JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa kauli yenye utata kuhusu Afrika, akisema, “Afrika ni makaburi kwa Waafrika. Inawezekanaje makaburi yakastawi?” Putin ameeleza kuwa Waafrika waliofanikiwa huweka fedha zao Uswisi, hupata matibabu Ufaransa, huwekeza Ujerumani, hununua bidhaa Dubai, hutumia bidhaa za Kichina, husali Roma au Mecca, watoto wao husoma Ulaya, na husafiri kwenda Canada, Marekani, na Ulaya kwa utalii. “Wanapofariki, huzikwa Afrika,” amesema Putin.
Kwenye hii video Manara anadai kuna Fact ambayo haisemwi kuwa Simba ilianza kuuza jezi na tiketi wiki 5 nyuma. Yanga wametumia wiki 1 tu kuuza tiketi na jezi na zimeisha, huku akisema kuna propaganda ambazo yeye alikuwa anatumia huenda ndio Simba wametumia kuonesha wamemaliza tiketi zao( Sold out) Anesena wana Yanga wajipongeze kwa kumaliza tiketi hizo kihalali. Je, Ni kweli Simba walianza kuuza Tiketi wiki 5 nyuma? Jamiicheck naomba msaada hapa tupate ukweli.
Picha hii inadaiwa kuchukuliwa maeneo ya Ubungo, Dar es Salaam. Inadaiwa kuwa twiga hawa wanasafirishwa kinyume cha utaratibu hivyo mamlaka za Serikali ikiwemo Polisi zifuatilie kwa undani suala hili. Kadhalika picha hiyo imetumika Oktoba 10, 2025 katika mtandao wa Instagram na kuelezwa kuwa "Muongoza watalii huko Zambia amekimbia na Twiga wawili na nyoka mmoja baada ya kuchelewesha kulipwa pesa zake"
Mei 29, 2023 kwenye Mtandao wa Twitter, Mtumiaji mmoja alichapisha andiko linalosomeka kuwa Mwaka 2016 Serikali Ilikataa kumpokea Balozi Mpya wa Zambia Nchini Tanzania Bwana Musenge Mukuma kwa kuwa Jina lake linatoa tafsiri Mbaya Katika Lugha ya Kiswahili. Andiko la aina hii liliwahi pia kuchapishwa Januari 1, 2023 kwenye Mtandao huohuo. Ukweli upoje?
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…