale Soweto miongoni mwa wale vijana waliokuwa wakipiga hatua akaanguka na damu kuanza kumtoka kifuani.
Vijana wale wakashtuka na kugundua kwamba kweli watu wale hawakuwa wazuri kwao, wakajificha na kuanza kushambuliana nao. Milio ya risasi ilisikika kila kona mahali hapo, wale waoga, wakakimbia lakini waliokuwa na bunduki nao wakajiweka sawa na kuanza kupambana na watu hao.
Bruno alikuwa amekwisharudi na kuwa nyuma ya gari la maofisa wale wa CIA, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya kwani kwa jinsi alivyokuwa mweusi, kama angejitokeza mbele ya watu wale ilikuwa ni lazima kumuua kwa kuwa wangehisi kwamba naye alikuwa adui.
Hakuondoka mahali hapo, alijibanza kwenye ukuta huku akifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Baada ya dakika kadhaa, milio ya risasi ikaacha, Wazungu wale wakajua kwamba watu weusi waliokuwa wakipambana nao, wote walikuwa wamekufa na hivyo kuanza kuingia ndani.
Walipofika, ni maiti tu ndizo zilizokuwa zikionekana huku zikiwa zimetapakaa damu. Ndani ya nyumba ile, wakaanza kumtafuta mzee Todd ambaye walijua kwamba alikuwa humo kwa kuwa bado GPS ilionyesha kwamba simu ile ilikuwa humo ndani.
Wakafanikiwa kuipata lakini kitu cha ajabu, mzee huyo hakuwepo. Wakaanza kuangalia katika kila chumba, wakafungua milango na kuingia ndani lakini hawakuweza kumuona mzee huyo ambaye walifika hapo kwa lengo la kumtaka yeye tu.
Walipohakikisha kwamba hakuwepo, hawakutaka kupoteza muda kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka na kuziacha maiti mulemule ndani ya nyumba ile.
Wakati wanatoka, wanaingia ndani ya gari lao na kuondoka mahali hapo, bado Bruno alikuwa amejibanza kwenye kile kiukuta, alipoona gari limeondoka mahali hapo, haraka haraka akatoka na kwenda ndani ya nyumba ile.
Hali aliyoikuta humo ilimuogopesha mno, hakuwahi kufikiria hata siku moja kwamba katika maisha yake kuna siku angeweza kuziona maiti nyingi zikiwa zimetapakaa kama ilivyokuwa siku ile.
Akaziruka na kumfuata yule mwanaume ambaye aliichukua ile kadi na kuanza kumpekua mifukoni mwake, akabahatika kuikuta kadi ile ambayo aliichukua na kuondoka zake.
Bado mtaa ulikuwa kimya, hakukuwa na mtu aliyethubutu kutoka ndani ya nyumba yake kwa kuhofia maisha yake, kila mtu alibaki ndani huku dakika zikiendelea kwenda mbele.
Bruno alipoondoka hapo, moja kwa moja akaelekea kule mlimani, alikuwa akikimbia, alichoka lakini hakutaka kusimama, kwake, mzee Todd alikuwa kila kitu, alihitaji kumsaidia mzee huyo kwa kuwa alionekana kuhitaji msaada kupita kawaida.
Alipofika kule juu, akamkuta pale pale alipomuacha na kumuonyeshea kadi ile kwamba alifanikiwa kuipata kitu kilichoonekana kumfurahisha mzee yule.
“Kwa hiyo?” aliuliza mzee Todd.
“Tuondoke tukapange vyumba hotelini,” alisema Bruno na kuanza kuondoka hapo.
Mzee Todd hakutaka kuvua miwani wala kofia aliyokuwa ameivaa, hakutaka kugundulika na mtu yeyote yule, alijua kwamba alikuwa akitafutwa kila kona hivyo kama angeendelea kujificha hivyo basi ingemsaidia kuwa salama mpaka siku ambayo angefanikiwa kufika nchini Marekani.
Alijua kwamba kutafutwa kwake ni Maxwell ndiye alikuwa amefanya hivyo, alihisi kitu hicho kwani mbali na kuwa na urafiki wa mashaka lakini kila mmoja alihitaji kuwa na nguvu ya kibiashara kitu kilichoonekana kuvuruga kila kitu.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika sehemu iliyokuwa na hoteli ndogo iitwayo Elizabeth Royal, moja kwa moja wakaelekea mpaka mapokezi ambapo wakafanya harakati za kuchukua chumba.
“Tutakaa kwa siku tano,” alisema Bruno ambaye akachukua ile kadi na kumpa dada wa mapokezi ambaye akaingiza namba za kadi katika kompyuta yake na kuchukua kiasi kilichotakiwa kama malipo kwa muda huo. Alipomaliza, akawapa kadi zilizotumika kama funguo na kuondoka mahali hapo kuelekea vyumbani kupumzika.
***
Maxwell alichanganyikiwa, mpaka kipindi hicho hakujua mahali mzee Todd alipokuwa. Alihisi kabisa kichwa chake kikichanganyikiwa, mwanaume huyo alikuwa muhimu mno kwake, alimtaka kwa udi na uvumba na ndiyo maana alihangaika kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba anauawa kwa gharama yoyote ile.
Vijana waliokuwa nchini Afrika Kusini nao hawakuweza kumsaidia kwa chochote kile, kila alipowapigia simu walimwambia kitu kimoja kwamba bado waliendelea kumtafuta na hawakujua mahali alipokuwa.
Alikuwa na familia yake, ilikuwa ni lazima kuhakikisha kwamba watu hao hawaondoki mikononi mwake, alihakikisha kwamba anawafanyia umafia wa nguvu hata kama mzee huyo hakuonekana.
Alimpa saa sabini na mbili ambazo zilikuwa ni siku tatu, alijua kwamba kwa jinsi alivyokuwa akiipenda familia yake, ilikuwa ni lazima mzee Todd afanye kila liwezekanalo kufika nchini Marekani.
Siku ya kwanza ikakatika, ya pili ikaingia na kukatika lakini bado majibu yalikuwa yaleyale kwamba Todd hakuonekana na vijana wake walikuwa wakiendelea kumtafuta kila kona bila mafanikio.
“Kwa hiyo?” aliuliza kijana mmoja kwenye simu, alitaka kusikia kutoka kwa bosi wake kama ilikuwa ni muhimu kuimaliza familia yake hata kama hakuwa amerudi au walitakiwa kusubiri.
“Tuongeze siku mbili, inawezekana akafika,” alisema Maxwell.
Hawakuwa na jinsi, wakaongeza siku mbili huku wakiendelea kuitunza familia yake kwa chakula na vitu vingine. Kila siku Juddie alikuwa kwenye maumivu makali, hakujua mahali mume wake alipokuwa, alitamani kumuona, hata kama asingemuona akiwa hai basi aione hata maiti yake na kujihakikishia kwamba mume wake alifariki dunia.
Siku hizo zilipokwisha, Maxwell hakuwa na jinsi, akamwambia kijana yule awamalize na kisha kuipiga picha miili ya watu hao ili baadaye amtumie mzee Todd na kumwambia kwamba aliiteketeza familia yake na alibaki yeye tu, na ilikuwa ni lazima amtafute na kumuua.
“Kill them both,” (waue) alisema Maxwell kwenye simu.
“Hakuna shida bosi!” alisema kijana huyo na kukata simu, utekelezaji ulitakiwa kufanyika mara moja.
***
Japokuwa walikuwa wamepatana kukaa mahali hapo kwa muda wa wiki moja lakini mpaka kipindi cha mwezi nzima Bruno na mzee Todd walikaa ndani ya hoteli hiyo waliyokuwa wamechukua chumba.
Hawakuonekana kuwa na hofu yoyote ile kwani kwa jinsi walivyokuwa ilikuwa vigumu sana kumgundua mzee Todd kwamba alikuwa mtu aliyekuwa akitafutwa mno kutokana na sakata la madawa ya kulevya lililokuwa likimkabiri.
Waliishi kwa amani japokuwa muda mwingi mzee huyo alikuwa akimfikiria mke na mtoto wake. Hakujua kama watu hao walikuwa hai au la kwani tangu alipopewa muda wa saa sabini na mbili mwezi uliopita, hakuwasiliana nao tena.
Hakuonekana kuwa na raha hata kidogo, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele. Alitamani kuondoka barani Afika, hakutaka kuendelea kuishi huko na wakati hakujua familia yake ilikuwa ikiendeleaje nchini Marekani.
Dada wa mapokezi, Thandi ambaye aliwapokea katika hoteli waliyokuwa wamechukua chumba alionekana kuwa na wasiwasi na wateja hao. Mtu aliyemtia hofu alikuwa mzee Todd ambaye muda wote aliokuwa akiongea, kofia na miwani haikutoka mwilini mwake.
Alikuwa akijiuliza mambo mengi kuhusu mtu huyo, hakujua sababu ya kufanya hivyo, alijaribu kumwangalia vizuri zaidi lakini hakupata jibu juu ya mwanaume huyo, hakujua alikuwa nani na kwa nini hakutaka kuondoa kofia wala miwani aliyokuwanayo.
Alijaribu kuvumilia, alitaka kuona kama ingetokea siku moja mzee huyo kuvua kofia yake lakini jambo hilo halikuweza kutokea, kila alipokuwa akitoka chumbani kwake kofia yake ilikuwa kichwani.
Japokuwa lilionekana kuwa jambo la kawaida lakini kwa mhudumu huyo likaonekana kuwa jambo moja kubwa sana kwani katika kipindi hicho kulikuwa na matukio mengi ya kigaidi yaliyokuwa yakitokea nchini Afrika Kusini, akahisi kwamba inawezekana mzee yule alikuwa mmoja wa magaidi waliotaka kuilipua hoteli yake.
Kukosa amani kwake kukampeleka kumuhadithia mpenzi wake nyumbani. Alimwambia ukweli kuhusu wageni hao waliokuwa wamechukua mwezi mzima kazini kwake lakini katika kipindi chote hicho hakuwahi kuona kofia ikitoka kichwani mwa mzee Todd.
“Mwezi mzima?” aliuliza mpenzi wake.
“Ndiyo! Ni mwezi mzima ile kofia ipo kichwani,” alijibu Thandi.
“Mmh! Labda kuna kitu hapo, umejaribu kufuatilia kwa karibu kujua sababu?” aliuliza mpenzi wake.
“Hapana! Ila anaonekana ana pesa sana kwani hivyo vinywaji anavyokuywa, ni balaa,” alisema Thandi kwa lengo la kumsifia mzee Todd.
Wakati wakizungumza mambo kuhusu wageni hao, kichwa cha mpenzi wake kikaenda sehemu nyingine kabisa. Yeye alikuwa mmoja wa vijana waliokuwa wamewekwa nchini Afrika Kusini kwa lengo la kumtafuta mzee Todd. Alikuwa kijana wa Maxwell ambaye aliamua kuwatawanya wengi nchini humo kwa kuamini kwamba mzee Todd alikuwa ndani ya Afrika Kusini.
Alipoambiwa na Thandi kuhusu jambo hilo, hakutaka kubaki nalo bali alichokifanya ni kwenda kuwaambia vijana wenzake kile alichoambiwa na mpenzi wake kwani hata naye alikuwa na hofu tele kwa kuhisi kwamba inawezekana huyo Mzungu alikuwa ni yule Todd waliyekuwa wakimtafuta.
“Sasa kofia si jambo la kawaida tu,” alisema mwenzake baada ya kupewa taarifa.
“La kawaida? Unajua kwamba inawezekana akawa Todd tunayemtafuta?”
“Ni vigumu! Hivi Todd anavyotafutwa anaweza kuwa hotelini kweli?”
“Inawezekana kwani hayupo peke yake, yupo na kijana mwingine. Mmesahau tulivyoambiwa kwamba kwenye meli Todd alikuwa na kijana mwingine wa Kiafrika?” aliuliza mpenzi wa Thandi.
Hilo kidogo likawaingia vichwani mwao. Ilitakiwa kuanza kufuatilia na kujua watu hao walikuwa ni wakina nani na kwa nini mwanaume huyo wa Kizungu alikuwa akivaa kofia muda wote.
Walichokifanya ni kuwatuma vijana wawili na kuanza kuwafuatilia katika hoteli hiyo. Vijana hao wakaenda na kupanga vyumba huku wakitakiwa kufuatilia kila hatua ambayo watu wale walikuwa wakichukua.
Baada ya siku mbili, vijana hao wakafanikiwa kumuona Bruno na mzee Todd wakiendelea na maisha yao kama kawaida hotelini pale. Kwa kumwangalia mzee Todd, kwao halikuwa na ugumu kugundua kama huyo alikuwa mzee huyo.
Haraka sana wakawaambia wenzao kwamba walimwangalia mzee huyo na kugundua kwamba alikuwa yuleyule waliyekuwa wakimtafuta na hivyo vijana hao kupiga simu kwa Maxwell na kumwambia kilichokuwa kikiendelea.
“Safi sana! Hakikisheni haondoki ndani ya hoteli hiyo,” alisikika Maxwell kwenye simu.
“Kwa hiyo tumuue au?”
“Hapana! Atekwe, msimuue hapo hotelini, watu wakikusanyika mnaweza kukamatwa na kuniletea matatizo,” alisikika Maxwell.
Mipango ya kutekwa kwao ikapangwa, hawakutakiwa kutekwa wakiwa vyumbani mwao bali walitakiwa kutekwa wakati wakiwa katika mgahawa wa hotelini hapo walipokuwa wakila.
Hilo wala halikuwa tatizo, walichokifanya ni kusoma ratiba yao kwanza. Wakagundua kwamba watu hao wawili walikuwa wakishuka mgahawani saa nne asubuhi, saa sita mchana na saa mbili usiku, hivyo kama walitaka kuwateka basi hiyo ndiyo mida yao waliyokuwa wakitoka kwenda kula.
“Tuwatekeni usiku, nadhani hiyo itakuwa salama zaidi,” alisema kijana mmoja na kukubaliana. Siku iliyofuata ndiyo ilikuwa siku ya kufanya tukio hilo, kuanzia asubuhi mpaka jioni walikuwa wakiwafuatilia kwa makini sana.
Majira ya saa moja hata kabla hawajakwenda kwenye mgahawa, tayari vijana hao walikuwa wamefika mahali hapo huku wakiwa na bastola zao viunoni.
Wakati Bruno na mzee Todd wakishuka kwenda kula, walikuwa wakiwaangalia tu, wakawaona wakiifuata meza moja, wakakaa na kuanza kula huku sehemu yote hiyo ikiwa na watu.
“Kwa hiyo? Tuwafuate sasa hivi?” aliuliza jamaa mmoja.
“Umewaambia washikaji waandae gari?”
“Ndiyo! Walisema gari lipo tayari hapo nje ya hoteli,” alijibu mwingine, walikuwa wakiongea kwa sauti ya chini.
“Basi sawa. Twende!”
Wakainuka na kuanza kuwafuata watu hao, walipowafikia katika meza ile, wakatoa bastola zao kisiri sana na kuwaambia wasimame. Kwanza walitaka kubisha lakini hata kabla ya kufanya hivyo, wakaziona bastola hizo kitu kilichowafanya kuogopa.
Waafrika Kusini hawakuwa watu wa mchezo, waliwafahamu, walikuwa na michezo ya kutisha na bastola zao, walikuwa wepesi kuua, kwao, kumwaga damu ilikuwa ni kama kumchinja kuku au kumuua panzi.
Wakainuka na kuanza safari ya kuelekea nje ya mgahawa ule huku wakiwa wametangulizwa mbele. Hakukuwa na mtu yeyote aliyegundua kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo, walichokiona ni marafiki wanne walikuwa wamewafuata wenzao na kuondoka mahali hapo.
Walipofika nje, tayari wenzao walikuwa katika gari moja mahali hapo, walichokifanya ni kuwataka kuingia garini na baada ya hapo, gari likawashwa na kuondoka mahali hapo kwa mwendo wa kawaida kana kwamba hakukuwa na kitu kibaya kilichokuwa kimetokea.
Hata kabla hawajafika mbali, kijana mmoja aliyekuwa amebaki ndani ya gari lile na dereva akachukua simu yake, akabonyeza namba fulani, baada ya sekunde kumi akaanza kuzungumza na mwanaume wa upande wa pili ambaye alikuwa Maxwell.
Alimwambia kwamba mtu aliyekuwa akihitajika alikuwa mikononi mwao hivyo walitaka kufuata maelekezo ya juu ya nini cha kumfanya mtu huyo.
“Just kill him,” (muueni tu!)
“And the other guy?” (na huyu mwingine?)
“Who is he?” (nani huyo?)
“He was with him, should we kill him too?” (alikuwa naye, naye tumuue pia?) aliuliza.
“Kill them both,” (waueni wote)
“Ok sir,” (Sawa bwana mkubwa) alisema kijana yule na hapohapo akaanza kuikoki bunduki yake, kilichotakiwa kufanywa ndani ya gari hilo ni mauaji tu.
Bruno na mzee Todd walijua kile kilichokuwa kikienda kutokea kwani waliisikia sauti iliyokuwa ikizungumza na kijana yule, wakajua kabisa kwamba walikuwa wakienda kufa humo garini.
Walitamani kuruka kupitia dirishani lakini walishindwa, vioo vilifungwa na mbaya zaidi walikuwa wamewekwa mtu kati hivyo wasingeweza kufanya kitu chochote kile.
Wakaanza kuomba msamaha, hawakutaka kufa kikatili ndani ya gari. Bruno ndiye aliyekuwa akilia sana, moyoni mwake alimkumbuka mpenzi wake, Sharifa, ilikuwa ni lazima aondoke Afrika Kusini kwenda nchini Kenya kumuona mpenzi wake aliyekuwa akimpenda kwa moyo wa dhati. Wakati wakiwa wanasali sala zao za mwisho, tayari vijana waliokuwa mule garini walikwishamaliza kuzikoki bastola zao na kilichosikika baada ya hapo ni milio ya risasi tu huku gari likiwa kasi.
“Paaa! Paaa! Paaa!” milio ya risasi ikasikika na damu kutapakaa garini.
***
Bado msichana Thandi alikuwa na hofu tele juu ya watu waliokuwa wamefika katika hoteli yao na kuchukua chumba, mwanaume yule wa Kizungu kila siku alikuwa na kofia kichwani mwake na miwani, hakutaka kuitoa, alipokuwa akifika mapokezini, alikuwa na vitu hivyo na hata alipokuwa akiingia ndani ya gari pia alikuwa na vitu hivyo.
Hilo lilizidi kumtia hofu msichana huyo, hakutaka kukubali, aliona kabisa kwamba ilikuwa ni lazima amwambie bosi wake juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwani kwa muda wa mwezi mzima mwanaume huyo kuwa hivyohivyo, lilionekana kuwa jambo gumu.
Mbali na kuzungumza na mpenzi wake, akazungumza na meneja wa hoteli hiyo ambaye naye akaanza kufuatilia na kugundua kwamba kulikuwa na ukweli kwa kile alichokuwa akiambiwa.
Hakutaka kuchelewa, meneja huyo akazungumza na polisi na kuwaambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Polisi hao walitaka kuthibitisha kile kilichokuwa kikiendelea na hivyo kwenda katika hoteli hiyo kujionea kwa macho yao.
Siku ambayo walikwenda na kuonyeshewa watu hao ndiyo siku ambayo Bruno na Todd walikuwa kwenye mgahawa wakila. Polisi waliokuwa na nguo za kiraia walikuwa mahali hapo, bastola zilikuwa viunoni mwao, walijiandaa na kitu chochote kile ambacho kingetokea mahali hapo.
Baada ya dakika kadhaa, wakawaona wanaume wawili wakisimama na kuwafuata watu wale waliowafuata, walisimama karibu nao na kuanza kuzungumza nao. Walikuwa polisi, walijua kila kitu alichokuwa akikifanya adui. Japokuwa watu wengine hawakuwa wameziona bunduki walizozionyesha watu hao kisiri na kuwataka kusimama, wao waliziona vizuri kabisa.
“What the hell is going on?” (nini kinaendelea?) aliuliza polisi mmoja huku jicho lake likiangalia kule kwa wizi.
“I don’t know, let’s keep waiting,” (sijui, hebu tuendelee kusubiri) alijibu mwenzake.
Baada ya sekunde kadhaa wakawaona watu wao wakisimama na kuanza kupiga hatua kwenda nje huku wale jamaa wakiwafuata kwa nyuma. Haikuwa ngumu kwao kugundua kwamba watu wale walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi na hivyo kuanza kuwafuatilia.
Walipofika nje, wakawaona wakiingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo. Nao hawakutaka kubaki, wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka kwa kulifuatilia gari lile.
Walilifuatilia gari hilo ambalo lilichukua Barabara ya Western Bypass ambayo ilikuwa ikielekea Upande wa Kaskazini mahali kuitwapo Woodmead kulipokuwa na makorongo makubwa. Magari yalikuwa yakitembea kwa mwendo wa kawaida, hawakusubiri sehemu yoyote ile, ilikuwa ni lazima kulifuatilia na kujua mwisho wa safari hiyo ilikuwa wapi.
Hawakuwa mbali kutoka katika gari hilo, ilikuwa ni sawa na hatua tano za miguu ya binadamu. Wakati wakiwa wamekwishafika Bryston, wakashangaa kuona mwanaume mmoja akitoa bastola yake ndani ya gari. Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea lakini waliangalia vizuri kabisa na kumuona mtu huyo akiwa na bastola yake dakika chache baada ya kuongea kwa simu.
“Stephen, take your gun and do the work,” (Stephen, chukua bastola yako ufanye kazi) alisema mwanaume aliyekuwa akiendesha gari.
Hilo halikuwa tatizo kwa huyo mtu aliyeambiwa kwani alikuwa miongoni mwa polisi waliokuwa na shabaha kubwa, alichokifanya, kama muvi vile akatokeza nusu ya mwili wake nje ya gari kupitia dirishani na kisha kunyoosha mkono wenye bastola kuelekea katika gari lile.
Watu waliokuwa pembeni walishangaa, hawakujua sababu ya mwanaume yule kufanya hivyo lakini hata kabla hawajapata majibu, Stephen akaachia risasi kadhaa ambazo zilipenya katika kioo cha nyuma, mwanaume mmoja akapigwa risasi ya shingo kwa nyuma, kwa kupagawa, wenzake wakaanza kurushiana risasi na Stephen ambaye alikuwa kwa nyuma na alikuwa akiwaona vizuri kabisa.
Kila mmoja akawasahau watu wao na hivyo kuanza kupambana na Stephen aliyeonekana kuwa si mtu wa mchezo hata kidogo. Mwenzake aliyekuwa ameshikilia usukani alijua vilivyo namna ya kupambana na watu waliokuwa kwenye gari hivyo alichokifanya ni kuendesha kwa kasi na kusimama upande wao wa kulia na hivyo kumpa nafasi Stephen kufanya kile alichokitaka.
Watu waliokuwa pembeni wakaanza kukimbia, kila mtu alikuwa akiyaokoa maisha yao kwani hali ilionekana kutisha na ilionekana kabisa kwamba muda wowote ule risasi zile zingewapata.
“Deal with the driver,” (shughulika na dereva) alisema dereva.
Hilo halikuwa na tatizo hata kidogo, haraka sana Stephen akaanza kushughulika na dereva aliyekuwa ameambiwa. Ni ndani ya sekunde thelathini tu, risasi mbili zikaingia katika mikono ya dereva, hakuendelea kuushikilia usukani na hivyo gari hilo kutoka barabarani na kuanza kuingia korongoni kwa kasi.
***
Abdul na Sharifa walikuwa wakikimbia kwa kasi, nguo ya harusi tena huku akiwa amepambwa vizuri ilikuwa mwilini mwa Sharifa lakini hakutaka kujali, alikuwa akikimbia huku akimfuata Abdul ambaye alimwambia kwamba mpenzi wake, Bruno alikuwa hai na hakufa kama alivyokuwa ameambiwa.
Moyo wake ulikuwa kwenye majonzi mazito, hakuamini kama alithubutu kukubali kuolewa na mwanaume mwingine na wakati hakuwa na uhakika kama mpenzi wake aliyempenda kwa mapenzi ya dhati alikufa kweli au la.
Walichukua dakika kumi kukimbia, wakasimama nje ya nyumba moja ambapo Abdul alimwambia kwanza wapumzike kwani walikuwa wamekaribia kufika kule alipoambiwa kwamba bruno alikuwepo.
Walipumzika pasipo kuongea kitu chochote kile, baada ya dakika kadhaa, ikambidi Sharifa aulize vizuri kama kweli kile alichokuwa amemwambia kule harusini kilikuwa kweli au alimdanganya.
“Bruno yupo wapi?” aliuliza Sharifa huku akimwangalia Abdul.
“Nimeambiwa alipiga simu. Twende kwa Alfred, yeye ndiye aliyepokea simu kutoka kwake na kumwambia kwamba Bruno yupo hai,” alisema Abdul.
Sharifa alionekana kukakasirika lakini hakuwa na la kufanya, walichokifanya ni kuanza kwenda kwa huyo Alfred huku akitaka kujua ukweli juu ya kile alichokuwa ameambiwa.
Walipofika, kijana huyo akawaweka kwenye kochi na kuanza kuzungumza nao. Aliwaambia kwamba alipokea simu kutoka kwa Onyango na kumwambia kwamba Bruno alikuwa hai, tena aliongea naye mwenyewe.
“Onyango?” aliuliza Abdul huku akionekana kutokuamini alichokisikia.
“Ndiyo! Onyango huyohuyo!”
“Yule aliyekimbilia Afrika Kusini?”
“Ndiyo! Sijui wamekutana vipi lakini inaonyesha kwamba Bruno naye yupo Afrika Kusini,” alisema Alfred maneno yaliyomfanya kila mtu kushtuka.
“Afrika Kusini?” aliuliza Sharifa huku akionekana kutokuamini.
“Ndiyo!”
Hilo halikumuingia akilini hata kidogo, alijaribu kufikiria namna ambavyo mpenzi wake huyo kufika Afrika Kusini kutoka nchini Kenya, alijaribu kujifikiria na kuunganisha safari ya kufika nchini humo lakini alikosa jibu kabisa, alibaki akishangaa, aliuliza mara nyinginyingi na Alfred alimwambia vilevile kwamba alikuwa Afrika Kusini.
“Kuna kingine sasa! Kama unashangaa yeye kuwa Afrika Kusini, basi hili jingine utazimia,” alisema kijana huyo.
“Lipi?”
“Bruno ni bonge moja la bilionea!” alisema Alfred.
“Bilionea?” aliuliza Abdul.
“Ndiyo!”
“Kivipi yaani?”
“Huo ni umbeya niliopewa na Onyango, kawa bilionea kivipi, sijui, ila ni bonge la bilionea. Atakapotoka nchini Marekani, atakuja Kenya,” alisema Alfred.
“Nchini Marekani?”
“Ndiyo!”
“Sasa Alfred unatuchanganya. Umesema Afrika Kusini, ukasema ni bilionea, sasa hivi unasema nchini Marekani, mbona hueleweki?” aliuliza Sharifa huku akimwangalia Alfred kwa macho yaliyojaa mshangao mkubwa.
“Yaani hata mimi mwenyewe sikumuelewa Onyango mpaka pale aliponihakikisha kwamba jamaa kweli ni bilionea,” alisema.
“Kivipi?”
“Alimwambia Onyango kwamba anahitaji namba yangu ya akaunti ili akutumie pesa. Nahisi zitakuwa zimefika manake nimeona mlio wa meseji, nafikiri ni pesa hizo,” alisema Alfred.
“Mimi ndiyo sikuelewi kabisaaaa, naona kama unaongea Kirumi,” alidakia Abdul.
“Hebu subiri!” alisema Alfred, akaingia mkono mfukoni na kutoa simu yake.
Kulikuwa na ujumbe wa simu umeingia, hapohapo akaufungua na kuanza kuusoma. Uso wake ukajawa na tabasamu pana, baada ya hapo, akampa Sharifa ausome ujumbe huo, ulikuwa ujumbe mfupi uliosomeka ‘You have received 100,000 dollars from bank account number 0987225677890, (umepokea kiasi cha dola laki moja kutoka akaunti ya benki namba 0987225677890).
“Umeona! Amesema hizi pesa amezituma kwa ajili yako,” alisema Alfred, hilo likawachanganya zaidi. Wakahisi kama kile kilichokuwa kikiendelea kilikuwa ni ndoto ambapo baada ya mudua mfupi wangeamka na kujikuta wakiwa kitandani.
***
Gari liliseleleka mpaka kule korongoni ambako hakukuwa na urahisi kwa mtu kufika huko mpaka uzungukie sehemu nyingine ya mbali. Kila mtu alikuwa hoi na wote walikuwa wakitokwa na damu.
Bruno na Todd walikuwa kimya, damu ziliwatoka kichwani mwao na hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimeendelea mpaka kuanza kushambuliwa kwa risasi.
Walichokifanya ni kuanza harakati za kutoka ndani ya gari lile lililokuwa limegeuka chini juu, juu chini. Wakazisogeza maiti zile na kisha kufungua mlango. Mzee Bruno akaanza kutoka, alipoanza kusimama, akashangaa akishindwa kutokana na maumivu makali aliyokuwa akisikia mguuni.
“Aauughh..” alijikuta akipiga kelele.
Damu zilikuwa zikimtoka mguuni, alipoangalia vizuri aligundua kwamba alipigwa risasi ambayo ilizama kabisa ndani ya mguu wake. Alisikia maumivu ambayo hakuwahi kuyasikia kabla, akashindwa kabisa kusimama, ili kusonga mbele ilikuwa ni lazima kushikwa au kubebwa.
Haraka sana Bruno akateremka na kuanza kuelekea katika upande aliokuwa Todd na kumshika kisha kumpeleka pembeni. Akamlaza chini na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
Kitu cha kwanza kabisa alichotakiwa kufanya kilikuwa ni kuitoa risasi iliyokuwa katika mguu wa mzee huyo. Alishindwa kwa kuwa hakuwa na kifaa chochote kile hivyo kumwambia kwamba walitakiwa kuondoka mahali hapo kuelekea nje ya eneo la eneo hilo.
Akamshika kwa kuupitisha mkono wa mzee huyo kwenye bega lake na kuanza kuondoka mahali hapo. Walichukua nusu saa wakafika juu kabisa barabarani.
Hawakujua ni mahali gani walitakiwa kwenda, walichokifanya ni kuanza kuelekea upande wa Kaskazini ambapo waliamini kwamba hakukuwa na mtu yeyote hatari. Walitembea kwa mwendo mrefu, baada ya dakika ishirini na tano, wakaanza kupigiwa honi, walipoangalia nyuma, gari ndogo aina ya Vitz ilikuwa nyuma yao.
Gari hilo likasimama na dereva aliyekuwa humo ndani kuanza kuwaangalia, kwa jinsi walivyoonekana, ilionyesha dhahiri kwamba walikuwa wakihitaji msaada, akawafungulia mlango na kuwaambia waingie ndani.
“Nini kimetokea?” aliuliza dereva huyo huku akiwaangalia kupitia katika kioo cha mbele, aliwaweka kiti cha nyuma.
“Tulitekwa,” alijibu Bruno.
“Mlitekwa?”
“Ndiyo! Bosi wangu wakampiga risasi ya mguu. Tunaomba utusadie,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo.
“Haina shida. Nitawapeleka hospitali sasa hivi!”
“Hospitali?”
“Ndiyo!”
“Hapana! Naomba utupeleke sehemu yoyote ile lakini si hospitali,” alisema Bruno.
“Kwa nini? Mzee ana risasi mguuni, inabidi iende ikatolewe,” alisema dereva.
“Hapana! Naomba utupeleke popote pale.”
Bruno alimwambia dereva huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jonathan jinsi maisha yao yalivyokuwa hatarini. Alimwambia kuwa kulikuwa na mtu mwenye mkono mrefu alikuwa akiwatafuta, aliwatuma watu kwenda kuwamaliza lakini walishindwa na gari lao kupata ajali na kutumbukia korongoni.
Hakuishia hapo, aliendelea kumdanganya kwamba kama mzee Todd angepelekwa hospitali inamaanisha kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wao kwa kuwa jamaa huyo aliyekuwa akiwatafuta alikuwa na watu wengi, kila kona alikuwa amesambaza watu wake kwa leo la kumlinda na hata kumfanyia kazi.
Kidogo hiyo ikamuingia Jonathan, akatokea kuwaamini na kuwaambia kwamba angewapeleka nyumbani kwake. Safari iliendelea, baada ya dakika arobaini wakafika nyumbani hapo ambapo akawateremsha na kuelekea ndani.
Akamuita mke wake aliyeitwa Magdalena na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea, jinsi alivyokutana na watu hao nje mpaka kuomba msaada wake. Hilo halikuwa tatizo, kwa kuwa mkewe huyo alikuwa na ndugu yake aliyekuwa daktari akampigia simu na kwenda nyumbani hapo.
Baada ya dakika kadhaa, Sophiane ambaye ndiye alikuwa daktari aliyepigiwa simu akafika nyumbani hapo na kumwangalia mzee Todd aliyekuwa hoi kitandani. Akaangalia jeraha, akaandika vifaa ambavyo vilihitajika kwa lengo la kumfanyia upasuaji na kutoa risasi hiyo.
“Inahitajika randi elfu ishirini,” alisema Sophiane.
“Mbona kiasi kikubwa hivyo?” aliuliza Jonathan.
“Ni vifaa vya gharama kwa kuwa ni risasi ndiyo inayotakiwa kutolewa, ila pia vifaa hivyo haiviuzwi kiholela kwani serikali ilitangaza majeraha yote ya risasi yalitakiwa kutibiwa hospitalini,” alisema Sophiana huku akiwaangalia watu hao.
Jonathan hakuwa na pesa za kutosha ila hilo halikuonekana kuwa tatizo lolote lile, Bruno akamwambia kwamba pesa ilikuwepo na kitu kilichohitajika kilikuwa ni hivyo vifaa tu.
Yeye, Jonathan na Sophiana wakaondoka kwenda mjini ambapo huko Bruno akaenda katika mashine ya ATM na kutoa kiasi cha pesa kilichotakiwa na cha ziada kwa ajili ya matumizi yao na kumkabidhi Sophiana ambaye alikwenda na kununua vifaa hivyo tena kwa kutumia vyeti vya udaktari.
“Twendeni nikaanze kazi,” alisema mwanamke huyo.
Baada ya dakika kadhaa wakafika nyumbani hapo na kuanza kazi. Risasi ikatolewa, kila mtu akafurahi na mzee huyo kuanza kutibiwa nyumbani hapo na hata alipopona, Jonathan akawaambia kwamba maisha yao yalikuwa hatarini hivyo walitakiwa kukaa mahali hapo kwa mwezi mzima jambo ambalo halikuonekana kuwa tatizo.
“Kwa hiyo huu ni mwezi wa pili tupo Afrika Kusini! Nitarudi lini nyumbani kuwaonyesha wakina James kwamba sikufa?” alijiuliza. Mwezi huo pia wakatakiwa kukaa hukohuko Afrika Kusini.
***
Maxwell alikuwa na presha kubwa, alitaka kusikia kile kilichokuwa kimeendelea nchini Afrika Kusini. Hakutulia nyumbani kwake, muda wote alikuwa akipigia simu nchini humo na kutaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea.
Alitaka kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, na kwa sababu aliona kama kudharauliwa kwa kile alichokuwa ameagiza, alichokifanya ni kuwapigia simu vijana wake na kuwaambia wammalize Bi Juddie na mtoto wake, Martha.
Hilo halikuwa tatizo, vijana hao walipoambiwa hivyo, wakawachukua watu hao na kwenda kuwaua na kuitupa miili yao ufukweni mpaka pale polisi walipopewa taarifa na kwenda kuichukua.
Ilikuwa ni taarifa mbaya mno kwa kila mtu, hakukuwa na aliyejua kama kulikuwa na mtu aliyekuwa nyuma ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea, wengi walimchukulia mzee Todd kama muuza madawa ya kulevya lakini kwa kile kilichotokea kilimgusa kila mtu.
Moyo wa Maxwell ukaridhika lakini bado kichwa chake kilimfikiria huyo Todd, hakujua vijana wake walifikia wapi kwani kila alipowapigia simu alipewa majibu ambayo hayakumridhisha hata kidogo.
Siku zikakatika mpaka mwezi mmoja kumalizika, bado hakukuwa na kitu kilichoendelea mpaka pale alipopigiwa simu na kuambiwa kwamba vijana walikuwa njiani kwenda kutekeleza suala la kumuua mzee huyo kwani walipewa taarifa kwamba alikuwa hotelini.
Hilo lilimfurahisha na kuahidi kulifuatilia kwa karibu sana. Walipokuwa ndani ya gari, akawapigia simu, akaambiwa kwamba walikuwa na watu hao na hivyo walikuwa njiani kwenda kuwamaliza.
Moyo wake ukajisikia furaha ya ajabu, akakata simu, akachukua chupa ya mvinyo na kuanza kunywa huku muziki ukipiga taratibu kwenye redio yake sebuleni kwake.
Baada ya saa moja alipoona kwamba kazi ile ilifanyika, akaanza kuwapigia simu vijana wake ili apate mrejesho kama kazi ile ilifanyika au la. Alipiga simu, haikuwa ikipokelewa, iliita na kuita lakini hali ilikuwa kimya kabisa.
Hilo lilimchanganya, haikuwa kawaida kwa vijana wake kutokupokea simu zake, alihisi kwamba kulikuwa na tatizo na hivyo kupiga zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu haikupokelewa.
“Nini kinaendelea huko? Mbona hawataki kupokea simu zangu?” aliuliza, hakupata jibu, kichwa chake kilichanganyikiwa kupita kawaida.
Baada ya dakika kadhaa, akapiga tena simu, haikuita muda mrefu, ikapokelewa na sauti ya mwanamke kusikika upande wa pili. Huyo ndiye aliyemwambia kwamba kulikuwa na ajali mbaya ilikuwa imetokea ambapo watu waliokuwa ndani ya gari hilo walikuwa wamekufa wote.
“Wamepata ajali?”
“Ndiyo! Ila kilichowaua si ajali,” alisikika mwanamke huyo.
“Ni nini?”
“Risasi,” alipoambiwa hivyo, moyo wake ukapiga paa, hakuamini, aliuliza zaidi na zaidi kwa kudhani kwamba majibu yangebadilika lakini yaliendelea kuwa vilevile kwamba vijana wake waliuawa na gari kuingia kwenye korongo.
“Haiwezekani! Haiwezekani!” alisema Maxwell huku akiwa amechanganyikiwa. Itaendelea....

hadi baby shunie anichumu hahahha joking
 
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "


Season 1


Kama miezi miwili hivi iliyopita nilikuwa zangu katika mihangaiko yangu nje ya jiji la mbeya.


Usiku mmoja majira ya saa nne na nusu nikiwa chumba cha kulala wageni simu ikaita mie nikajua ni waif labda anataka kunitakia usiku mwema kwani nilikuwa sijaongea nae muda huo.


Kucheki nikaona ni namba ngeni, huwa sina mazoea ya kupokea namba ngeni ila nikasema ngoja nipokee pengine ni wenyeji wangu wa eneo lile.


Duu!! Ikatokea sauti moja laini sana ya kike tena inaonyesha alikuwa anajiandaa kulala na anataka kuongea na mpenzi wake zile chati kama wewe unayesoma unazopenda kuongea na mpenzi wako kwenye simu... usijifanye kama hujui...


Basi nikapokea na kabla sijaongea neno akaanza " Hellow Darling siku yako imeishaje, nimekumis sana na baridi hii hope utajilinda?"


Muda huo nikawa nashangaa maana sina kazi za nje kwa muda tangu nilipooa many years ago. Basi nikaona hapa nisijifanye kuuliza jina lake wala anataka kuongea na nani nami nikaanza kula naye sahani moja.


Aiseee yule binti ana sauti yaani dunia nzima, basi tukaongea kama nusu saa na tukaachana huku yeye akilala na mie nikiwa sasa nawaza huyu binti ni wa wapi na anataka nini kwangu au katumwa kupata data kutoka kwangu na waif.


Usiku ule sikupata jibu na asubuhi nilipotaka kumpigia simu ikawa haipatikni. Nikaendelea na kazi zangu na ilipofika usiku mida ile ile simu ikaita tena na sasa nikaongea nae kwa muda mrefu zaidi ya jana yake.


Tuliendelea kuongea kwa siku kadhaa mara nikarudi zangu home na kila ilipofika mida ile ya kuongea nikajifanya natoka kwenda kupata bia moja kumbe ili niisikie ile sauti ya binti wa kwenye simu ambaye hata jina naogopa kumuuliza kwani inaonkena twafahamiana na mie naelewa kuwa ni WRONG namba.


Binti alikuwa mtata na kuna wakati unaweza washa TV bila kutarajia hasa sauti na utaalamu wa maneno utafikiri ana kiwanda cha kuchapisha maneno matamu ya mapenzi mdomoni mwake.


Siku moja jioni mida ileile nikiwa najiandaa kupokea simu .......


Je, ni nini kilitokea wakati najiandaa kupokea simu?


Itaedelea kesho....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom