JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Mwananchi Digital imeripoti kuwa katika bandari ya Dar es Salaam kuna malori (magari makubwa ya mizigo) yamekwama kwa siku kadhaa hivyo kusababisha madereva wa maroli kulala na kuamka hapo hadi kufikia siku nne, madereva hao wamedai kulala na kula kwenye magari yao na kuomba kujisadia katika vyoo vya ofisi za jirani kwa kuwa hapo bandarini hakuna vyoo. Madereva hao wamedai chanzo cha uchelewashaji huo wa mizigo unatokana na ucheleweshwaji wa kupakua na kupakia mizigo na na ucheleweshwaji wa vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.
Kuna madai kuwa Takukuru wameingia nyumbani kwa Kakoko leo ghafla na kumkuta na begi lenye $1,625,800 taslimu baada ya kusimamishwa kazi jana! Haijulikani hizo alizichota lini, lakini kama ni kweli inawezekana alikuwa akizichota pole pole kwa muda mrefu kidogo na huenda sasa hivi ana 'vijisenti' vingi sana huko Jersey au Switzerland kama yule mzee. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha madai haya
Hayawi Hayawi sasa yamekuwa, ilianza kama kamchezo kakuigiza kutokupeana support za kupostiana kati ya Rayvan na wasanii wenzake wawasafi lakini utetezi ukawa mwingi, Ikafuata mama yake Boss wa Rayvan kumkatia Behewa Rayvan huko Instagram yaan Mama Dangote kumunfollow Rayvan. Zikaja Event zote kubwa za wasafi Ikiwepo EP ya FOA kutopostiwa na kijana huyo Shaban Mwakyusa Almaarufu kama Rayvan na Leo hii kaamua kukata Behewa kwenye Bio yake na kuondoa Taarifa iliyokuwa ikimtambulisha kama msanii wawasafi. Inasemekana Rayvanny kaondoka Wasafi. Hii ni kweli?
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia kwenye Jumatatu hii ya Pasaka , Kwamba Mheshimiwa Juma Raibu aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro , kabla ya kung'olewa hivi karibuni , ameanza kampeni kabambe ya kuondoa miundo mbinu yote aliyojitolea akiwa madarakani . Wakati wa madaraka yake alisaidia kutengeneza miundo mbinu ya maji kwenye uwanja wa Mandela uliopo Kata ya Pasua , ili kusaidia vijana wanaotumia uwanja huo , Sasa baada ya kung'olewa kwenye Umeya naye akaamua Kama Mmbwai basi iwe Mmbwai tu , kang'oa miundo mbinu yote ya maji aliyosaidia . Zipo Taarifa kwamba anapanga kung'oa mabati yote aliyosaidia kwenye mashule mbalimbali pamoja na Zahanati . Akijibu tuhuma hizo, Juma Raibu amesema: “Siwezi ondoa misaada...
CEO wa Simba sports club Barbara Gonzalez kuna tetesi akafungiwa miaka mitano 5 au maisha kujihusisha na michezo haswa football Hii imetokea baada ya yanga kupeleka malalamiko TFF kuhusu tuhuma alizozitoa kwa team hiyo inapokea wageni ambao Simba ilikua ikicheza nao champion league na shirikisho Imeelezwa kua TFF wakiongozwa na karia bado wana hasira na huyo CEO kwakua aliwabania deal la GSM la billion 2 ambapo wanao huyo mwana dada ni kikwazo kikubwa kwao kwenye mipango yao ya kupiga pesa
Inasikitisha sana tunapoona viongozi waandamizi wa nchi hasa wabunge wakikubali kununua cheap doctorates kutoka vyuo vya kitapeli (rogue colleges). Hiyo inakupa picha kwamba hawa viongozi wetu hawajui hata kuangalia authenticity wakati kila kitu kipo online. Kwanza hiki sio chuo maana hakina address, hakina majengo na wala hakina makao makuu yanayoeleweka. Ni taasisi ya kijanjajanja tuu iliyoanzishwa na matapeli kwa ajili ya kuwatapeli watu wanaotaka umashuhuri nafuu hasa wa udaktari bila kutumia jasho Hiki chuo kilichowapa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma na wenzake kina kashfa ya siku nyingi ya kuuza hizi degree za heshima. Ukweli ni kwamba wanauza na sio wanatoa bure ama kulingana na mafanikio uliyonayo katika nyanja husika...
Back
Top Bottom